Namkataa beberu na mambo yake yote, na fahari zake zote

MANIAJE

JF-Expert Member
Aug 18, 2019
244
461
Mimi Mtanzania, nikiwa na na akili timamu, naahidi;

1. Kujitoa kwenye media za mabeberu (facebook, insta, twita na whatsapp).

2. Kuacha kutumia intaneti

3. Kuvunjavunja televisheni yangu

4. Kuchoma nguo zangu zote na viatu ambavyo havijazalishwa hapa nchini.

5. Kupinga mtaala unaofundishwa kwa lugha ya kibeberu.

6. Kutokutumia dawa yoyote iliyotengenezwa na beberu kwa matibabu.

7. Kuvunjavunja chombo chochote cha usafiri kilichotengenezwa na beberu, na sitatumia usafiri wowote uliotengenezwa na mabeberu hata uwe unakwenda kwa kasi. Nitatumia guu yangu (basi namba 11).

8. Kutokukanyaga katika barabara yoyote iliyofadhiliwa na beberu.

9. Kupinga matumizi ya mashine, au chochote ambacho kimeundwa au kubuniwa na beberu.

10. Kutumia kuni na mafiga kupika, na kuenzi Vyungu vyetu. Vikevile tutalia kwenye majani ya mgomba.

11. Kutofuata tamaduni za kibeberu, kuanzia dini zao, nyimbo zao, na mengineyo.

12. Mwisho kabisa, haka kasimu ka kibeberu ntakatumbukiza kwenye maji.

Mniandikie barua...eh, hivi kalamu ni za mabeberu... Na makaratasi na stempu

Ngoja kwanza... Hivi hili jina langu ni la kibeberu? Basi mnisamehe, nafuta kauli. Nawapenda mabeberu sitarudia tena

Kama unamkataa beberu hebu nikuone
 
Umesamehewa, kuviacha vitu vya wavumbuzi ni sawa na kutokuwa na uhai.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom