Namna hii wizi utaisha Tanzania ?

Salahan

JF-Expert Member
Sep 10, 2014
2,963
3,675
Katika zoezi la kupiga picha za vitambulisho vya shule, mpiga picha alimwambia mwalimu mkuu kwamba picha moja ni 500 kwa kila mwanafunzi.. Mwalim mkuu akawaambia walimu wa darasa kuwa wawaambie wanafunzi walete 1000 kila mmoja wao kwa ajili ya picha.. walimu wa madarasa wakawatangazia wanafunzi kuwa kila mmoja alete 1500 kwa ajili ya picha.. watoto wakasema kwa mama zao wao kuwa kuna kupiga picha na gharama ni 2000. Mama sasa kwa baba wa familia.. " Baby hizi shule za siku hizi kwa kupenda pesa.. kuna mchango wa picha 5000 mpenzi wangu mtolee mwanao apate kitambulisho.."

Asa namna hii wizi utaisha Tanzania ?
 
Hahahaha kama Mimi ndo baba nitapeleka mwenyewe shule sio kwa usawa huu wa magu
Kuna mdingi mmoja alifanya kama unavyosema, aisee madhara yake yalikuwa makubwa hata kwa tusiohusika.
Ilikuwa hivi: Tulikuwa na tour ya kishule kwenda Nairobi toka hapa Tz na tukawa tumekubaliana na Rector wa shule tuchangie 50,000/- tu kila mwanafunzi gharama zingine zote shule ingelipa ila dogo mmoja kaenda kwao kaomba 600,000/- baba yake kaomba deadline ya kupeleka hiyo shule then akamwambia dogo nitakutumia dogo kaja shule.
Siku ya siku (deadline) ilipofika mdingi katua shuleni moja kwa moja kwenye ofisi ya rector na mzigo wote 600,000/- akampa rector, rector bila kujua akadhani ni ada ya shule akafungua document za dogo kujua anadaiwa ngapi cha ajabu akakuta hadaiwi akamuuliza baba mtoto ya nini hii pesa mdingi akasema mwanae amemwambia wewe (rector) umewaambia wachangie 600,000/- kwa ajili ya tour. Rector akachanganyikiwa mzungu wa watu akaagiza dogo aitwe ...
 
Mkuu endelea mbona kama nimeielewa hii
 
Noma sana hebu malizia huo utamu...
 
Noma sana hebu malizia huo utamu...
...baada ya kuitwa dogo akaulizwa ile 600,000/- ni kwa ajili ya nini aliomba? akiwa hajitambui akasema hakuomba hiyo isipokuwa 50,000/- tu mdingi kusikia maneno ya mwanae akamrukia akaagza kiboko dogo akachezea viboko vya kutosha then mdingi akarudi na hela yote.
Rector akamleta dogo class akiwa analia shati jeupe la shule likiwa na michirizi ya kijani ya viboka; akatusimulia ujambazi aliofanya dogo kwa babake na papo hapo akatangaza kufuta safari nzima kwa kuhofia kufilisiwa kwa wazazi na ndo safari yetu ikaishia hapo.
Mbali na huyo jamaa mimi mwenyewe nilikuwa nimepewa 750,000/- kwa pamoja na dada na baba yangu baada ya kuwaarifu kuwa nitakuwa naenda Kenya. Baada ya safari kupigwa chini mtihani ulihamia kwangu nizirudishe ama nizile ila baadae nilirudisha 150,000/- kwa baba nyingine nikala na kununua nokia N92 zikiwa ndo zimetoka na zikipatikana kwa waaraau waenda Dubai tu
 
Umetshaa mkuu
 
Back
Top Bottom