Namna Madaraka/Mamlaka ya utawala yanavyolindwa.

Yericko Nyerere

JF-Expert Member
Dec 22, 2010
16,987
20,271
Dunia kote kuna mamlaka, na vitabu vitakatifu vinasema mamlaka yote hutoka kwa Mungu, hiyo ni falsafa tu kwamba Watu ni Mungu, na Sauti yao ni ya Mungu.

Dola zote hulinda mamlaka ama madaraka yao, pasipo kufanya hivyo dola hiyo hupoteza udhibiti wa mamlaka hayo.

Kuna aina kuu nne za ulinzi wa madaraka amba ni:

1). Nguvu ya dola ambayo ipo kisheria (legal legitimacy).

2). Nguvu ya uongozi (Political legitimacy)

3). Nguvu ya kipropaganda (Propagated Legitimacy)

3). Nguvu za mtutu (Militias Legitimacy)

Naam, kila aina ya ulinzi wa madaraka ina aina za utendaji wake, na maranyingi hufuata alama za nyakati na watu unaowaongoza/tawala. Ili ujihakikishie udhibiti ni lazima uzingatie alama za nyakati na watu hao unaowadhibiti. Aina hizo ni kama hizi:

A). Nguvu ya dola ambayo ipo kisheria (legal legitimacy).

Udhibiti wa madaraka wa aina hii huwa katika Sheria ya udhibiti wa kisheria kwa madaraka ya utawala", ambayo ni moja ya hatua tatu za utungaji wa sheria za utawala za jamii yoyote mathalani Taifa, na huwasilishwa kwenye baraza ama bunge la umma ambalo ni idara ya utungaji sheria ya Taifa. Sheria hiyo ina lengo la kuweka utaratibu na kanuni kwa utekelezaji wa madaraka wa serikali, ili kupunguza hasara kwa watawala na kwa wananchi hadi kufikia kiwango cha chini kabisa, madhumuni ya utungaji wa sheria hiyo ni kuweka kanuni na udhibiti kwa madaraka ya utawala.

Ulazimishaji wa matumizi ya madaraka ya utawala ni vitendo vya kulazimisha vinavyofanywa na idara za utawala kwa ajili ya kuzuia vitendo vya ukiukaji wa sheria na kuhakikisha maamuzi ya kiutawala yanatekelezwa, na ni hatua za lazima zinazochukuliwa katika kulinda utaratibu wa jamii na maslahi ya umma.

Hivi sasa, kutokana na kukosa kigezo cha sheria cha namna moja, baadhi ya dola za utawala zinapotekeleza sheria, zinakosa mbinu madhubuti za kulazimisha kushughulikia baadhi ya vitendo vikubwa vya kukiuka sheria, na pia zinatumia ovyo hatua za kisheria za kulazimisha katika baadhi ya nyakati. Hivyo kuweka kigezo cha namna moja kwa mujibu wa sheria katika matumizi ya madaraka ni matakwa ya kutumia madaraka kwa mujibu wa sheria, na pia ni matakwa ya kulinda maslahi halali ya wananchi.

Wasomi na wanazuoni wa kileo duniani wamesema matumizi ya hatua za kulazimisha kwa idara za utawala ni "upanga wenye makali kuwili". Kwani yanaweza kuhakikisha wananchi wanatekeleza wajibu wa kisheria na kuchangia usimamizi wa serikali kuhusu utaratibu wa jamii na uchumi wa kimasoko; lakini kwa upande mwingine, yanaweza kutumiwa ovyo na kuathiri haki za wananchi.

Lengo la aina hii ya ulinzi wa madaraka kisheria ni kuhimiza kutumia madaraka kwa mujibu wa sheria na kulinda haki na maslahi ya wananchi. Matumizi ya hatua za kulazimisha ni mbinu ya kuhimiza watu husika kutekeleza wajibu wa kisheria, wala siyo lengo ovu. Dola za utawala duniani zinawaelimisha na kushawishi watu hao watekeleze wajibu wao kisheria.

Hapa madaraka yatalindwa kwa sauti na kauli ya watu wote lakini yakiwa kisheria. Mfumo huu ulitumika tangu karne 13 na kupungua ukali kunako karne ya 18, japo bado leo ungalipo na ndio msingi wa ulinzi wa madaraka.

B). Nguvu ya uongozi (Political legitimacy)

Njia hii mara nyingi ndio inatumiwa kuanzia karne 18 mpaka hivi sasa, Madaraka yanalindwa kwa kiongozi kupendwa na watawaliwa, mioyo ya watu inakuwa na kicheko kila kiongozi atokeapo mbele yao.. Mara nyingi viongozi hawa huwa wakuchaguliwa kidemokrasia, Na ulinzi wao huwa katika kutimiza matarajio ya Watawaliwa. Hapa ndipo huitwa utawala wa kidemokrasia.

C). Nguvu ya kipropaganda (Propagated Legitimacy)

Hii ni njia nyingine ya kulinda madaraka, ni njia mpya iliyoingia karne ya 20, Yani mnakuwa na dola inayotawaliwa na kikundi cha waongo (matapeli waliokubuhu). Utapeli wao ni dhidi ya umma. Serikali inayoshughulika na kupotosha ukweli kuwa uongo na uongo kuwa ukweli, yote kwa maslahi ya udhibiti wa madaraka hayo. Mfano Serikali inaweza kuutangazia ulimwengu kuwa Osama tumemuua, lakini haitoi ushahidi hata wa picha ya Simu ya Tecno tu kuonyesha mazishi yake, wakati juzi serikali hiyohiyo ilimnyonga Sadaam Hussein hadharani. Ama mnakuwa na serikali inayosema fulani kaenda kutibiwa ulaya kafia huko na kuzikwa huko, hata picha tu hakuna, Hii ni serikali ya kipropaganda, na inafanikiwa kulinda madaraka yake kwakuwa watu wake wengi ni WAJINGA.

E). Nguvu za mtutu (Militias Legitimacy)

Ulinzi wa aina hii kijeshi ulichipuka mwanzo mwa karne ya 13 na kuisha karne ya 20, nchi nyingi zilikuwa wa hanga wa mfumo huu wa ulinzi wa madaraka kijeshi, ndio mfumo ulioijenga Roma, ndio mfumo uliomwinua Nimrodi, Pamoja na kuwa ni mfumo uliopitwa na wakati na ni mfumo pumbazi wa taifa kiuchumi, lakini ndio mfumo uliomsimika Gadafi, ndio mfumo unaoiweka hai ZANU-PF, ndio mfumo unaoileo NRM, ndio mfumo unamwinua hai CCM ndii mfumo unaotawala mataifa yote masikini dunia hasa Afrika.

Njia hii mara nyingi hutumiwa na dola iliyoshindindwa njia zote tatu pale juu, na ikishindwa mfumo huu hatua inayofuata huwa ni kunywa damu za watu na kisha dola hiyo huondolewa kwa aibu madarakani na viongozi wake hunyongwa.

Wakati wa vuguvugu la ukombozi wa Afrika baada ya mvutano wa kanisa katoliki na Anglikana kwamba nani asimamie show ya uhuru, hatimae Katoliki walishinda na Anglikana wakalazimika kuunga mkono, ndipo ilipotokeza FABIAN SOCIETY, hii ilianzishwa na wenye fedha ulimwenguni chini ya Malkia Elizaberth kuhakikisha transformation badala ya revolution duniani..ndio waliombeba sana Mwalimu Julius Nyerere kumjenga alivyokua mwamini wa nguvu ya uongozi. MS Weaken alikuwa sehemu ya familia hiyo, ipo nyaraka ya urithi wake alomwandikia Julius Nyerere
 
Kwani hukusoma ufupisho darasa la pili. Sio uvivu wa kusoma bali nafukuzana na muda.
 
Hivi kila mtu akigoogle na kusoma mavitabu akileta hapa stori inaruhusiwa? Namimi ngoja nitaleta stori ya Gaddafi hapa tujifunze udiktekta wake.
 
Ndiyo maana Mungu akatuletea UKUTA ili kutulinda na hiyo nguvu ya mtutu, eeh Mungu tunakuomba utulinde
 
Duh,hapo kwa malkia ,halafu Nyerere...kuna ukweli aisee?Machale yananicheza,huwenda ikawa fabrication...by default siamini mpaka utoe ushahidi mkuu Yeriko...siamini mpaka proven otherwise!
 
Mkuu Yericko Nyerere, hizi topic za dizaini hii hazikufiti, endelea na zile za UNAFIKI, ndo type yako, tumekuzoea na hizo za leo A ni poa B mbaya kesho A ni mbaya B ni poa!
 
Duh,hapo kwa malkia ,halafu Nyerere...kuna ukweli aisee?Machale yananicheza,huwenda ikawa fabrication...by default siamini mpaka utoe ushahidi mkuu Yeriko...siamini mpaka proven otherwise!
Unataka ushahidi wa Malkia, katoli na Nyerere dhidi ya uhuru au unataka urithi wa Nyerere kwa Malkia?

Jipe muda wa kusoma maandiko na machapisho mengi
 
Back
Top Bottom