Namkubali mama Tibaijuka, lakini nimeona doa la kwanza kwake leo

Watanzania acha kulalamika kila kitu, nchi imeshindwa kuendelea kwa vitu kama hivi, Kigamboni ni strategic area,Daudi Mchambuzi anahoji kwa nini Kigamboni? jibu ni kwamba Kigamboni ni strategic area kama ambavyo wamarekani waliamua manhatan iwe strategic business centre.

Bigup mama Tibaijuka hayo ndo maamuzi magumu tunayotakiwa kufanya kama wananchi na viongozi kwa ujumla. Ulalamishi hautusaidii ingawa ni kweli pia katika kutafuta kizuri kuna watakaoumia, na hili sio geni kwa aliyeshawahi kwenda vitani analifahamu.
 
Tsh 60 bn ni hela ndogo sana kwa mradi kama ule. Lakini amesema watatumia mbinu 'za kisasa' kutafuta hela zingine nje ya bajeti.

Jambo moja ambalo nadhani mama Tibaijuka anatakiwa awe makini ni huu mtindo wake wa kutumia maneno ambayo yanawashusha watu chini. Kwa mfano 'tutatumia mbinu za kisasa'! hapa anaongea na watu wa zama za ujima? Kwa nini asiwe specific? Au ndio mambo ya nshomile, lazima ujikweze kidogo na elimu?
Kwa watu kama wewe nadhani tatizo lenu ni "nshomile" kwanza, hoja baadae. Nshomile ngozi ngumu. Kejeli, dharau na wivu vingekuwa vinaunguza nshomile wote tungekuwa mishikaki. Mbona wengine wakifanya madudu, tena makubwa mno, hamuhoji asili zao? Ha!!!
 
Kwa watu kama wewe nadhani tatizo lenu ni "nshomile" kwanza, hoja baadae. Nshomile ngozi ngumu. Kejeli, dharau na wivu vingekuwa vinaunguza nshomile wote tungekuwa mishikaki. Mbona wengine wakifanya madudu, tena makubwa mno, hamuhoji asili zao? Ha!!!


Soma tena, nimeuliza swali, lakini sioni kama umenipa jibu.
 
Ni vyema tukampa nafasi tuone mradi utafikia wapi! Ila huyu mama ana jitahidi sana

Note, no one is parfect.
 
Unataka ukuu wa wilaya CDM wakishinda??


Duh! MAGAMBA bwana mkiambiw ahata kama mnawachukia someni sera zao hamtaki.
NAPE wape shule kwanza hawa vijana kabla ya kumpiga ADUI lazima umsome kwanza na ndio mana wengi humu wa MAGAMBA Hamuwezi hoja zaidi ya Vioja kwa kuwa hamataki kusoma wala kufikiri,

Kwa tarifa tu ni kuwa CDM hawana CHEO KAMA HIKO KWENYE SEREKALI YAO>
 
tibaijuka alieleza vizuri tu jana ikiwa kweli atafanya kama yote aliyoyasema jana pamoja na changamoto ndogondogo tunaweza kusogea.
japo hajasema kuhusu ardhi iliyochukuliwa na wageni kinyemela na wananchi kutupwa kando na huku serikali ikipata pato kidogo kwamba atafanya nini
 
Mama Tibaijuka alikuwa mzuri kipindi yupo UN ila mfumo mbovu wa TZ umeshamuaribu kabisaaa!

Sent from my BlackBerry 9800 using JamiiForums
 
mm nimemsikiliza, kwa kweli mama ni mzalendo wa ukweli

na inaonyesha ana hamu na shauku na dhamira ya dhati kutuletea mabadiliko. tumuungeni mkono
 
Mkuu ungenisaida sana kuorozesha mafanikio ambayo nchi iliyapata kwa kuwepo Tibaijuka huko UN- HABITAT kama siyo yeye kupata pesa nakuwapeleka watoto wake kusoma outside which is personal benefit.
 
Huyu mama ni msemaji mzuri,lakini bado hana jawabu la matatizo ya wizara yake,si rahisi kuonyesha ufanisi katika mfumo unaoleta kushindwa.Pesa kidogo tulionayo iendane na matumizi,pia watu wenye uwezo na kazi hasa kitaaluma,
 
Back
Top Bottom