Namna bora ya kujifunza jinsi ya kuishi ni kujifunza jinsi ya kufa!

66KV

JF-Expert Member
May 16, 2014
1,219
2,407
Heshima kwenu wanabodi
Kila mmoja wetu jua kuna siku moja atakufa, lakini bahati mbaya kabisa hakuna hata mmoja kati yetu anayeamini kabisa kabisa kwamba kuna siku atakufa na kufukiwa chini ,kama tungalikuwa tunaamini hivo basi tungalifanya mambo yetu kwa uangalifu mkubwa huku kichwani tukiwa Tunajuwa muda wetu ni mchache mno mno, kuna uwezekano mkubwa kabisa miili yetu itakaa makaburini miaka mingi kuliko miaka tuliyoishi duniani (sitoi guarantee ni mtazamo)

Kwakuwa kifo ni HALISI na hatuna namna ya kukiepuka, twaweza kukitumia kifo kama ALARM/NOTIFICATION ambayo kila sekunde/dakika ama saa inalia na kukumbusha kuwa MUDA UMEISHA,FANYA HARAKA,FANYA YALE AMBAYO KWELI UNGEPENDA YAFANYIKE KABLA HUJAONDOKA, chukulia kama umevaa kengele masikioni mwako inayokwambia kila wakati YOUR RUNNING OUT OF TIME BOY/GIRL.....,DO WHAT'S IMPORTANT ONLY(samahani kwa vingereza uchwara)

Ukiweza kukaa na hii alarm na kuisikiliza kila wakati itakusaidia sana sana kuchagua mambo ya kufanya ambayo ungependelea uyaone yamefanyika kabla hujaondoka, na bila shaka utachagua vizuri,rekodi zinaonesha wagonjwa waliogua magonjwa yasiyoyopona mfano saratani Muda ule mchache uliosalia huwa wanaishi purposely kuliko kipindi ambacho walikuwa na afya njema. Afya njema ni kama illusion tu inayosahaulisha kuwa muda umekwisha

kama una marafiki wapende sana sana,hujui umebakiwa na muda kiasi gani,kama una mke na watoto wapende sana sana hakuna muda wa kupoteza, Ukipata nafasi ya kuonesha upendo wako toa upendo wako wote , kwa sababu mwisho wa siku SISI NI KAMA VIPANDE VYA HADITHI ,maisha unayoishi unaandika hadithi ,HAKIKISHA UNAACHA HADITHI TAMU KABLA YA KUONDOKA ,usiogope KIFO kipo tu ,Kitumie KIFO kuacha alama katika maisha ya watu.

Mwisho kumbuka kuishi miaka mingi haimaanishi kwamba umeishi maisha marefu ,waweza ishi miaka 40 ndani ya hiyo miaka ukaacha alama kama mtu aliyeishi miaka 80, Pia waweza ishi miaka hata 100 ukaondoka kama vile hukuwahi kuishi, tutengeneze moments za kukumbukwa kwa familia zetu,marafiki zetu ,majirani zetu na wooote wanaotuzunguka.

Niwatakie utekelezaji mwema wa majukumu yenu.
wasalaam.
 
Jamaa umefikiria nini. Naona umeenda mbali sana kihisia ingawa watu wengi watapuuzia hata kucoment kwenye uzi huu but ukweli ndio huo hakuna atakaye weza kubadilisha ulicho kiandika hapo. Long live kiongozi
 
Naam kuna watu wameishi miaka michache tu lkn wanaendelea kutajwa mpaka leo na wataendelea kutajwa mpaka dahari ama kwa wema au kwa ubaya
 
Naona Mkuu umeandika kwa hisia mno, na hisia za namna hii huwa zinapatikana usiku hasa ukiwa unawaza haya na yale.
 
Ni kweli, Tumia muda uliyopo kujitengenezea Jina lisilo sahaulika,
Akina 2pac, Che Guevala, Pablo Escobar N.k wote hawa walitumia muda wao vizuri.
"Historia haipigiwi Makofi"
 
6 Reactions
Reply
Back
Top Bottom