namna bora ya kukiri na kuomba msamaha kwa akina mama. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

namna bora ya kukiri na kuomba msamaha kwa akina mama.

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by gfsonwin, Aug 4, 2012.

 1. gfsonwin

  gfsonwin JF-Expert Member

  #1
  Aug 4, 2012
  Joined: Apr 12, 2012
  Messages: 16,943
  Likes Received: 1,817
  Trophy Points: 280
  Wewe ni mama ama binti ambaye umeolewa ma una mchumba, katika kuish kwenu najua kabisa kuna kukoseana kwa hapa na pale. Je wewe unapokosea wajua jinsi ya kukiri kosa na kuomba msamaha? je watanguliza ubabae na mdomo wa kama chiriku ama unayaona na unakubali makosa yako? Je panapo kuyaona na kuyakubali je wachukua hatua gani zaid?

  soma hapa:
  1)Ona kosa lako kabisa kisha jiweke kwenye nafasi ya mwenzako iwe kama wewe ndo umetendewa.
  2)Ona na dadavua athari za kosa lenyewe kabla hata hajakuambia ili uweze kufikiri njia sahihi ya kupata suluhu.
  3) kwa upole kabisa unapoambiwa kwamba umekosea usikasirike wala kupandisha hasira, tulia msikilize hadi amalize, wala usianze kulia kama njia ya kujihami ama kuropoka maneno makali( hili linawahusu akina dada)
  4)Onyesha kwamba umeyatambua makosa yako kihisia na hata kwa kusema kisha taja suluhu kwako wataka iwe ni nini.
  5)wakati wa kutoa suluhu jiweke kwenye nafasi ya mwenzi wako isiwe kitu ambacho kitamuumiza mwenzio bali kiwe ni kile ambacho kitawanufaisha.
  6)umesha tambua kosa, umelielezea, ukasema wataka suluhu ya jambo iwe nini, basi omba msamaha hata kama atasema hasamei kwa wakati huo wewe omba.
  7) usiyaweke maneno ambayo mwenzi wako anaweza kuwa anayasema moyoni kwa wakati huo manake mengine yawezekana yakawa yanamtoka kwa hasira tu. Ila weweuwe mpole wala usimbughudhi kwa lolote lile hadi moyo wake utulie.
  8)silaha kubwa sana kwa mama wakati wa kkukiri na kuomba msamaha hasa panapo makosa makubwa basi iwe ni upole na unyenyekevu wala isiwe maneno ya kuropoka na jeuri ama kashfa.
  9) kwa kujua upendo wa mwenzi wako kwako basi ni busara kabisa ukampa muda wa yeye kusahau hapa waweza kumuomba akupe ruhusa uende kwenu kidogo ili aone kama bado anaweza kukuhitaj.
  10) mwombe Mungu sana wala usitangaze kwa watu manake Mungu anasema katika zab 62:1-2 kwamba umngoje bwana kwa kimya na yeye atakuwa mwamba wako hutatikisika sana.


  hitimisho njia hii siyo lazima ikafanya kazi kwa kila mtu ila kwa wewe mwanamke mwenzangu najua itakusaidia.

  kwaharini bana niko fungateni nitarudi tena kujibu hoja zenu. ila nikimaliza funngate nakuja na bandiko kali la wababa manake nimejifunza mengi nilipo huku.
   
 2. Kongosho

  Kongosho JF-Expert Member

  #2
  Aug 4, 2012
  Joined: Mar 21, 2011
  Messages: 36,126
  Likes Received: 301
  Trophy Points: 160
  mie kwa kweli nikikosa na nikaona nimekosa, na nikaona mtu kaumia, huwa naomba msamaha haswaa hadi niridhike kuwa nimesamehewa.

  Ila wasameheaji wengine wanasamehe kiongo ongo, hapa ndio huudhi. Anyway hii inasaidia ukimpa muda wa kutafakari kwanza.
   
 3. Kaunga

  Kaunga JF-Expert Member

  #3
  Aug 4, 2012
  Joined: Nov 28, 2010
  Messages: 12,590
  Likes Received: 796
  Trophy Points: 280
  Thanks shostito kwa somo hili zuri.
   
 4. gfsonwin

  gfsonwin JF-Expert Member

  #4
  Aug 4, 2012
  Joined: Apr 12, 2012
  Messages: 16,943
  Likes Received: 1,817
  Trophy Points: 280
  Kongosho kweli hiyo ni njia nzuri sana katika maisha shostito manake kuna watu huwa hawajui kabisa kama wanakosea na hawa hujizidishia haki sana katika maisha to me ni watu ambao wanaboa sana kwakweli. Lakini pia kuna wakaka ni wagumu kusamehe hadi maudhi.
   
 5. mtotowamjini

  mtotowamjini JF-Expert Member

  #5
  Aug 4, 2012
  Joined: Apr 23, 2012
  Messages: 4,540
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Tunashukuru kwa ushauri ngoja niiprint hii nimepelekee mama yeyoo!!!:happy:
   
 6. gfsonwin

  gfsonwin JF-Expert Member

  #6
  Aug 4, 2012
  Joined: Apr 12, 2012
  Messages: 16,943
  Likes Received: 1,817
  Trophy Points: 280
  ahsante sana Kaunga lakini na wewe tuongezee maujuzi kidogo.
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 7. Asprin

  Asprin JF-Expert Member

  #7
  Aug 4, 2012
  Joined: Mar 8, 2008
  Messages: 50,860
  Likes Received: 23,478
  Trophy Points: 280
  Hebu niambieni kwa muhtasari gfsonwin anazungumzia nini? Wengine tumezoea makalkuleshen bana
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 8. gfsonwin

  gfsonwin JF-Expert Member

  #8
  Aug 4, 2012
  Joined: Apr 12, 2012
  Messages: 16,943
  Likes Received: 1,817
  Trophy Points: 280
  asante lakini na wewe tuongezee point bana jf tunajifunza mkuu.
   
 9. gfsonwin

  gfsonwin JF-Expert Member

  #9
  Aug 4, 2012
  Joined: Apr 12, 2012
  Messages: 16,943
  Likes Received: 1,817
  Trophy Points: 280
  khaaa! umesahau jinsi nilivyokuomba msamaha siku ile????
   
 10. Mr Rocky

  Mr Rocky JF-Expert Member

  #10
  Aug 4, 2012
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 15,187
  Likes Received: 563
  Trophy Points: 280
  gfsonwin asante sana kwa kutoa somo
  Ni somo zuri sana na sio kwa upande mmoja tuu bali pande zote kunapokuwa na makosa
  Samahani ni neno moja dogo sana ila kwa wengine ni gumu sana kulisema Asprin kwani hujaona makalkulesheni hapo juu aise
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 11. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #11
  Aug 4, 2012
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,826
  Likes Received: 22,463
  Trophy Points: 280
  mtu anaomba msamaha hadi kulia na machozi
  baada ya siku mbili 'anafanya yale yale' tena sasa na zaidi....

  women bana
   
 12. Mtambuzi

  Mtambuzi Platinum Member

  #12
  Aug 4, 2012
  Joined: Oct 29, 2008
  Messages: 8,795
  Likes Received: 1,247
  Trophy Points: 280
  Naanza kujiuliza kama ukija na uzi wa kina baba wawe wanaomba msamaha, subiri utakachokipata kutoka kwao......
  Wanaume wengine bwana kwao kuomba msamaha kw awake zao wanaona kama vile ni kujishusha, sana sana anaweza tu kusema. "samahani basi." na kama mwanamke anashindwa kuelewa, kibao kitamgeukia, yatakumbushwa makosa yake ya nyuma ambayo pengine alishasahau..............

  Chonde chonde dada gfsonwin hiyo mada ya wanaume iweke tu kapuni........................LOL

  Msinitafute na mie niko fungate na mama Ngina......
   
 13. Mr Rocky

  Mr Rocky JF-Expert Member

  #13
  Aug 4, 2012
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 15,187
  Likes Received: 563
  Trophy Points: 280
  The Boss hiyo ipo sana na wala sio la kujificha
  yaani unaweza kufikiria may be anafanya kusudi au vipi maana anarudia kitu kile kile ambacho ulimsamehe nacho
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 14. gfsonwin

  gfsonwin JF-Expert Member

  #14
  Aug 4, 2012
  Joined: Apr 12, 2012
  Messages: 16,943
  Likes Received: 1,817
  Trophy Points: 280
  ni kweli kabisa Mr Rocky na nimeliweka leo kwa wanawake kwani nataka kuona michango ya akina baba humu takuwaje na nitokapo fungateni basi nitaweka bandiko la wababa ili nione pia wamama tutachangia vipi.
  ukweli kuna wanawake wagumu wa kuomba samahan hadi unajiuliza hivi yale madaha ya kike kwa huyu mtu yapo? je ana staha za kike kweli? mtu ni mkatili hsi kwa mume tu hadi kwa watoto na wafanyakazi mwaka mmoja anabadili wadada wa kazi mara kumi kwa ubabe wake kashfa ni zake, umbwamba usiseme lol! wanawake wa staili hii naomba Mungu sana wapite mbali na kijana ama baba yeyote wa humu jf.
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 15. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #15
  Aug 4, 2012
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,826
  Likes Received: 22,463
  Trophy Points: 280

  kuliko kuomba msamaha bora tu useme
  ukweli kuwa 'huna uhakika hutarudia tena'
  anything is possible...
   
 16. Mr Rocky

  Mr Rocky JF-Expert Member

  #16
  Aug 4, 2012
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 15,187
  Likes Received: 563
  Trophy Points: 280
  gfsonwin kumbe mnajijua eee
  Wapo hao bana yaani yeye hata kama ni kaugomvi kadogo utamjua tuu mume akipandisha sauti na yeye anapandisha
  hana cha kujishusha mbele ya mume wala watoto na kwake yeye always yuko right
  Kuomba kwake msamaha ni nadra sana maana kwake huo msamiati haupo
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 17. gfsonwin

  gfsonwin JF-Expert Member

  #17
  Aug 4, 2012
  Joined: Apr 12, 2012
  Messages: 16,943
  Likes Received: 1,817
  Trophy Points: 280
  @bos hiyo ni kweli na hii hutokana na hili kuna watu ambao panapo kosa hujifunza kitu na kamwe hatakiacha alichojifunza na huyu huwa mwalim mzuri sana kwa wengine.

  lakin pia kuna ambao hawajifunzi na hii hutokana na akili ya uelewa ya mtu, mazingira anayoish na aina ya watu anao intarakti nao. ni vizuri wa wewe mkosewa ukajua kwamba nini ababisho ili ukalifanyia kazi.
   
 18. peri

  peri JF-Expert Member

  #18
  Aug 4, 2012
  Joined: Mar 22, 2011
  Messages: 2,588
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  lol, jf bana, full maujanja.
  Kuna vitu vingi adimu.
  Ujumbe umefika na umeeleweka.
   
 19. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #19
  Aug 4, 2012
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,826
  Likes Received: 22,463
  Trophy Points: 280
  if only kuna enough time for all that...
   
 20. gfsonwin

  gfsonwin JF-Expert Member

  #20
  Aug 4, 2012
  Joined: Apr 12, 2012
  Messages: 16,943
  Likes Received: 1,817
  Trophy Points: 280
  yaani sindano inauma sana ingawa ni dawa hivyo kwa hawa miye nawachoma sindano najua wapo watakao pona. ukienda fungate ubebe na kipakato chako manake nitaku tag unisaidie wakinirushia makombora lol!
   
Loading...