Namna gani unaweza kukabiliana na mawazo kipindi hiki cha CoronaVirus

JamiiTalks

JF Advocacy Team
Aug 7, 2018
128
500
1. Ni kawaida kuhisi huzuni, kupata mawazo, kuchanganyikiwa, kuogopa au kuwa na hasira wakati wa matatizo. Ongea na watu unaoamini watakusaidia. Wasiliana na familia yako au marafiki

2. Kama ni lazima ukae nyumbani, kuwa na maisha yenye afya ikiwa ni pamoja na kula lishe sahihi, kulala, kufanya mazoezi na na kuongea na failia yako nyumbani na watu wengine kwa kutumia simu au barua pepe

3. Usitumie sigara, pombe au dawa nyingine kushughulikia hisia zako. Ikiwa unahisi umezidiwa, zungumza na Wataalamu wa Afya. Kuwa na mpango wa wapi pa kwenda na jinsi ya kutafuta msaada kwa mahitaji ya kiafya kama itahitajika

4. Pata ukweli. Kusanya taarifa zitakazo kusaidia kuamua kwa usahihi hatari iliyopo ili uweze kuchukua tahadhari inayofaa. Tafuta chanzo cha kuaminika kama WHO, Wakala wa Serikali au kingine cha kuaminika

5. Punguza wasiwasi na kufadhaika kwa kupunguza muda aambao wewe na familia yako mnatumia kuwangalia au kusikiliza Chombo Cha Habari ambacho habari zake unaona zinakera
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom