SoC01 Namna bora ya Waajiri kuwakomboa Watumishi wao na kadhia ya madeni katika Taasisi za Kifedha

Stories of Change - 2021 Competition

Mwadilifu Mdhulumiwa

JF-Expert Member
Jul 22, 2021
418
630
Utangulizi

Kwa muda mrefu kumekuwapo na kilio cha watumishi wa umma na taasisi za binafsi wakilalamikia masharti magumu wanayokumbana nayo katika taasisi za kifedha nchini ikiwemo riba kubwa za mikopo wanayoomba kwenye taasis hizo.

Mabenki na taasisi hizo humvutia mkopaji kwa kumuwekea utaratiu wa kulipa deni lake kidogo kidogo kwa muda wa miezi au miaka kadhaa ili kumfanya aamini kuwa mkopo huo ni nafuu lakini kiuhalisia hakuna mkopo wa riba wenye unafuu kwani ukipiga hesabu ya marejesho yote kwa muda husika unawezakuta mkopaji amelipa zaidi ya 100% ya kiasi alichokopeshwa.

Pia kuna ujanja ujanja mwingi ambao mabenki na taasisi ndogondogo za kifedha huwafanyia wakopaji wanapoingia nao mikataba sababu wengi wao hawana uelewa mzuri juu ya sheria za fedha na mikataba ya kibiashara.

Mathalani unaweza kukuta mkopaji amekopeshwa kiasi cha Tshs 1,000,000/= , lakini anaambiwa kwenye mkataba ajaze kakopeshwa 1,500,000 alafu anapigiwa riba ya mkopo kutoka hapo kwenye kiasi hicho ilihali mkononi kapewa 1,000,000 tu!

Pia kuna wizi unaofanywa na mabenki ya umma kupitia mikopo inayoitwa Top Up. Hii ni mikopo ambayo mkopaji anakuwa ana deni lingine analoendelea kulipa, anapewa mkopo mwingine juu ya ule mkopo wa awali.

Katika kuumpatia mkopo huu mabenki humtaka muhusika kukopa kiasi kinachozidi mkopo wake wa awali ili aonekane ametumia mkopo huo kulipa deni lote la awali na abakie na salio flani.

Mathalani mtumishi anaweza kuwa awali alikopeshwa 10,000,000/=, ambapo deni zima likasoma 23,000,000/=, Baada ya miaka 3 akienda benki na kufanya top up,

Hapa kwanza atauliza benki kiasi halisi anachodaiwa hadi kufikia muda huo. Hapa mabenki mengi huwa hawaongei ukweli, unaweza kuambiwa bado unadaiwa 9,200,000/= wakati umeshafanya marejesho kwa karibu nusu ya muda wa deni na deni zima limepungua toka 23,000,000 hadi 14,000,000.

Ili apate kiasi flani kwenye mkopo wake wa top up, inabidi mkpaji aombe kukopeshwa kiasi flani ambacho ni zaidi ya 9,200,000, mfano 11,000,000, Hapa deni lake litapaa upya kutoka 14,000,000 mpaka 25,000,000 huku mkononi akiambulia 1,500,000/= tu !

Kwa hiyo ukiangalia utaona kuwa alichokopeshwa mtumishi hapa ni 1,500,000/= tu, lakini deni lililoongezeka ni karibu 11,000,000/= .

Kutokana na ukubwa huu wa deni, mtumishi husika hubakia akiendelea kwenda kufanya hiyo top up kila anapofikwa na shida za gharama .

Matokeo yake deni hili humuandama mtumishi mpaka kustafu kwake ambapo hufyeka mafao yake ya kiinua mgongo na kumfanya mtumishi husika kustafu akiwa masikini.

Katika bandiko hili nitajadili sababu zinazopelekea watumishi wa umma na binafsi kujikuta wakizama katika dimbwi la madeni ya mabenki na namna bora ya waajiri kuwakomboa na kadhia hiyo.

Sababu Za Watumishi Wengi Kuzeeka Na Mikopo

Miongoni mwa sababu zinazochangia watumishi wengi wa umma kujikuta akizeeka na mkopo unaomfuata mpaka kwenye mafao yake ya uzeeni ni pamoja na hizi zifuatazo:-

Usimamizi Mbovu Wa Sekta ya Fedha

Ufuatiliaji na uthibiti wa huduma zinazotolewa na taasisi za kifedha umekuwa hafifu sana pamoja na uwepo wa sheria, kanuni na miongozo mbalimbali ya serikali.

Hata pale kiongozi mkubwa kama Rais au Waziri mkuu anapokuwa akizindua tawi flani la taasisi ya kifedha na kuyataka mabenki nchini kupunguza masharti ya mikopo na viwango vya riba wanazotoza wananchi lakini utekelezaji wa maagizo haya na miongozo mingine umekuwa ni wa kusuasua sana.

Mfano ipo sheria ya huduma ndogondogo za kifedha ya mwaka 2019 ambayo ilitungwa ili kuthibiti mikopo umiza katika taasisi ndogo ndogo za kifedha, lakini mpaka sasa hakuna unafuu wowote wa mikopo kwenye taasisi hizo. Mteja anaweza kukopeshwa milioni 5 baada ya miezi 6 akalipishwa milioni 10. Sheria ipo na wasimamizi wapo lakini hakuna ufuatiliaji.

Viongozi na Wanasiasa Wengi Kujiingiza Kwenye Biashara ya Fedha

Uchunguzi unaonyesha kuwa sehemu kubwa ya wanasiasa tena wenye mamlaka ndani ya taasisi na vyombo vya serikali ni wafanya biashara wenye hisa katika makampuni na taasisi nyingi za kifedha. Hali hii husababisha mgongano wa kimaslahi pindi suala hili linapofikishwa mbele ya vyombo wanavyovisimamia.

Mathalani wabunge wenye hisa katika mabenki na makampuni yanayofanya biashara ya kukopesha fedha hawawezi kuchangia hoja kinzani za kuzibana taasisi hizi pindi mjadala unaohusu suala hili unapofikishwa bungeni.

Uwezeshaji Mdogo Wa Waajiri Kwa Watumishi Wao.

Pamoja na kuwa watumishi wa umma na binafsi ndio wawezeshaji wa sekta zote katika uendeshaji wa shughjuli za kila siku, lakini waajiri hawa wamekuwa wakitekeleza mipango na miradi yao ya maendeleo kwa kuyalenga tu mazingira ya majengo na ofisi anapofanyia kazi mtumishi lakini masilahi ya mtumishi atakaye hudumia ofisi hizo yakiachwa nje ya miradi hiyo.

Mathalani katika utekelezaji wa miradi mikubwa ya mpango wa kuboresha Elimu ya msingi(MMEM) na Mpango wa kuboresha Elimu ya Sekondari(MMES), majengo ya shule nyingi za msingi na sekondari nchini kote yalikarabatiwa na kuboreshwa, lakini mwalimu ambaye ni mdau wa moja kwa moja katika sekta hii hakuna alichowezeshwa katika miradi hii.

Angalau miradi hii ingekuwa na manufaa zaidi kama ingeambatana na kuwakopesha walimu vifaa vya usafiri na ujenzi kama magari, mabati, saruji, nondo n.k.

Ubinafsi Mwingi Kwa Wanaopewa Mamlaka ya Kuwasimamia Watumishi Wenzao

Uchunguzi umeonyesha kuwa ndani ya taasisi nyingi za umma kuna usiri mkubwa juu mafungu ya fedha za uwezeshaji yanayotolewa na serikali kusaidia watumishi kujikomboa kiuchumi. Mathalani kuna fungu la fedha hutolewa na hazina kwa Halmashauri zote nchini ili kusaidia watumishi kujikomboa kiuchumi.

Lakini ukiwauliza watumishi kuhusu fedha hizo wengi wao hawafahamu chochote! Hata kwa zile Halmashauri ambazo taarifa ya fedha hizo hutolewa lakini pia wakubwa wa taasisi hizo hujenga mazingira ya kuhakikisha wanazifaidi wao peke yao huku watumishi wa kawaida wakiambulia kidogo sana au wasipate kabisa.

Mathalani mwaka 2018, hazina walitoa jumla ya shilingi 300,000,000, kwa ajili ya kuwawezesha watumishi wa Halmashauri flani huko mkoani Rukwa.

Katika fedha hiyo, mkurugenzi na mweka hazina kila mmoja akajikatia 40M, kisha wakafuatia wakuu wa idara na vitengo 20M, 15M , 10M na kuendelea, alafu Ili kujenga mazingira ya kupruni wakopaji, uongozi uliweka masharti magumu ya vigezo vya kukopesheka kama vile kusema mtumishi anayestahili kukopeshwa ni yule tu asiye na mkopo katika benk za umma au asiwe amebakiza 1/3 ya mshahara ghafi anaochukua.

Lakini ukilitazama suala hili kwa umakini utagundua kuwa hawa wote waliojikatia fedha hiyo tangu mkurugenzi hadi wakuu wa vitengo, kiuhalisia hawa ndio hawakuwa na vigezo vya kukopeshwa fedha hizo bali watumishi wa kawaida, kwakuwa mkurugenzi na wakuu wa idara na vitengo wao wana mishahara yao mizuri na posho ndefu za kila mwezi wanazoita ni stahiki zao za kisheria.

Zaidi ya yote, watumishi wenye madeni kwenye benki za umma ilitakiwa fedha hiyo ingenunua hayo madeni alafu makato yao yahamishiwe hazina au halmashauri ili kuwapunguzia mzigo wa madeni.

Kukosekana Kwa Sheria Mathubuti Za Kuboresha Maslahi ya Watumishi.

Mpaka sasa hakuna sera wala sheria yoyote inayomlazimisha mwajiri kuboresha maslahi ya mtumishi wake. Bali kilichopo ni kama hiari ya mwajiri kuboresha au kutoboresha maslahi ya mtumishi kutegemeana na hali yake ya kiuchumi au jinsi anavyoguswa na hali za watumishi wake.

Hali hii imetoa mwanya kwa waajiri wengi kupuuzia kuboresha maslahi ya watumishi wao huku wakibakia kutunga sababu za kila wakati.

Demokrasia Isiyo Rafiki Kwa Watumishi wa Umma

Sheria ya uchaguzi inayotawala mchakato wa kugombea nafasi mbalimbali za kisiasa zenye maslahi mazuri kiuchumi, kama vile udiwani, ubunge n.k, imekuwa sio rafiki kwa watumishi wa umma.

Sheria hii inatamka kuwa mtumishi wa umma akishateuliwa tu na chama chake kugombea wadhifa wowote wa kisiasa, utumishi wake unakuwa umekoma siku hiyohiyo, pasipo kujali kama mtumishi husika atashinda katika uchaguzi huo au la!

Kimsingi matakwa ya sheria hii yanawalazimisha watumishi kustaafu au kuacha kazi zao kwa lazima badala ya kuwapa haki ya kutafuta fursa za uongozi na papo hapo wakalinda nyadhifa zao za kiutumishi mpaka pale wanaposhinda na kuapishwa kushika nyadhifa nyingine za uongozi.

Nini kifanyike Kuwakomboa Watumishi Wetu na Madeni ya Taasisi za Fedha?

  • Kiundwe chombo maalum kwa ajili ya kuthibiti usimamizi na uendeshaji wa taasisi zote za kifedha.
  • Zitungwe sheria kali zitakazowabana wanasiasa kutojihusisha na biashara zozote kwa kipindi chote wanachokuwa madarakani.
  • Serikali iunde mfuko maalum kwa ajili ya uwezeshaji watumishi wake na uwepo usimamizi mzuri wa fedha za uwezeshaji ili kuhakikisha walengwa wanakuwa ni watumishi wa kipato cha kati na cha chini tu.
  • Serikali iboreshe sheria kuruhusu fao la kujitoa na pia ianzishe utaratibu wa kuwalipa mafao watumishi wa umma kila baada ya kipindi cha miaka mitano kama ilivyo kwa wabunge na madiwani. .
  • Sheria za uchaguzi ziboreshwe ili zilinde nyadhifa za kiutumishi kwa watumishi wa umma wanaogombea nafasi za kisiasa mpaka pale mtumishi husika atakapoapishwa kushika wadhifa mwingine wa uongozi.
  • Kuwepo na utaratibu wa serikali kununua madeni ya watumishi kwenye mabenki na taasisi za fedha ili kuwapunguzia mzigo wa marejesho.
  • Sheria ya mafao iboreshwe ili kuwezesha watumishi wa umma wanapostafu utumishi wao, na wenyewe wawe wanajengewe nyumba za makazi kulingana na hadhi zao na kila mwezi walipwe pensheni 80% ya mshahara wa mtumishi aliyeko ajirani.
Hitimisho

Kukosekana kwa sera na sheria rafiki kwa maisha na maslahi ya watumishi ndio chanzo cha watumishi wengi kujikuta wanatumbukia katika madeni ya taasisi za kifedha, hivyo ni wakati sasa kwa serikali na waajiri wengine kuzifanyia maboresho kanuni na sheria zinazosimamia maslahi na mikataba ya watumishi wao.

Aidha waajiri wawe na mpango endelevu wa kuwaelimisha watumishi wao namna bora kuitumia mikopo yao katika kufanya uwekekezaji wenye tija kwa maisha yao ya sasa na baadae.

"Mathalani unaweza kukuta mkopaji amekopeshwa kiasi cha Tshs 1,000,000/= , lakini anaambiwa kwenye mkataba ajaze kakopeshwa 1,500,000 alafu anapigiwa riba ya mkopo kutoka hapo kwenye kiasi hicho ilihali mkononi kapewa 1,000,000 tu!"

Huwa unakopa wapi mkuu unakopigwa hivi
 
"Mathalani mtumishi anaweza kuwa awali alikopeshwa 10,000,000/=, ambapo deni zima likasoma 23,000,000/=, Baada ya miaka 3 akienda benki na kufanya top up,

Hapa kwanza atauliza benki kiasi halisi anachodaiwa hadi kufikia muda huo. Hapa mabenki mengi huwa hawaongei ukweli, unaweza kuambiwa bado unadaiwa 9,200,000/= wakati umeshafanya marejesho kwa karibu nusu ya muda wa deni na deni zima limepungua toka 23,000,000 hadi 14,000,000.

Ili apate kiasi flani kwenye mkopo wake wa top up, inabidi mkpaji aombe kukopeshwa kiasi flani ambacho ni zaidi ya 9,200,000, mfano 11,000,000, Hapa deni lake litapaa upya kutoka 14,000,000 mpaka 25,000,000 huku mkononi akiambulia 1,500,000/= tu !

Kwa hiyo ukiangalia utaona kuwa alichokopeshwa mtumishi hapa ni 1,500,000/= tu, lakini deni lililoongezeka ni karibu 11,000,000/="

Sijui ni unakopa wapi na unanyiwa hivi lakini hesabu ya top up wala haipo hivi ulivyoilezea hapa mkuu. Kinachofanyika ni kwamba unatakiwa ufute deni la kwanza ili upate mkopo mpya, mfano hapo kama deni lako ni hiyo 9,200,000/= basi utakopa kiasi cha juu kidogo kulingana na makato yako yanavyoruhusu, mfano ndio hiyo 11,000,000/= basi utapata 1,800,000/= wakati deni lako litabaki 11M tu sababu lile la nyuma umefuta.
Sio kwamba eti utapewa deni hili na lile jingine ambalo ulishalilipa, kama unafanyiwa hivyo nenda katoe taarifa kwa wahusika wakusaidie maana unaibiwa.
 
Mkuu yawezekaba wewe ni mkopeshaji ndio maana unajaribu kutetea huu uporaji wa mabenki!
Unataka kusema mtu akikopa 11M anarejesha hiyoiyo 11M bila riba ??? Mfano umekopa deni la msingi 11M, kwa marejesho ya miaka 6 kwa riba ya 21.8% , hesau ipo hivi:-
1. Deni la msingi ni 11,000,000
2.Riba ni 11,000,000 X 21.8% X 6 Inakupa 14,388,000
3.Jumla ya deni lote Tunajumlisha Deni la msingi(11M) na Riba ya mkopo(14,388,000) hapa jumla inakupa 25,388,000
Hili ndilo deni utakalorejesha kwa miaka 6 ambapo riba pekeake tu ni 14,388,000 wakati wewe mkononi ulipewa 1,800,000 tu, huoni kwamba huo ni wizi mkavu??? usibishe kitu kama huna experience nacho mkuu!
Tena unaongea kwa mzaha wakati watumishi wameshalizwa!
 
Ndo maana sijawahi kuwaza kuchukua mkopo mm
 
Nenda BOT mkuu hao wanaokukopesha wanakuumiza sana kama ndio hesabu wanakupigia kwa rate hizo, njoo DM nikuelekeze sehemu nzuri ya kukopa, kwa rate nzuri na ndio kimbilio la watumishi, ukikopa wewe naamini na wenzako watakuja.
 
Ile dhana aya Taasisi nyingi za Umma kukosa ubunifu na kuwa na huduma mbovu inachangiwa na maslahi duni kwa watumishi wa umma,

Nitatolea mfano sekta ya Elimu na Afya, Shule za Umma zinatoa matokeo mabovu kutokana na Walimu kukosa motisha, mishahara midogo, mazingira ya kazi mabovu, Mwalimu anafundisha anawaza watoto wake watakula nini, pesa yote imeishia kwenye mikopo, mtaani madeni chungu nzima,

Kwa upande wa Afya nako ni hivyo hivyo, mtaalamu wa Afya anatoa huduma kwa Mgonjwa, akiwa hana matumaini ya familia yake kupata mlo kwa siku hiyo, matokeo yake utakuta watumishi wa Afya wanatafuta part time/Vijiwe ili waweze kujikimu.
Ili lilikuwa tatizo kwa Hospitali kubwa kama Muhimbili wakaja na njia ya kuwapa motisha watumishi, asilimia fulani ya kile wanacho zalisha kinarudi kwa watumishi kama motisha/Allowance. Taasisi nyingi za Afya zikaiga, na kweli zikawa na matokeo chanya.

Mfano ukichukulia Taasisi ya Jakaya kikwete/JKCI, leo ni ni mojawapo ya Taasisi za Umma za kutolewa mfano katika maswala ya kibingwa ya Moyo, na Nchi nyingi zinaleta wagonjwa wao pale, sababu watumishi wake wanathaminiwa, wanapewa motisha, nafasi za kusomeshwa nk.
Serikali ikiamua inaweza kuondoa machungu ya watumishi wa Umma, na kuwaondolea mizigo ya Mikopo umiza kutoka kwenye mabenki .
 
Hili sualala mikopo kwa watumishi ni pasua kichwa. Actually ni bomu ambalo siku likilipuka sijui itakuwaje. Watumishi wengi wana hali mbaya mnoooo.
 
Mtoa mada kuna sehemu umepotosha watu kwenye top up na kukopa milioni 1.5 ukapewa 1
 
Back
Top Bottom