Namkumbuka Rashid Kheri Baghdelleh, rafiki wa Baba yangu

Mohamed Said

JF-Expert Member
Nov 2, 2008
20,839
30,168
NAMKUMBUKA RASHID KHERI BAGHDELLEH RAFIKI WA BABA YANGU

Anza kwa kuangalia picha hapo chini.

Baba Said Salum, Babu Salum Abdallah na juu ni Kheri Rashid Baghdelleh.

Baba na Baghdelleh wakifahamiana toka udogo wao Dar es Salaam ile ya 1950s.

Baghdelleh baada ya uhuru akawa Regional Commissioner, Western Province babu wakati ule Mwenyekiti wa Tanganyika Railways African Union (TRAU).

Nilipokwenda Tabora likizo nilimuona Baghdelleh na Humber yake nyeusi gari la Kiingereza.

Baghdelleh kijana wa Kinubi, babu yangu Mmanyema wote watu wa TANU hao wakati wa kupigania uhuru.

Baghdelleh yuko gazeti la Mwafrika kitengo cha propaganda cha TANU dhidi ya Waingereza.

Mgomo wa Railways wa 1960 Mwafrika linautangaza kwa vishindo kiongozi wa mgomo Salum Abdallah na Kassanga Tumbo.

TRAU na TANU wako bega kwa bega dhidi ya Edward Twining na serikali yake.

Babu yangu shujaa mgomo umedumu miezi mitatu hadi Mwingereza kasalimu amri kaomba mazungumzo.

Wameelewana mgomo umekwisha salama.

Mwaka 1961 uhuru umepatikana.

Nyerere, Kawawa na Kamaliza wanataka vyama huru vya wafanyakazi mfano wa TRAU vivunjwe kiundwe chama kimoja tu na kiwe chini ya TANU.

Hapo ndipo Salum Abdallah na Nyerere walipopambana.

1964 Salum Abdallah akajikuta yuko kizuizini Jela ya Uyui kwa tuhuma za kutaka kupindua serikali na kumuua Nyerere.

Baghdelleh na Bwana Jela Munthali wanaingia ndani ya selo kuzungumza na "wahaini."

Mmoja wa hawa wahaini ni Bilal Rehani Waikela.

Munthali anamjua babu yangu vizuri ni baba ya rafiki yake lakini zaidi ni mpambanaji mwenzake enzi za kupigania uhuru wa Tanganyika.

Munthali na Baghdelleh walikuwa na uso gani wa kumtazama Salum Abdallah?

Baba yangu alimwuliza Baghdelleh ampe ukweli kwa nini khasa baba yake kawekwa kizuizini?

Baghdelleh hakumficha baba ukweli.

Alimweleza sababu ya babu kufungwa na kuitwa, "mhaini."

Mara ya mwisho kumuona Rashid Kheri Baghdelleh alikuja nyumbani kumuona baba yangu.

Haikupita miaka mingi Baghdelleh akafa katika ajali ya gari Arusha.

Screenshot_20210806-214147_Facebook.jpg
 
Nanakupongeza sana Mzee Mohamed kwa kuandika huu uzi bila kumtaja SYKES. Hii ni hatua muhimu kwako.
Dira,
Ikiwa historia ni ya African Association (1929), TAA,(1950), TANU (1954), Julius Nyerere (1952) na kupigania uhuru wa Tanganyika huwezi kuieleza kwa ukweli wake bila kumtaja Abdulwahid Kleist Sykes.

Wako kama wewe walikuwa wanataabishwa na kuona historia nzima ya uhuru wa Tanganyika akina Sykes wako kila mahali wakaamua labda kwa ajili ya hasad, choyo na wivu kuwakwepa wakajipachika wao.

Kilichoandikwa ikawa siyo historia ya kweli.

Ukiwakwepa hawa inabidi umkwepe na baba yao muasisi wa African Association na harakati za siasa Tanganyika.

Itabidi pia ukwepe kueleza vipi Julius Nyerere alivyopokelewa Dar es Salaam na vipi alikuja kuongoza TANU.

Nyerere alipokelewa na Abdul Sykes na haya kayaeleza mwenyewe baada ya kuwa kimya kwa miaka mingi.

Baba, Kleist Sykes founding Secretary AA, mtoto, Abdul Sykes Act. President na Secretary TAA 1950 - 1953, founder member TANU 1954 kadi yake no. 3 no. 2 Ally Sykes no. 7 Abbas Sykes.

Historia hiyo niliyoandika ni historia ya babu yangu, baba yangu, Baghdelleh na jinsi babu alivyowekwa kizuizini 1964.

Ingekuwa ni historia ya TANU ungewasoma waliounda TANU na wafadhili wake kwa ajili hiyo ungewaona Sykes wote.

Hiyo pongezi uliyonipa sistahili hata kidogo kwani si haki yangu.

"Hatua muhimu," chembelecho kwangu ni kuandika historia ya Abdul Sykes na kuieleza historia ya kweli ya TANU si kumkwepa kumwandika kama muasisi wa TANU na sifa zake nyingine nyingi.

Mimi ndiye niliyopewa jukumu la kumwandika Kleist Sykes katika Dictionary of African Biography (DAB)hizi ni volume sita zimechapwa na Oxford University Press, New York (2011) na ni mradi wa Harvard na Oxford University Press New York.

Sykes unawakuta ndani ya hilo Kamusi la watu mashuri Afrika hapo juu lakini kwenye kitabu kilichoandikwa na TANU Tanzania hayumo.

Hakika haya ni maajabu.
Kuna kitu hapa si bure.

Ati pongezi kwa kutomtaja Sykes.

Pongezi hizo wapelekee Chuo Cha CCM Kivukoni wao ndiyo wanastahili maana wameweza kuandika historia ya TANU bila kumtaja Abdul Sykes, nduguze na baba yao.

Screenshot_20210807-220109_Photos.jpg
 
View attachment 1884648
Mzee Mohamed tatizo nini kukataa pongezi zangu za dhati. Huoni kama uzi wako uko kipekee bila jina la SYKES? Huu uzi unasomeka na watu wa itikadi zote.
 
Nanakupongeza sana Mzee Mohamed kwa kuandika huu uzi bila kumtaja SYKES. Hii ni hatua muhimu kwako.
POLE SANA. KWA HUWA UNAUMIA SANA UNAPOLIONA JINA LA BABU YAKE DULLY SYKES? INAPOBIDI KUTAJWA FAMILIA YA SYKES, ITATAJWA TU. NA KAMA HILO ANDIKO HALIMHUSU SYKES, BASI HATOANDIKWA.
 
Mzee Mohamed tatizo nini kukataa pongezi zangu za dhati. Huoni kama uzi wako uko kipekee bila jina la SYKES? Huu uzi unasomeka na watu wa itikadi zote.
Dira,
Nimeeleza naamini vizuri kwa wewe na yeyote yule kuelewa kwa nini ikiwa ni historia ya TANU na uhuru wa Tanganyika huwezi kuacha kumtaja Abdul Sykes.

Jaribu kuandika historia ya vijiji vya ujamaa bila ya kumtaja Julius Nyerere.

Nimekuletea mfano huo hapo juu ya ujamaa vijijini kukuzindua.

Sijui watu wa itikadi gani wananisoma lakini ikutoshe tu kuwa vitabu vyangu vimechapwa na Oxford University Press, Nairobi na New York, Minerva Press London, Abantu Publications Nairobi, Phoenix Publishers Nairobi na Ibn Hazm Dar es Salaam.

Ninavyofahamu mimi Oxford University Press wanawaandikia wasomaji wa dunia nzima na mimi ni mmoja katika orodha ya waandishi wake.

Wewe unaniambia kuwa kuna wasomaji hawanisomi na sababu hawapendi historia ya Sykes.

Itikadi yao hairuhusu kumsoma Sykes.

Hassan Upeka mmoja wa waandishi wa kitabu, "Historia ya TANU," alishangazwa na jibu alilopewa na kiongozi wa jopo la waandishi wa Chuo Cha CCM Kivukoni pale alipowaeleza wanajopo wenzake kuwa bila ya kumtaja Abdul Sykes hicho wanachoandika haitakuwa historia ya TANU.

Yule kiongozi alimwambia Upeka kuwa historia wanayoandika haina uhusiano wowote na Abdul Sykes.

Hili jibu ndilo lililomshangaza Hassan Upeka.

Walikusanyika watu Ukumbi wa Mondlane, Northwestern University, Evanston Chicago, Illinois kuja kumsikiliza Mohamed Said akimzungumza Abdul Sykes katika historia ya TANU na kupigania uhuru wa Tanganyika.

Hawa walikuwa wataalamu wa African History katika vyuo vikuu vya Marekani.

Hawa ni wasomi wa itikadi ipi?
Je, unawatambua watu hawa?

Mimi nasomeka na nasikilizwa pia.
Bahati mbaya sijapata kuchunguza ni watu wa itikadi gani wanaonisoma na kunisikiliza pia.

1628453580742.png
 
View attachment 1885709
Mzee Mohamed sina shaka kabisa na kiwango cha usomi wako. Mimi pia nakukubali sana kwa kuwa ni msomi ambaye pia una exposure ya kutosha. Isitoshe umezaliwa na kukulia mjini. Kinachonikwaza ni karibu kila andiko lako lazima jina la Sykes liibuke. Hata ukiandika taazia ya mtu kuna sentensi lazima iwe na SYKES. Hata kama ni ufuasi huu wako ni kero.
 
Nimecheka kidogo.

Hebu rejea na soma post iliyopita nimekueleza Chuo Cha CCM Kivukoni wamekataa kuingiza jina la Abdul Sykes katika historia ya TANU waliyokuwa wanaandika mwaka wa 1981.

Hili halijakushangaza unanishangaa mimi kwa kumtaja Abdul Sykes na kuona ni ''kero.''

Chuo Cha CCM Kivukoni bila shaka na wao waliona ni kero pia kama unavyoona wewe kuwa jina la Abdul Sykes litajwe.

Hata alipokufa magazeti ya TANU yalikataa kumwandika anavyostahili.

Brendon Grimshaw Mhariri wa Tanganyika Standard ndiye alichapa taazia ya Abdul Sykes.

Ndiyo nimesema umenifurahisha hadi nimecheka.

Inakuwaje nyote nyie chembelecho, ''mkwazike,'' na jina la Sykes?

Uhuru na Nationalist magazeti ya TANU, wakwazike, Chuo Cha CCM Kikwazike, wewe ukwazike...

Mnakwazika na Abdul Sykes aliyeunda chama cha TANU akakifadhili kwa mapesa yake akampokea Nyerere na kuishinae nyumbani kwake awakwaze...

Hivi inakuwaje hivi?

Hivi unajua Nyerere alipotoka kwa Msajili wa Vyama kusajili TANU alikwenda nyumbani kwa Ally Sykes Mtaa wa Kipata (sasa Mtaa wa Sykes) alipokuwa anasubiriwa kuwasilisha taarifa kwa Abdul na Ally Sykes?

1628455781040.png

1628455868485.png

Hii ni taazia ya Brendon Grimshaw aliyochapa katika Sunday News kumuadhimisha Abdul Sykes baada ya kifo chake 1968.
 
Ukapimwe akili wewe mzee. Haupo sawa kichwani na hakuna anayeamini uwongo wako wa Sykes. Iweje kichaa mmoja tu aendeshe kampeni ya Sykes dunia nzima?

Screenshot_20210809-072519_Facebook.jpg

MRADI WA DICTIONARY OF AFRICAN BIOGRAPHY (DAB) MWAKA WA 2008

Baada ya matatizo yaliyoniandama katika vitabu hivyo viwili nilivyoandika siku moja mwaka wa 2008 nikapokea email kutoka kwa Prof. Emmanuel Akyeampong kutoka Harvard akaniomba niwe mmoja wa waandishi karibu 500 kutoka kila pembe ya dunia watakaoandika kamusi ya watu mashuhuri Afrika.

Mradi huu ulikuwa unajulikana kama Dictionary of African Biography.

Huu ulikuwa mradi wa Harvard na Oxford University Press New York.

Prof. Akyeampong akaniomba pia niwe mshauri wake kwa majina ya Watanzania ambao mimi naona wamefanya makubwa kwa hiyo wanastahili maisha yao kuandikwa katika hii kamusi.

Prof. Akyeampong akaniomba mimi niandike maisha ya Kleist Sykes yeye akimkusudia Kleist Abdulwahid Sykes.

Mimi hapo hapo nikaanza kazi yangu ya ushauri.

Nikalikata jina la Mayor wa Jiji la Dar es Salaam rafiki na ndugu yangu Kleist, nikamshauri kuwa anaestahili kuingia katika DAB ni babu yake, Kleist Sykes Mbuwane (1894 - 1949) na si huyu Kleist mtoto wa Abdul Sykes.

Prof. Akyeampong alivutiwa sana na kile alichosoma kuhusu babu yake Kleist Abdulwahid na kamusi ilipochapwa mwaka wa 2011 maisha ya Kleist Sykes Mbuwane babu yake Kleist Abdulwahid yakawa ndani ya DAB.

Abdul na Ally na wao pia wametajwa pamoja na baba yao katika historia ya kupigania uhuru wa Tanganyika.

DAB ina volume sita na ni maarufu hivi sasa duniani kama kitabu cha rejea kwa watu mashuhuri na mashujaa wa Bara la Afrika.
 
Dira,
Ikiwa historia ni ya African Association (1929), TAA,(1950), TANU (1954), Julius Nyerere (1952) na kupigania uhuru wa Tanganyika huwezi kuieleza kwa ukweli wake bila kumtaja Abdulwahid Kleist Sykes.

Wako kama wewe walikuwa wanataabishwa na kuona historia nzima ya uhuru wa Tanganyika akina Sykes wako kila mahali wakaamua labda kwa ajili ya hasad, choyo na wivu kuwakwepa wakajipachika wao.

Kilichoandikwa ikawa siyo historia ya kweli.

Ukiwakwepa hawa inabidi umkwepe na baba yao muasisi wa African Association na harakati za siasa Tanganyika.

Itabidi pia ukwepe kueleza vipi Julius Nyerere alivyopokelewa Dar es Salaam na vipi alikuja kuongoza TANU.

Nyerere alipokelewa na Abdul Sykes na haya kayaeleza mwenyewe baada ya kuwa kimya kwa miaka mingi.

Baba, Kleist Sykes founding Secretary AA, mtoto, Abdul Sykes Act. President na Secretary TAA 1950 - 1953, founder member TANU 1954 kadi yake no. 3 no. 2 Ally Sykes no. 7 Abbas Sykes.

Historia hiyo niliyoandika ni historia ya babu yangu, baba yangu, Baghdelleh na jinsi babu alivyowekwa kizuizini 1964.

Ingekuwa ni historia ya TANU ungewasoma waliounda TANU na wafadhili wake kwa ajili hiyo ungewaona Sykes wote.

Hiyo pongezi uliyonipa sistahili hata kidogo kwani si haki yangu.

"Hatua muhimu," chembelecho kwangu ni kuandika historia ya Abdul Sykes na kuieleza historia ya kweli ya TANU si kumkwepa kumwandika kama muasisi wa TANU na sifa zake nyingine nyingi.

Mimi ndiye niliyopewa jukumu la kumwandika Kleist Sykes katika Dictionary of African Biography (DAB)hizi ni volume sita zimechapwa na Oxford University Press, New York (2011) na ni mradi wa Harvard na Oxford University Press New York.

Sykes unawakuta ndani ya hilo Kamusi la watu mashuri Afrika hapo juu lakini kwenye kitabu kilichoandikwa na TANU Tanzania hayumo.

Hakika haya ni maajabu.
Kuna kitu hapa si bure.

Ati pongezi kwa kutomtaja Sykes.

Pongezi hizo wapelekee Chuo Cha CCM Kivukoni wao ndiyo wanastahili maana wameweza kuandika historia ya TANU bila kumtaja Abdul Sykes, nduguze na baba yao.

View attachment 1884648
Maalim wangu,Sheikh Mohammed Said.. Naomba ufafanuz..
Naomba Nitajie Matajir walokuwa wanaifadhili Tanu Miaka ya 1950,ningependa niwafaham majina yao..
Shukran
 
Always...
Niruhusu nilitengeneze swali lako.

Ili kupata picha kamili itakuwa vyema tukianza historia hii ya wafadhili toka enzi za African Association.

African Association (AA) iliasisiwa Dar es Salaam mwaka wa 1929 Kleist Sykes akiwa Katibu muasisi.

Katika waasisi hawa Kleist ndiye aliyekuwa na uwezo mkubwa wa fedha kushinda wenzake wote kwa kuwa mbali na kuwa mfanyakazi wa Tanganyika Railways alikuwa pia akifanya biashara ya duka la "pilipili bizari" kisha akafungua duka la kuuza vifaa vya ujenzi na baadae akafungua kampuni Sykes and Sons katika miaka ya 1940s wanae walipokwenda kupigana Burma Vita Vya Pili Vya Dunia 1939 - 1945.

Hii kampuni ya Sykes and Sons ilimiliki machimbo ya chokaa Kigamboni na ndiyo iliyomnyanyua sana Kleist.

Kuwa na machimbo ya chokaa wakati ule ilikuwa sawa na mtu kuwa na kiwanda cha kutengeneza rangi mfano wa Sadolin Paint kwa kuwa nyakati zile nyumba nyingi zikipakwa chokaa.

Kleist alikuwa na nyumba kadhaa alizopangisha.

Kleist alikuwa mfadhili no. 1 wa AA na Al Jamiatul Islamiyya fi Tanganyika (Umoja wa Waislam wa Tanganyika) vyama ambavyo yeye alikuwa Katibu muasisi.

Aziz Ali yeye alikuwa mfadhili mkubwa katika mambo ya Uislam lakini mwanae Dossa Aziz yeye alijitolea zaidi katika kufadhili AA na TANU.

African Association ilikuwa na matawi sehemu nyingi katika majimbo lakini matawi maarufu yalikuwa Kanda ya Ziwa na Dodoma.

Kanda ya Ziwa mfadhili Mkuu alikuwa Mzee Bomani na mwanae Paul.

Bahati mbaya historia za wafadhili wengine hazifahamiki mathalan Aikael Mbowe yeye alikuwa mfadhili mkubwa wa TANU.

Wafadhili wa TANU kuanzia 1954 ni hawa hawa waliofadhili AA kati ya 1929 na matawi yalipofunguliwa majimboni.

Dar es Salaam uasisi wa AA kama ilivyokuja kwa TANU ukoo wa Sykes ulikuwa na ushawishi mkubwa katika uasisi na ufadhili wake.

Wafadhili wakubwa wa TANU Dar es Salaam walikuwa John Rupia ambae alikuwa mfanyabiashara mkubwa, Dossa Aziz yeye alirithi mali ya baba yake Aziz Ali na Abdul na Ally Sykes.

Mfadhili mwengine wa TANU alikuwa Mzee Mshume Kiyate.

Mfadhili mkubwa wa TAA na TANU Lindi alikuwa Suleiman Masudi Mnonji.

Tanga kulikuwa na wafadhili wawili wa TANU - Makata Mwinyi Mtwana na Sadik Patwa, Muhindi aliyekuwa na kiwanda cha soda.

Hii historia haija kamilika wako wafadhili wengi ambao historia zao hazifahamiki.

Naona tabu kueleza historia ya babu yangu Salum Abdallah.

Yeye baada ya kuwekwa kizuizini 1964 alipotoka jela alikaa mbali na TANU hadi alipofariki 1974.

Lakini katika mazishi yake TANU ilijitokeza na walisoma risala wakamsifia kwa ukarimu wake kwa TANU wakati wa kupigania uhuru wa Tanganyika.

1628570189908.png

Picha ilipigwa katika mgahawa wa Sadiki Patwa Tanga wakiwemo Mwalimu JK Nyerere na Bw. Patwa kulia kwake unapoitazama picha. Kulia mwenye koti na kofia Mzee Rashid Makoko na wa pili yake ni mwanae Rashid Mamboleo Makoko na kushoto mwenye koti na kofia Mzee Makata Mwinyimtwana Mwafrika tajiri mkubwa Tanga katika miaka ya 1950/60.
 
Always...
Niruhusu nilitengeneze swali lako.

Ili kupata picha kamili itakuwa vyema tukianza historia hii ya wafadhili toka enzi za African Association.

African Association (AA) iliasisiwa Dar es Salaam mwaka wa 1929 Kleist Sykes akiwa Katibu muasisi.

Katika waasisi hawa Kleist ndiye aliyekuwa na uwezo mkubwa wa fedha kushinda wenzake wote kwa kuwa mbali na kuwa mfanyakazi wa Tanganyika Railways alikuwa pia akifanya biashara ya duka la "pilipili bizari" kisha akafungua duka la kuuza vifaa vya ujenzi na baadae akafungua kampuni Sykes and Sons katika miaka ya 1940s wanae walipokwenda kupigana Burma Vita Vya Pili Vya Dunia 1939 - 1945.

Kleist alikuwa na nyumba kadhaa alizopangisha.

Kleist alikuwa mfadhili no. 1 wa AA na Al Jamiatul Islamiyya fi Tanganyika (Umoja wa Waislam wa Tanganyika) vyama ambavyo yeye alikuwa Katibu muasisi.

Aziz Ali yeye alikuwa mfadhili mkubwa katika mambo ya Uislam lakini mwanae Dossa Aziz yeye alijitolea zaidi katika kufadhili AA na TANU.

African Association ilikuwa na matawi sehemu nyingi katika majimbo lakini matawi maarufu yalikuwa Kanda ya Ziwa na Dodoma.

Kanda ya Ziwa mfadhili Mkuu alikuwa Mzee Bomani na mwanae Paul.

Bahati mbaya historia za wafadhili wengine hazifahamiki mathalan Aikael Mbowe yeye alikuwa mfadhili mkubwa wa TANU.

Wafadhili wa TANU kuanzia 1954 ni hawa hawa waliofadhili AA kati ya 1929 na matawi yalipofunguliwa majimboni.

Dar es Salaam uasisi wa AA kama ilivyokuja kwa TANU ukoo wa Sykes ulikuwa na ushawishi mkubwa katika uasisi na ufadhili wake.

Wafadhili wakubwa wa TANU Dar es Salaam walikuwa John Rupia ambae alikuwa mfanyabiashara mkubwa, Dossa Aziz yeye alirithi mali ya baba yake Aziz Ali na Abdul na Ally Sykes.

Mfadhili mwengine wa TANU alikuwa Mzee Mshume Kiyate.

Mfadhili mkubwa wa TAA na TANU Lindi alikuwa Suleiman Masudi Mnonji.

Tanga kulikuwa na wafadhili wawili wa TANU - Makata Mwinyi Mtwana na Sadik Patwa, Muhindi aliyekuwa na kiwanda cha soda.

Hii historia haija kamilika wako wafadhili wengi ambao historia zao hazifahamiki.

Naona tabu kueleza historia ya babu yangu Salum Abdallah.

Yeye baada ya kuwekwa kizuizini 1964 alipotoka jela alikaa mbali na TANU hadi alipofariki 1974.

Lakini katika mazishi yake TANU ilijitokeza na walisoma risala wakamsifia kwa ukarimu wake kwa TANU wakati wa kupigania uhuru wa Tanganyika.

View attachment 1886805
Picha ilipigwa katika mgahawa wa Sadiki Patwa Tanga wakiwemo Mwalimu JK Nyerere na Bw. Patwa kulia kwake unapoitazama picha. Kulia mwenye koti na kofia Mzee Rashid Makoko na wa pili yake ni mwanae Rashid Mamboleo Makoko na kushoto mwenye koti na kofia Mzee Makata Mwinyimtwana Mwafrika tajiri mkubwa Tanga katika miaka ya 1950/60.
Tatizo Mzee Mohamed inaonekana baadhi ya waliofadhili ilikuwa ni kwa malengo binafsi badala ya watanzania wote. Ilikuwa lazima wageukwe ili kutoweza kutimiza nia zao za kibinafsi.
 
Dira...
Katika hiyo orodha niliyokuletea kwanza tuanze na African Association mfadhili Kleist Sykes alikuwa na malengo yapi katika umri wake ndani ya siasa za Tanganyika 1929 - 1949 alipofariki kuhitaji ageukwe na nani amgeuke.

Wanae watatu Abdulwahid, Ally na Abbas ndani ya TAA na TANU walikuwa na malengo gani yaliyohitaji wageukwe.

Suleiman Masudi Mnonji alikuwa na na malengo yapi, Mshume Kiyate, Dossa Aziz, John Rupia, Paul Bomani na baba yake kwa kuwataja wachache hawa wote walikuwa na malengo gani kuanzia 1950s hadi uhuru unapatikana 1961.

Unadhani unasema ''inaonekana,'' wewe umeona nini?

Hebu tufahamishe tujue.

Hao unawaeleza kuwa waligeuka watu wao walikuwa na kipi zaidi ya hao wengine kiasi wawe na haki ya kuwa mahakimu?

Babu yangu alikuwa na orodha yake ya vibaraka walioisaliti Tanganyika na majina yao yote ninayo.

Ningependa sana kukusikia na wewe ili nilinganishe.
 
Dira...
Katika hiyo orodha niliyokuletea kwanza tuanze na African Association mfadhili Kleist Sykes alikuwa na malengo yapi katika umri wake ndani ya siasa za Tanganyika 1929 - 1949 alipofariki kuhitaji ageukwe na nani amgeuke.

Wanae watatu Abdulwahid, Ally na Abbas ndani ya TAA na TANU walikuwa na malengo gani yaliyohitaji wageukwe.

Suleiman Masudi Mnonji alikuwa na na malego yapi, Mshume Kiyate, Dossa Aziz, John Rupia, Paul Bomani na baba yake kwa kuwataja wachache hawa wote walikuwa na malengo gani kuanzia 1950s hadi uhuru unapatikana 1961.

Unadhani unasema ''inaonekana,'' wewe umeona nini?

Hebu tufahamishe tujue.

Hao unawaeleza kuwa waligeuka watu wao walikuwa na kipi zaidi ya hai wengine kiasi wawe na haki ya kuwa mahakimu?

Babu yangu alikuwa na orodha yake ya vibaraka walioisaliti Tanganyika na majina yao yote ninayo.

Ningependa sana kukusikia na wewe ili nilinganishe.
Utatundekea haki km utatujuza na hao waliowazunguka wenzi wao
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom