Namna gani ya kukabiliana na changamoto za kwenye mitandao?

M'Jr

JF-Expert Member
Jul 8, 2011
3,743
2,000
Kutokana na kukua kwa teknolojia, socialization imekuwa rahisi sana siku hizi.

Tofauti na zamani ambapo njia kuu ya kukutana ilikuwa physical, siku hizi njia kuu ya kukutana na watu imekuwa digital, kwa maana ya kutumia mitandao na njia nyingine zinazoendana na hizo.

Kukutana huku kumekuwa kunapelekea kuanzishwa kwa mahusiano ndani ya mitandao hii. Hata hivyo, pamoja na makutano haya ya mtandao kuongezeka na kuendelea kukua kwa kasi, bado yamekuwa yakikumbana na changamoto nyingi kubwa ikiwa mindset ya watu wengi kuwa kwenye mfumo wa zamani pamoja na kwamba wanapractice mfumo mpya.

Kwa mfano, imekuwa ni aghalabu kwa watu waliokutana online na kuwa wapenzi kutangaza hadharani kuwa wamekutana online, hii inachangiwa sana na baadhi ya watu kudhani kuwa hakuna mahusiano ya kweli yanayopatikana kupitia mitandao.

Sasa wengi wetu hapa tumetumia mitandao kwa muda sasa, na katika muda huo tumeshajikuta kwenye mahusiano mara moja au zaidi ambayo yamekutana na changamoto hizi na zile kwasababu tu yametokea kwenye mtandao, tunaweza kushare changamoto hizo na namna gani ya kukabiliana nazo?

Mada mezani
 

M'Jr

JF-Expert Member
Jul 8, 2011
3,743
2,000
Out of Topic: Long time no see u, mzima?

Mi mzima hofu na mashaka ni kwako uliye mbali na upeo wa macho yangu. Juzi nilikuona kwenye sredi Fulani hivi nikakosa pozi la kukupa hi. Nilikumiss though.... Kongosho
 
Last edited by a moderator:

Apologise lady

JF-Expert Member
Sep 16, 2013
5,981
2,000
Ni mahusiano kama mahusiano wanayokutana sehemu yoyote, mimi nadhani jambo baya ni wengi huwa si wakweli yaani bado watu wapo kitoto kitoto, lets say mtu anaishi sehemu tofauti na mke/mume wake anajitambulisha kuwa yuko single na mtu wa hivi hadi mtu uje kugundua kuwa ni mtu mwenye mke/mume inachukua muda sana.


Ila ukweli ni mahusiano ambayo ukimkuta mtu mwaminifu anayejitambua, anayejielewa utafurahi na utasahau shida zoteeeee.
 

M'Jr

JF-Expert Member
Jul 8, 2011
3,743
2,000
Ni mahusiano kama mahusiano wanayokutana sehemu yoyote, mimi nadhani jambo baya ni wengi huwa si wakweli yaani bado watu wapo kitoto kitoto, lets say mtu anaishi sehemu tofauti na mke/mume wake anajitambulisha kuwa yuko single na mtu wa hivi hadi mtu uje kugundua kuwa ni mtu mwenye mke/mume inachukua muda sana.


Ila ukweli ni mahusiano ambayo ukimkuta mtu mwaminifu anayejitambua, anayejielewa utafurahi na utasahau shida zoteeeee.
Kwa mfano ukijikuta kwenye mahusiano ya namna hii, unaweza kusimama na watu ukawaambia kwa mfano "Huyu tulikutana JF"? bila kuhisi vinyweleo kukusimama?
 

Apologise lady

JF-Expert Member
Sep 16, 2013
5,981
2,000
Kwa mfano ukijikuta kwenye mahusiano ya namna hii, unaweza kusimama na watu ukawaambia kwa mfano "Huyu tulikutana JF"? bila kuhisi vinyweleo kukusimama?


Ndio nitasema, hata mpenzi niliyenae nilikutana nae jamiiforums na maisha yako byeeeeee, ninafuraha kila siku, sijawahi kujuta.
 

Bavaria

JF-Expert Member
Jun 14, 2011
50,654
2,000
Mahusiano ya mitandao hayana ubaya wa aina yeyote kama mmependana...
Na haina tofauti na kukutana na watu wengine mtaani...
Kikubwa ni kuwa na upendo wa dhati...
Ukiona mtu analeta utoto basi hajajiandaa kuwa kwenye mapenzi ambayo hata angekutana na mwingine mtaani ange behave hivyohivyo...
 

kijani11

JF-Expert Member
Jan 19, 2014
7,171
2,000
Mahusiano ya mtandaoni watu wanakuwaga na hofu nayo kwa sababu kuna nafasi kubwa sana ya mtu kuweka taarifa zisizo sahihi kwa lengo la kufanya avutie,

Pia nchi zilizoendelea wapo watu wametumia njia hizi kuwatapeli watu, na kuwafanyia matukio mengine ya kinyama kwa kuanzisha mahusiano na wadada/wakaka na mwishowe kuwapeleka sehemu za kukutania na kuishia kuwabaka au hata kuwaua.

Kingine kinachoogofya watu ni kujiuliza huyu huko alipo anapokuatana na watu kila siku ameshindwaje kupata mwenza je ana kasoro gani?

Pia kumekuwa na story/matukio ya watu kusema nilichati na mkaka/mdada siku ya kuonana naye ilibidi nitafuute uchochoro wa kujificha maana alikuwa mzee/mnene sana/mwembamba sana n.k tofauti ya nilivyotarajia.
 

Coran

Member
Jan 26, 2014
62
95
Mahusiano ya mitandaoni hayana tofauti na mengne kama mtaridhianaa na kila siku utajiona mwenye Furaha
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom