Namna Duwasa-Dodoma Ilivyopoteza Mwelekeo Baada Ya Serikali Kuhamia Dodoma

1987SANAWA

JF-Expert Member
Nov 29, 2013
332
500
Habari za mchana! Miaka ya 2016 kurudi nyuma Mamlaka ya maji safi Dodoma(DUWASA) ilikuwa inafanya vizuri sana Kwa kuwa matumizi ya maji hayakuwa makubwa sana na hii ilipelekea wawazuie baadhi ya wasambazaji Wa Huduma za maji kama water project iliyokuwa inasambaza maji maeneo ya Miyuji proper Kwa kutumia mamlaka yake ya kiserikali,

Lakini kwasasa hali ni tofauti kabisa, maeneo kadhaa hususani Miyuji proper kuna shida kubwa ya maji, ukienda kuwaambia ofsn kwao yanaweza kutoka siku mbili mfululizo kisha yanapotea mwezi mzima.

Napenda kuwashauri DUWASA kama maji hayatoshi waweke mgao Kwa baadhi ya maeneo isipokuwa sehemu muhimu zaidi kama mahospital na mijini ambapo shughuli zinapamba moto muda wote, maeneo mengine waweke migao ikibidi maji yatoke walau Mara mbili Kwa wiki na ratiba ifahamike.

Maji yanatutesa sana+Corona ni shida juu ya shida. Na kama wameshindwa kabisa wawaruhusu water project watusambazie maji.

Mchana mwema wakuu
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom