Namna 5 sahihi tunazotumia kupunguza gharama za ujenzi hadi 40%

JAMII BORA

Member
Apr 18, 2017
78
58
Nianze kwa kushukuru wadau humu JF kwa mchango wao wa mawazo hadi makala hii kukamilika.

Kwanza kabisa kabla hujafikiria kupunguza gharama za ujenzi unatakiwa kufahamu gharama halisi za ujenzi, Wengi wa wateja tulokutana nao, walikuwa na tatizo linalofanana, nalo ni kwamba huwa wanataka kupunguza gharama za ujenzi wakati hawana uelewa mzuri wa gharama halisi za ujenzi zilivyo. Ni vyema ukajua kwanza nyumba/jengo fulani la ukubwa fulani na ubora fulani katika mazingira fulani linagharimu kiasi gani cha fedha mpaka kukamilika ndio ufikirie uwezekano wa kupunguza hizo gharama ili ujue umeokoa kiasi gani cha fedha katika mradi huo.

Sasa twende tuangalie mbinu mbalimbali za kupunguza gharama hizi za ujenzi;

1. Namna ya kwanza na pengine sahihi zaidi ya kupunguza gharama za ujenzi ni kuwa makini na ukubwa wa jengo husika, kwa sababu ukubwa wa jengo unachangia kwa kiasi kikubwa sana ukubwa wa gharama za ujenzi wake, kwa hiyo kupunguza vile visivyo na umuhimu na kupunguza ukubwa wa sehemu za ndani ya jengo kama sio muhimu sana kwako ni njia ya kwanza sahihi sana. Huwa tunapokea mteja, anaweza kukwambia nataka unitengenezee nyumba ndogo ya gharama nafuu ya vyumba vitano viwe vikubwa, mtu anataka nyumba ndogo ya bei nafuu lakini yenye vyumba vingi halafu viwe vikubwa. Weka vyumba ambavyo ni standard, kama ni nyumba ya kuishi unaweza kuchagua baadhi ya vyumba kama vile sebule na masterbedroom viwe vikubwa kiasi labda na jiko liwe na nafasi ya kutosha kupangilia vinavyohitajika na vyumba vingine viwe vya kawaida.
Kama ni majengo ya biashara au ofisi unaweza kupunguza maeneo yasiyotumika (dead spaces) kuondoa visivyo na ulazima na vingine vya namna hiyo.

2. Namna ya pili sahihi kupunguza gharama za ujenzi ni kutengeneza ramani halisi ya jengo lako. Tunachofanya Tunamuandalia bure mteja michoro tunayoifanya kwa kuzingatia gharama, hapa unaweza kuepuka kutumia gharama zaidi kwa sababu utakuwa tayari umefanya makadirio ya ujenzi ambapo utaondoa uwezekano wa kuongezeka gharama zitakazoweza kuongezeka aidha kwa wewe mteja kuongeza jengonje ya ramani au kupunguza chochote kutokana na kukosa mwongozo

3. Namna ya tatu sahihi ya kupunguza gharama za ujenzi ni wataalamu wetu wa ujenzi kufanya kazi kwa pamoja kwa ushirikiano huku wakiweka kipaumbele katika kupunguza gharama. Tunapoanza mhandisi mihimili (structural engineer) anashauriana na msanifu/mbunifu majengo (architect) namna ya kupunguza idadi ya nguzo au upana wake kwenye baadhi ya maeneo ili kuepuka kutengeneza sehemu zisizo na umuhimu (dead spaces) zitakazolazimu kutanua jengo zaidi kufidia huo ukubwa uliochukuliwa na nguzo, yote haya bila kuleta madhara

4. Namna ya nne sahihi ya kupunguza gharama za ujenzi ni kufanya kazi kama mpango wa kazi ulioandaliwa kutokana na makubaliano na mteja. Hii itakusaidia kuepuka uwezekano wa kuongezewa gharama baada ya makubaliano kupishana na uhalisia (variations) ya kitu chochote.Lakini hii haizuii kujadiliana baina yetu na mteja kama kuna mabadiliko ya muhimu na kukubaliana.

5. Namna ya tano sahihi ya kupunguza gharama za ujenzi ni manunuzi ya jumla ya vifaa vya ujenzi. Mahitaji yote ya mradi husika unakaa chini na wataalam wetu tukapanga aina ya vifaa vya ujenzi kadri ya mazingira uliyopo. Jambo hili linahitaji umakini mkubwa sana kwa sababu, tunapokea simu za wanaoomba ushauri baada ya kufika mbele ya safari katika huo ujenzi na kukuta kilichonunuliwa hakifai au pengine kimeharibika na hakifai tena kwa sehemu iliyokusudiwa. Tunashauri anza na mtaalam wa ujenzi unayemwamini ili usije kujikuta unajiingiza kwenye hasara badala ya kupunguza gharama.

Tumeambatanisha nyumba ya vyumba viwili,sebule,choo cha ndani na jiko tulojenga kwa milioni 12 tu,ikikamilika ndani ya siku 60, tukiokoa 40% ya gharama ukifananisha na wengine walojenga ramani kama hii.(Wengi wametumia kuanzia milioni 20).

Kwa ushauri bure juu ya ujenzi, au huduma za kujenga nyumba bora huku ukipunguza gharama, wasiliana nasi

0713 039 875 au 0742 499 177

Drone Online Ads

IMG_20201029_123207_4.jpg
IMG_20201029_123725_8.jpg
IMG_20201029_123359_1.jpg
IMG_20201029_123326_1.jpg
 
Asante kwa ushauri.

Ila hapo kwenye nyumba ulioambatanisha umekosea kusema "mlijenga nyumba kwa siku 60 na kuokoa 40%" hivi kweli mmeokoa 40% kwa lipi hapo wakati madirisha mmeweka nyavu, plasta hamjafanya na finishing kwa ujumla hamjafanya?

Au unasemea kuokoa 40% kunyanyua boma? Kutokana na picha uliyoweka naomba ubadilishe kichwa cha mda na kisomeke " okoa 40% ya ujenzi wa boma".
 
Karibu ndugu. Tumeokoa 40% ya gharama ukifananisha na nyumba za ukubwa huu zinazoagharimu zaidi.
 
Hiyo point 5 umezungumza vyema ila pia kuna sababu nje ya ulivyotegemea kama sasa ujenzi unaumiza kichwa mfano mdogo kabla ya uchaguzi cement ilikuwa chini.

Ila week hii moja cement ukienda kichwa kichwa unaumia.
 
Ni kweli. Ndiyo sababu sisi huwa tunanunua kwa materials ya ujenzi kwa pamoja pale tunapoanza hivyo mabadiliko ya bei hayataathiri mradi tuliopo
 
Asante kwa ushauri.

Ila hapo kwenye nyumba ulioambatanisha umekosea kusema "mlijenga nyumba kwa siku 60 na kuokoa 40%" hivi kweli mmeokoa 40% kwa lipi hapo wakati madirisha mmeweka nyavu, plasta hamjafanya na finishing kwa ujumla hamjafanya?

Au unasemea kuokoa 40% kunyanyua boma? Kutokana na picha uliyoweka naomba ubadilishe kichwa cha mda na kisomeke " okoa 40% ya ujenzi wa boma".
Hapo hata msingi hauna mkanda huo ni ujenzi au kupanga tofali??
 
mkuu acha kudanganya watu kwa manufaa yako huwezi kusave 40% ya gharama ya ujenzi kwa izo njia zako ulizoandika hapo. Boq mpaka ipungue kwa percent yote hio ni lazima kuwe na change in quality na specification au changes in quantity ya items na ukishabadili quality tayari huwezi sema umesave hela. Hakuna value engineering duniani kokote inayoweza kusave 40% ya contract sum ya jenga na bado usialter quality ya uo ujenzi. its probably huwa unaestimate juu sana au unapunguza specifications na quality ndo uweze kuapata io 40%. Cost control nzuri probably itspunguza aprox 5-8% ya contract sum na hapo iwe imefanywa na qs mzuri kwanzia design stage mpaka mda ya kumaliza mradi haya unayosema wewe ni uongo mtupu na next to impossible. Hivi mkuu unaijua 40% wewe??
 
Nianze kwa kushukuru wadau humu JF kwa mchango wao wa mawazo hadi makala hii kukamilika.

Kwanza kabisa kabla hujafikiria kupunguza gharama za ujenzi unatakiwa kufahamu gharama halisi za ujenzi, Wengi wa wateja tulokutana nao, walikuwa na tatizo linalofanana, nalo ni kwamba huwa wanataka kupunguza gharama za ujenzi wakati hawana uelewa mzuri wa gharama halisi za ujenzi zilivyo. Ni vyema ukajua kwanza nyumba/jengo fulani la ukubwa fulani na ubora fulani katika mazingira fulani linagharimu kiasi gani cha fedha mpaka kukamilika ndio ufikirie uwezekano wa kupunguza hizo gharama ili ujue umeokoa kiasi gani cha fedha katika mradi huo.

Sasa twende tuangalie mbinu mbalimbali za kupunguza gharama hizi za ujenzi;

1. Namna ya kwanza na pengine sahihi zaidi ya kupunguza gharama za ujenzi ni kuwa makini na ukubwa wa jengo husika, kwa sababu ukubwa wa jengo unachangia kwa kiasi kikubwa sana ukubwa wa gharama za ujenzi wake, kwa hiyo kupunguza vile visivyo na umuhimu na kupunguza ukubwa wa sehemu za ndani ya jengo kama sio muhimu sana kwako ni njia ya kwanza sahihi sana. Huwa tunapokea mteja, anaweza kukwambia nataka unitengenezee nyumba ndogo ya gharama nafuu ya vyumba vitano viwe vikubwa, mtu anataka nyumba ndogo ya bei nafuu lakini yenye vyumba vingi halafu viwe vikubwa. Weka vyumba ambavyo ni standard, kama ni nyumba ya kuishi unaweza kuchagua baadhi ya vyumba kama vile sebule na masterbedroom viwe vikubwa kiasi labda na jiko liwe na nafasi ya kutosha kupangilia vinavyohitajika na vyumba vingine viwe vya kawaida.
Kama ni majengo ya biashara au ofisi unaweza kupunguza maeneo yasiyotumika (dead spaces) kuondoa visivyo na ulazima na vingine vya namna hiyo.

2. Namna ya pili sahihi kupunguza gharama za ujenzi ni kutengeneza ramani halisi ya jengo lako. Tunachofanya Tunamuandalia bure mteja michoro tunayoifanya kwa kuzingatia gharama, hapa unaweza kuepuka kutumia gharama zaidi kwa sababu utakuwa tayari umefanya makadirio ya ujenzi ambapo utaondoa uwezekano wa kuongezeka gharama zitakazoweza kuongezeka aidha kwa wewe mteja kuongeza jengonje ya ramani au kupunguza chochote kutokana na kukosa mwongozo

3. Namna ya tatu sahihi ya kupunguza gharama za ujenzi ni wataalamu wetu wa ujenzi kufanya kazi kwa pamoja kwa ushirikiano huku wakiweka kipaumbele katika kupunguza gharama. Tunapoanza mhandisi mihimili (structural engineer) anashauriana na msanifu/mbunifu majengo (architect) namna ya kupunguza idadi ya nguzo au upana wake kwenye baadhi ya maeneo ili kuepuka kutengeneza sehemu zisizo na umuhimu (dead spaces) zitakazolazimu kutanua jengo zaidi kufidia huo ukubwa uliochukuliwa na nguzo, yote haya bila kuleta madhara

4. Namna ya nne sahihi ya kupunguza gharama za ujenzi ni kufanya kazi kama mpango wa kazi ulioandaliwa kutokana na makubaliano na mteja. Hii itakusaidia kuepuka uwezekano wa kuongezewa gharama baada ya makubaliano kupishana na uhalisia (variations) ya kitu chochote.Lakini hii haizuii kujadiliana baina yetu na mteja kama kuna mabadiliko ya muhimu na kukubaliana.

5. Namna ya tano sahihi ya kupunguza gharama za ujenzi ni manunuzi ya jumla ya vifaa vya ujenzi. Mahitaji yote ya mradi husika unakaa chini na wataalam wetu tukapanga aina ya vifaa vya ujenzi kadri ya mazingira uliyopo. Jambo hili linahitaji umakini mkubwa sana kwa sababu, tunapokea simu za wanaoomba ushauri baada ya kufika mbele ya safari katika huo ujenzi na kukuta kilichonunuliwa hakifai au pengine kimeharibika na hakifai tena kwa sehemu iliyokusudiwa. Tunashauri anza na mtaalam wa ujenzi unayemwamini ili usije kujikuta unajiingiza kwenye hasara badala ya kupunguza gharama.

Tumeambatanisha nyumba ya vyumba viwili,sebule,choo cha ndani na jiko tulojenga kwa milioni 12 tu,ikikamilika ndani ya siku 60, tukiokoa 40% ya gharama ukifananisha na wengine walojenga ramani kama hii.(Wengi wametumia kuanzia milioni 20).

Kwa ushauri bure juu ya ujenzi, au huduma za kujenga nyumba bora huku ukipunguza gharama, wasiliana nasi

0713 039 875 au 0742 499 177

Drone Online Ads

View attachment 1619812View attachment 1619814View attachment 1619815View attachment 1619816
Kama ushauri wako utapelekea kupata nyumba za quality hii basi siutaki
 
Back
Top Bottom