X_INTELLIGENCE
JF-Expert Member
- Mar 25, 2014
- 9,647
- 12,215
" Mimi kugombea urais kwangu siyo tatizo, ila nataka kuweka mambo sawa.
Hata nisipogombea hiyo hainizuii kwenda mbinguni.
Kwanza mtu mwenye uchu wa madaraka ya kwenda Ikulu anatakiwa kuepukwa kama ukoma."
Nukuu ya mwanasiasa na mwanaharakati mkongwe, marehemu mchungaji Christopher Mtikila, siku chache kabla ya kifo chake.
Mtikila alifariki October 4, 2015 kwa ajari ya gari katika kijiji cha Msolwa, Chalinze mkoani Pwani. Alizaliwa mwaka 1950 mkoani Iringa.
Ikiwa ni mwaka sasa tangu atutoke Mchungaji Mtikila anakumbukwa kwa kuwa mtu mwenye misimamo mikali na asiye ogopa chochote huku akikumbukwa kwa kuwa mstari wa mbele kudai uhuru wa Tanganyika na mara kadhaa alichoma moto bendera ya Tanzania na kumtukana waziwazi rais wa kwanza wa Tanzania, Mwalimu Julius Nyerere.
Mpaka anafariki Mchungaji Mtikila ameacha shauri Mahakama Kuu ya Tanzania akipinga kuzuiwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi ya Tanzania ( NEC ) kugombea urais kupitia chama chake cha DPP katika uchanguzi mkuu uliofanyika wiki chache baada ya kifo chake
Mwenyezi Mungu akulaze mahala pema peponi mzee wetu umetangulia naamini mema uliyoyafanya yatabaki kufanya ukumbukwe daima