Namna asubuhi yako inavyotakiwa kuwa

josephdeo

Member
Nov 23, 2015
95
196
Habari the choosen people nawasalimu katika jina la jamuhuri.

Leo niko hapa kuwasogezea haya. Kuna msemo ambao unasema kuwa siku njema huonekana asbuhi. Waswahili husema samaki mkunje angali mbichi. Pia ndivyo inavyokuwa ili kutengeneza siku nzuri inapaswa kufanyika asbuhi

Kwa maana hiyo asbuhi yako ndio huamua ni kwa kiasi gani siku yako itakuwa kwa mjumuisho. Asbuhi ndio sehemu ambayo huwa na matayarisho juu ya siku husika.

Kila mmoja wetu anapoamka ndio upangilia mipango yake ya kuendesha siku hiyo kwani tayari anakuwa na uhakika juu ya kuwa na uzima. Hivi ukiamka huwa unasema Nini?, ni nini ambacho kinakuwa akilini mwako!!.

Pale ambapo unaona kuwa sasa ninayo siku nyingine ya kuvuta pumzi ya bure kutoka kwa Mwenyezi Mungu?, ukiachana na maombi ya shukrani kwa Mungu kwaajili ya ulinzi na kujikabidhi kwake kwaajili ya siku nzima huwa unajitamkia nini?

Maswali yanaweza kuwa mengi haya tuliyokuuliza wewe msomaji na sababu zilizo pelekea sisi kukuuliza maswali hayo ni kutaka kufahamu asbuhi yako huwa inakuwaje?.

Ili sisi tuwezekukwambia kuwa unatakiwa kuitumiaje asbuhi yako. Tunafahamu kuwa watu wanalala na majeraha moyoni, wanalala wamechoka, wanalala wameumizwa na wanalala na msongo wa mawazo juu ya kufikilia kesho yao.

Pamoja na yote hayo Mungu akiwapa nafasi basi wote wataamka na kuianza siku mpya. Sasa katika hayo yote wewe unaianzaje siku yako kwa maneno gani? Asbuhi yako inakuwa na maneno gani?.


******
Kwanza ni muhimu kutambua kuwa kuna nguvu kubwa katika kujinenea inayopatikana kwenye kinywa chako. Kuna nguvu kubwa ambayo inapatikana kwenye kinywa chako pale ambapo unaongea na wewe.

Kuwa makini: tunaweza kuwa tumekuacha na jukumu la kukurudia ili tuweze kwenda wote ni la kwetu pia. Wewe ambaye una mwili wa nyama na unamiliki jina sio wewe ambaye upo ndani na kwa lugha rahisi tunaweza kuita roho.

Yaani kuna roho yako na wewe ambaye sasa una mwili wa nyama hivyo mara zote kuna nguvu kubwa pale ambapo huu mwili wa nyama unaiambia nafsi au roho maneno yenye faraja.

Nafsi inapopata yale maneno inatengeneza kujiamini katika roho yako ambayo ndio kiunganishi kati yako na Mwenyezi Mungu na kisha kuutengenezea mwili wako hali ya kujiamini na kupambana.

Asbuhi yako inatakiwa kuwa yenye kujinenea yaliyo mema kwako ilikutengeneza nafasi ya kuwa na siku nzuri kwa kutwa hiyo. Hii aijalishi utalala na mawazo au maumivu ya kiwango gani.

Inapofika asbuhi ya siku mpya inakupaswa kufahamu kuwa hiyo ni siku nyingine na unatakiwa kuyaacha yote yaliyokukwaza na kukuumiza nyuma na kujinenea vyema ili siku yako iweze kuwa bora na nzuri.

Asbuhi ndio wakati wa kutafuta siha ya siku yako itakavyokuwa na hili siha hiyo iwe bora ni vyema kujinenea maneno ya kujiinua na kujifariji juu ya siku hii mpya ambayo Mwenyezi Mungu amekupa kama zawadi.

Jitangazie ujasiri ndani yako katika asbuhi yako jiweke katika mazingira ya kuwa wewe ni bora kwa uwezo wako na hakuna aliye kama wewe mwenye uwezo wako.

Jinenee kuwa wewe ni nuru ya ulimwengu na hivyo ulimwengu unakuhitaji ili kuendelea kuwa na mwangaza na kamwe giza aliwezi kukaa wala halina nafasi ndani yako.

Jinene kuwa wewe ni mbarikiwa hivyo laana wala mipango ya shetani haiwezi kupata nafasi kwako.

Jinenee kuwa wewe ni mshindi na utashinda vita yoyote itakayo kuja mbele yako kwa yule akutiaye nguvu Mungu Mwenyezi.

Jinenee kuwa wewe ni mkuu na hivyo uwezi kushindwa na chochote hapa chini ya jua. Jinenee kuhusu uwezo ulionao wa kuweza kuhimili mipango yote mibaya kukuhusu.


*****
Jitahidi kujinenea yale yote yaliyo mema ambayo yatakusaidia katika kuanza siku yako ukiwa na hali ya mapambano na ladha ya maisha.

Ukiwa mwaminifu na kuanza siku yako kwa namna hii basi utakuwa mtu hodari, shujaa na hautakatishwa tamaa na chochote kwa sababu ujasiri utakuwa ndani yako.

Hivyi ndivyo ambavyo unatakiwa kuanza asbuhi yako mara baada ya kumshukuru Mungu kwa uzima.

Maisha yatakuwa mazuri sana kwa upande wako ikiwa utazingatia haya na mara zote utakuwa na siku bora kama utaanza siku yako kwa namna hii. Asante!
 
Back
Top Bottom