Namna hii dada zetu watasalimika mikononi mwa Polisi....

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Mar 10, 2006
33,475
39,991
Katumiwa ujumbe na afande; ameshindwa kujibu -- akubali au akatae. Ilikuwa ni mfululizo wa SMS

SMS 1 - Unajua nakuthamini zaidi ya POSHO na MSHAHARA, bila wewe siwezi kuishi ni sawa na kukosa BUNDUKI eneo la tukio lako mpenzi wangu.

SMS 2 - Usiniweke roho juu kama yanavyoniweka maandamano ya CHADEMA

SMS 3 - Nitakuheshimu kama ninavyoliheshimu LINDO, wewe ndio IGP wa moyo wangu, daima nitakuweka mbele kama kama LIGHT MAKER kwenye gwaride. Mbona uko kimya.

SMS 4 - Nijibu basi nipate kufungua JALADA ndani ya moyo wako. Usinifanye moyo ukaenda mbio kama DEFENDER MPYA, ntakuwekea usalama kama msafara wa RAIS; nina RB ya mapenzi.

Ungekuwa wewe mdada ungesemaje...???
 
Ha! ha! haa! Kwa nondo hizi, hawezi salimika mtu! Tutashuhudia manyoya tu. Na ukiona manyoya ujue kesha liwa!
 
Nimeipenda hiyo namba 2 "Usiniweke roho juu kama yanavyoniweka maandamano ya chadema"
 
whaat.. watu walidhania hii ni joke? this is serious mwenyewe kaimbisha anasubiria jibu
 
Tatizo kubwa la Polisi wetu wao wana mkono wa kupokea tu hawajazoea kutoa, ndio maana hata Dada zetu hawako interested nao, wewe imagine anaingia Bar na mrembo lakini hata bia anataka anywe za kumboom mwenye Bar ili usiku wakipitisha muda wakufunga asiwaletee Defender.
 
Hahahahaaaaa! Ungemalizia Baada ya Kutoswa

SMS 1. Ujue wewe nakushuku razima unajihusisha na bishara ya mibange!!! Twende kituoni ukatoree maerezo!
SMS 2. Ore wako nijue unajivinjari na nani, Nitarimwngosi mwenyewe na ribunduki rangu!
 
SMS 1 - Unajua nakuthamini zaidi ya POSHO na MSHAHARA, bila wewe siwezi kuishi ni sawa na kukosa BUNDUKI eneo la tukio lako mpenzi wangu.

SMS 2 - Usiniweke roho juu kama yanavyoniweka maandamano ya CHADEMA

SMS 3 - Nitakuheshimu kama ninavyoliheshimu LINDO, wewe ndio IGP wa moyo wangu, daima nitakuweka mbele kama kama LIGHT MAKER kwenye gwaride. Mbona uko kimya.

SMS 4 - Nijibu basi nipate kufungua JALADA ndani ya moyo wako. Usinifanye moyo ukaenda mbio kama DEFENDER MPYA, ntakuwekea usalama kama msafara wa RAIS; nina RB ya mapenzi.

MMM hapa umetuletea jambo!
Kweli wadada wanajionea mambo na vituko wanapoimbishwa. Imagine hapo anaimbishwa na askari wa kawaida, sijui meseji za mgambo au mwanajeshi zitakuwaje?! Ningetamani pia kumvizia na kumuona daktari naye anaimbisha, ningeshangaa zaidi kuona sms za kiongozi wa dini naye akifanya zoezi hilo hilo, sijui watatumia verse kwenye kuimbisha?! Na konda je? Na huyo msukuma mkokoteni? :A S embarassed:
 
Huyo dawa yake kumjibu 'nakuoenda kama chadema. Uje umevaa gwanda nikakuchukulishe kadi ya chadema' uone atakavyokimbia.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom