Namkubali sana Dr. JPM lakini natamani arekebishe na hili

doublep

JF-Expert Member
Jan 8, 2015
241
152
Wapendwa wana JF, nimelileta hili kwa sababu linaniuma sana.
Mimi ni Mtaalamu katika sekta ya Elimu. Kiukweli najua na kuamini kuwa Elimu yetu Tanzania inashukuka kila siku kwa sababu mbalimbali za kuingiza siasa kwenye mambo ya kitaalamu.
Kwa mfano
1.kuweka maswali ya kuchagua katika masomo yote mtihani wa darasa la saba. Hii ina lengo la kuonesha ufaulu mkubwa kesho watu wajisifu watoto wanafaulu sana
2. Kupunguza wastani wa ufaulu form two.
Na kadhalika. Hiyo ni mifano michache ipo mingi.
Naamini siasa zikiondolewa kwenye taaluma mbalimbali Elimu yetu itapanda.
Karibuni wana jamvi tujadili labda litamfikia JPM na nonaamini atarekebisha.
 
Back
Top Bottom