Namkubali mama Tibaijuka, lakini nimeona doa la kwanza kwake leo | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Namkubali mama Tibaijuka, lakini nimeona doa la kwanza kwake leo

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Maseto, Jul 12, 2012.

 1. M

  Maseto JF-Expert Member

  #1
  Jul 12, 2012
  Joined: Apr 3, 2012
  Messages: 710
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 45
  Nilimsikiliza kwa makini jana Profesa Tibaijuka juu ya mradi wa Kigamboni.Aliposema juu ya kuwapeleka baadhi ya wananchi wa kigamboni kutembelea miji mbalimbali kujifunza juu ya miji bora,nilianza kuhisi kuwa kuna tatizo juu ya huu mradi.Mimi naishi kijiji fulani huku Mtwara lakini huwa nafuatilia mambo ya mjini.
  Nilimsikiliza pia mbunge wa Kigamboni jana na leo.Lakini kilichonishitua zaidi ni maelezo ya Tibaijuka wakati wa majumuisho.Kwa kiwango fulani hakuwa yule mama ninayemfahamu.
  Kuna mambo matatu hajaeleweka juu ya mradi wa Kigamboni:
  1. Inakuwaje waziri kuwapeleka baadhi ya wananchi kujifunza nje wakati hilo si tatizo lao.Tatizo lao ni namna mradi utakavyowafaidisha wao.
  2. Mchanganuo wa matumizi ya pesa iliyotengwa yakoje.Pesa shilingi 60 bilioni ni ndogo sana kwa mradi mkubwa kama ule.
  Nimeshindwa kumuelewa Mama leo.Inatisha kuona kuwa mama aleyefanya mafanikio makubwa duniani anakuwa haeleweki hivi!
  3. Suala la kuwaalika Madiwani hao wanne lilitakiwa kutolewa maelezo ya kina.

  Mimi nasema kuna tatizo juu ya mradi huu wa Kigamboni.Pengine kuna mambo yaliyojificha ambayo hatuambiwi vizuri.
   
 2. F

  FJM JF-Expert Member

  #2
  Jul 13, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 8,090
  Likes Received: 81
  Trophy Points: 145
  Tsh 60 bn ni hela ndogo sana kwa mradi kama ule. Lakini amesema watatumia mbinu 'za kisasa' kutafuta hela zingine nje ya bajeti.

  Jambo moja ambalo nadhani mama Tibaijuka anatakiwa awe makini ni huu mtindo wake wa kutumia maneno ambayo yanawashusha watu chini. Kwa mfano 'tutatumia mbinu za kisasa'! hapa anaongea na watu wa zama za ujima? Kwa nini asiwe specific? Au ndio mambo ya nshomile, lazima ujikweze kidogo na elimu?
   
 3. a

  afwe JF-Expert Member

  #3
  Jul 13, 2012
  Joined: Oct 29, 2010
  Messages: 4,077
  Likes Received: 108
  Trophy Points: 160
  Bilioni 60 ni kwa ajili ya kulipa fidia kwa wananchi kwa mwaka huu wa fedha. Isije kuwa sisis ndio hatukuelewa
   
 4. a

  andrews JF-Expert Member

  #4
  Jul 13, 2012
  Joined: Mar 28, 2012
  Messages: 1,682
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  huyu muha ya wa muleba aende muleba akasaidie vibibi visibakwe hana jipya mtoto wa nyoka ni nyoka na samaki mmoja akioza wote wameoza ndani ya ccm hakuna mkweli wote ni wazandiki wakubwa:eek2:
   
 5. m

  mambomengi JF-Expert Member

  #5
  Jul 13, 2012
  Joined: May 16, 2009
  Messages: 829
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 35
  Ukitaka kujua ugumu wa kuongoza wizara za CCM Tanya kazi wizarani ujue madudu yaliyomo na mawaziri na wakurugenzi wanavyolazimishwa kupika madudu from upstairs
   
 6. m

  mambomengi JF-Expert Member

  #6
  Jul 13, 2012
  Joined: May 16, 2009
  Messages: 829
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 35
  Ukitaka kujua ugumu wa kuongoza wizara za CCM Tanya kazi wizarani ujue madudu yaliyomo na mawaziri na wakurugenzi wanavyolazimishwa kupika madudu from upstairs
   
 7. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #7
  Jul 13, 2012
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 59,115
  Likes Received: 32,721
  Trophy Points: 280
  Mkuu FJM, hakuna mbinu za kisasa zozote bali ni usanii tu. Kama kuna "mbinu za kisasa za kutafuta pesa" kwanini zisitumike ili kutimiza madai ya madaktari au kutimiza ile ngojera ya DHAIFU "Maisha bora kwa kila Mtanzania yanawezekana."

  Kama kwaida yao wamekurupuka bila kufanya tathmini ya kina hivyo mradi huo hautafanikiwa halafu tutarudi pale pale kwenye ngojera nyingine ya DHAIFU "Serikali haina uwezo" ya kumalizia mradi wa kigamboni huku wachukuaji wakiendelea kuzoa mabilioni ya Watanzania kila kukicha kupitia rasilimali za Watanzania mbali mbali zikiwemo dhahabu, almasi, uranium, Tanzanite, wanyama wetu, gesi n.k.
   
 8. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #8
  Jul 13, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 100
  Trophy Points: 145
  Majibu rahisi ukiwauliwa watu wa Kigamboni.
  • Watu watatumwa Marekani kuangalia miji ya huko.
  • Pesa ya kujazia itatoka Marekani.
   
 9. M

  Mpigaji JF-Expert Member

  #9
  Jul 13, 2012
  Joined: Feb 6, 2011
  Messages: 386
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Unataka ukuu wa wilaya CDM wakishinda??
   
 10. N

  Njoka Ereguu JF-Expert Member

  #10
  Jul 13, 2012
  Joined: Apr 7, 2012
  Messages: 823
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 35
  Hii imekuwa ni desturi kwa watazania kutaka kupinga na kuhoji kila kitu, na kwa mazingira hayo hakuna litakaloamuliwa hata liwe na maslahi kiasi gani bila kuwa na upinzani. Kila kitu watu watahoji hata kama hawajui wanahoji nini. Tumezoea tuachie huru ili kujenge slums basi na tuendelea na migogoro midogo midogo na kulipana vifine hayo ndiyo maisha tunayoyataka.


  Ndiyo maana unaona hii kigamboni inaleta shida kwa kuwa kuna watu wanataka na wanaamini wakiunganisha wananchi kupinga mradi huo kwa maswali madogo kama "wananchi watafaidika nini?" nadhani hapo ndipo tunapokosea na kuchelewesha maendeleo, ndiyo kuhoji kitu ni sawa but kwa Tanzania this is too much na tumeona mara nyingi tu imechelewesha shughuli za maenedeleo kwa kisingizio cha kuhoji especial pale kikundi cha watu fulani kinapoona hakina maslahi ya moja kwa moja kwao.
   
 11. MNAMBOWA

  MNAMBOWA JF-Expert Member

  #11
  Jul 13, 2012
  Joined: Oct 17, 2011
  Messages: 1,969
  Likes Received: 55
  Trophy Points: 145
  tatizo kwani nn? kwani madiwani wa kigamboni cyo wa tz? na sh bil 60 hazitoshi kuanzia ? hata wakitenga bil nyingi kiasi gani mradihuo cyo kwamba utaisha leo. acheni siasa jamani roma haikujengwa kwa cku moja
   
 12. grndossy

  grndossy JF-Expert Member

  #12
  Jul 13, 2012
  Joined: Apr 20, 2011
  Messages: 311
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Nakubaliana sana na wewe ndugu yangu. Watu wengine masikio yao ni ya utafiti wa mapungufu tu hayataki kusikia yale ya maendeleo. Yaani kati ya yale yote Waziri Tibaijuka aliyosema hakuna walichoona zaidi ya kuchokonoa ubaya tu? Mnyonge mnyongeni haki yake mpeni. Ndio sababu tunaambiwa watanzania maneno mingi na hii ni dalili ya kukosa kazi za kufanya vichwa haviko busy.
   
 13. B

  Bobuk JF-Expert Member

  #13
  Jul 13, 2012
  Joined: Oct 8, 2010
  Messages: 5,877
  Likes Received: 458
  Trophy Points: 180
  Kigamboni project is another WHITE ELEPHAT PROJECT aka CAPITAL CITY DEVELOPMENT AUTHORITY (CDA) Mark my words!
   
 14. SMU

  SMU JF-Expert Member

  #14
  Jul 13, 2012
  Joined: Feb 14, 2008
  Messages: 7,629
  Likes Received: 1,659
  Trophy Points: 280
  Kwa nini kigamboni? Nchi hii ina maeneo makubwa tu amabayo hayajajengwa, hayalimwi na wala sio hifadhi. Kwa nini wasiendeleze mji mkuu wetu wa Dodoma kwanza?

  Inakera sana kuona watu wenye elimu ya kiwango cha Mama Tibaijuika wanashiriki kufanya maamuzi dhaifu kama hii ndoto ya kigamboni! Hili 'liinchi' bwana sijui nani "katuroga"!
   
 15. owawajr

  owawajr Member

  #15
  Jul 13, 2012
  Joined: Jul 30, 2009
  Messages: 46
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Kwa sehemu kubwa huyu mama anawajibika ila anaangushwa na mfumo wetu
   
 16. Mzalendo JR

  Mzalendo JR JF-Expert Member

  #16
  Jul 13, 2012
  Joined: Jun 6, 2012
  Messages: 1,179
  Likes Received: 184
  Trophy Points: 160
  Yawewzekana ni mfumo ndio unamuangusha, ila kuinadi Kigamboni imeniuma na sijui ni mfumo tena au?
   
 17. grndossy

  grndossy JF-Expert Member

  #17
  Jul 13, 2012
  Joined: Apr 20, 2011
  Messages: 311
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Mimi nafikiri kabla mtu hajachangia kitu awe na hakika juu ya ufahamu wa lile analochangia. Haihitaji elimu kubwa sana kuelewa kwamba ili uweze kufanikiwa katika jambo lolote ni lazima wale unaowahudumia wakuelewe na wawe na uelewa usio na mashaka juu ya lile unalokusudia kulifanya ili waweze kukupa support.

  Mradi wa Kigamboni ni mradi mpya katika nchi yetu. Hatuna mji mwingine ulishawahi kujengwa hapa ambao tungeweza kujifunzia hapo. Hatua ya Waziri kutaka baadhi ya wanachi kuwa na ziara hiyo ni mafunzo kwa vitendo. Wataenda kujifunza kutoka kwa wenzetu ambao tayari walishafanya hiyo project ili wajue faida na hasara zake. Mimi nampongeza sana Mh. Waziri kwa kushirikisha wananchi. Hebu fikiria, ameshirikisha wananchi makelele, angesema anaenda yeye peke yake na wataalamu au kamati fulani mngesemaje? Hao wawakilishi wa wananchi watakaokwenda ndio watakaokuja kuwapa wenzao mwanga wa kile kitakachoendelea maana sidhani kama wananchi hao watawauza wenzao kwani kwa siku hizi hakuna mtu ambaye yuko tayari kudanganywa. Wakisema uongo kutokana na sababu yoyote wenzao wa Kigamboni wtatambua na hawatakubaliana nao.

  Tuache utamaduni huu wa hovyo wa kufikiri kupinga kila kitu ndio unaonekana wa maana; no, sometimes unaonekana kituko na tunajinyima maendeleo wenyewe kwa ujinga wa kila wakati kuwa na mtizamo hasi. Tusiwe jogoo aliyewekewa almasi na punje ya muhindi akadonoa punje ya muhindi. Let us change our mindset and think positive.
   
 18. omujubi

  omujubi JF-Expert Member

  #18
  Jul 13, 2012
  Joined: Dec 6, 2011
  Messages: 4,144
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 145
  haka kamsemo kwenye red naona kila anayesimama bungeni anapenda kukatumia ...na sasa kameingia jf!

   
 19. JamboJema

  JamboJema JF-Expert Member

  #19
  Jul 13, 2012
  Joined: Jun 14, 2011
  Messages: 1,148
  Likes Received: 30
  Trophy Points: 145
  Njia za kisasa ndo kama alizotumia Jairo?
   
 20. Daudi Mchambuzi

  Daudi Mchambuzi JF-Expert Member

  #20
  Jul 13, 2012
  Joined: Nov 25, 2010
  Messages: 28,636
  Likes Received: 28,452
  Trophy Points: 280
  Kwanini kigamboni??
  Kwanini mradi unafanyika mahala ambapo tayari kuna makazi ya kudumu ambayo itahitajika gharama kubwa ya kufidia wakazi??
  kwanini wasichague msitu wowote na kujenga mji huo ili kuepuka gharama kubwa za fidia pamoja na usumbufu kwa wakazi wa kigamboni??
   
Loading...