Namna gani text sms, picha na video za whatsapp na telegram zinavyojaza memory ya simu

Mnyamahodzo

JF-Expert Member
May 23, 2008
1,932
987
Habari za kutwa wakuu.
Naomba msaada wa kuelemishwa athari za mitandao ya kijamii katika kupunguza uwezo wa kutunza kumbukumbu wa simu. Mitandao ya kijamii ninayohitaji kujua zaidi ni Whatsapp na Telegram ambayo inazidi kuwa na watumiaji wengi kwa pamoja yaani magroup. Imenitokea mara kadhaa nashindwa kutumia whatsapp napata ujumbe ya kwamba nipunguze picha ama video katika simu yangu ndipo nitaweza kutumia whatsapp. Sasa hoja yangu inakuja, katika matumizi ya mitandao hii ya kijamii ni kwa namna gani inajaza uwezo wa kutunza kumbukumbu wa simu yangu? Na nini nifanye ili niwe nasimu yenye uwezo wa kumbukumbu mzuri? Nitafura sana nikijulishwa athari za sms, picha na video katika hilo hapo juu...yaani athari ya kipengere kimoja baada ya kingine.
Nashukuru sana kwa kuelewa na kupewa msaada.
 
Fungua memory ya simu nenda Whatsapp kisha fungua file la media then fungua image futa file la sent



Fanya hivohivo na kwa sent videos
 
unatumia simu gani? ni ngumu kulijibu hilo swali bila kujua aina ya simu unayotumia
 
unatumia simu gani? ni ngumu kulijibu hilo swali bila kujua aina ya simu unayotumia
Mkuu hivi kwa nini folder la whatsapp halikai kwenye SD card mara zote linakaa kwenye internal Memory ya Simu hata nikili move kwenye Sd card lkn suddenly linarudi kwenye internal memory msaada wako.
 
nunua memory yenye uwezo mkubwa kuanzia gb 4,8,16 au 32, nenda kweye setting then tafta memory setting, weka default writting memory chagua SD,
then nenda file manager umove,( usicopy) mafile ya picha na video kutoka kwenye internal memory kwenda external memory, kama ukikopy bas ukimaliza futa picha na video kwenye phone memory, kingine move installed kwenda kwenye SD, hiyo itasaidia kuongeza free space kwenye internal memory.
 
Chief, mimi natumia Samsung focus, OS~window.

simu yako uwezo wake wa kuhifadhi kumbukumbu ni 8gb na kati ya hizo around 5gb ndio inakuwa unaweza kuzitumia.

5gb inaathirika vipi na whatsapp na telegram?
assume picha 1 ni kb 100, video 1 ni mb10 na voice 1 ni mb5

5gb inaweza hifadhi video 500 au picha 50,000 au voice(miziki) 1,000

unapokuwa katika group vitu hivyo hapo juu hutumwa sana hivyo ni jambo la kawaida simu yako kujaa baada ya miezi kadhaa.

njia za kutatua tatizo

-ingia whatsapp halafu nenda setting then kwenye media auto download eka off vyote, hii itasaidia vitu vikitumwa na watu visidownload hadi utakapoamua wewe,

-tafuta simu nyengine yenye kumbukumbu kubwa zaidi atleast 16gb kwa dunia ya sasa unakuwa na ahueni kidogo.

kuhusu idea ya memory card achana nayo simu yako ni windows phone za zamani sidhani kama utaweza hamisha vitu vya whatsapp vije kwenye memory card
 
Mkuu hivi kwa nini folder la whatsapp halikai kwenye SD card mara zote linakaa kwenye internal Memory ya Simu hata nikili move kwenye Sd card lkn suddenly linarudi kwenye internal memory msaada wako.
baadhi ya simu linakaa kwenye external memory card, wanajua wenyewe whatsapp wanatumia kigezo gani. kipindi unaeka hio whatsapp memory card ilikuwa kwenye simu?
 
baadhi ya simu linakaa kwenye external memory card, wanajua wenyewe whatsapp wanatumia kigezo gani. kipindi unaeka hio whatsapp memory card ilikuwa kwenye simu?
Ndiyo mkuu natumia HTC desire 816 folder la whatsapp halikai kwenye memory card hata niki remove suddenly linarudi kwenye internal memory ya simu.
 
Ndiyo mkuu natumia HTC desire 816 folder la whatsapp halikai kwenye memory card hata niki remove suddenly linarudi kwenye internal memory ya simu.
jaribu kutafuta solution nyengine za kawaida ikishindikana zipo apps zinamount folder la whatsapp kwenye memory card, kila kitu kinachoingia automatic kinahamishiwa kwenye sd card ila nahisi kwa kiasi fulani ita affect perfomance ya simu sababu kutakuwa na mihamisho miwili ila unaweza test.

hii app inahitaji root na ipo playstore search folder mount
 
Back
Top Bottom