Nami nikawaona Wapanda Farasi Wanne....

Rev. Kishoka

JF-Expert Member
Mar 7, 2006
4,526
1,529
Naomba niwape mistari ya Biblia kusoma kama kianzio cha mada yangu.

Mwenye uwezo naomba usome Ufunuo wa Yohana mlango wa 6.Aidha naambatanisha hii linki kutoka Wikipedia kusaidia..

http://en.wikipedia.org/wiki/Four_Horsemen_of_the_Apocalypse

Nitanukuu Sura ya 6 mstari wa 9-10

6:9 And when he had opened the fifth seal, I saw under the altar the souls of them that were slain for the word of God, and for the testimony which they held: 6:10 And they cried with a loud voice, saying, How long, O Lord, holy and true, dost thou not judge and avenge our blood on them that dwell on the earth?

Farasi wangu wanne wanawakilisha Njaa, Magonjwa, Dhuluma na Vita.

Ukimsoma Johnson Mbwambo katika makala yake ya Raia mwema wiki iliyopita, ni dhahiri huko tunakokwenda kwa miezi 24 hata 48 hali itakuwa ni ngumu sana kwa Watanzania kimaisha. http://www.raiamwema.co.tz/08/04/16/mbwambo.php

Beno Ndulu katuambia safari ya neema itachukua miaka 40. Uchumi wa dunia unayumba, suala nas wali ni je Watanzania tunajiandaa vipi?

Njaa; Mvua hizi za masika zimekuwa nyingi kupita kiasi na kuangamiza mazao. Je tuna akiba za kutosha za chakula kutukimu kwa miaka japo miwili?

Magonjwa; Sambamba na mvua hizi, ni mlipuko wa magunjwa, Malaria, Kipindupindu huku bado tuna pigana na ukimwi. Je kama hatuna chakula cha kutosha na bora miili yetu itajijenga vipi na kuwa na kinga asili (immune) kupambana na maradhi?

Dhuluma; Kuibuka na kushamiri kwa Ufisadi na Uhujumu kunaashiria kukomaa kwa dhuluma na unyonyaji. Je kulegalega kwa Serikali kuchukua hatua kali na za haraka kuzuia mfumuko huu was dhuluma kutaendelea mpaka lini?

Vita; Vita vya matabaka, vita vya itikadi, vita hivi mshindi atakuwa nani? Ikiwa njaa maradhi na dhuluma vinaendelea na kutugawa kimatabaka na kiitikadi, mwishowe si vita? je tutaepushaje hili?

Wakati Yohana anazungumzia kilio cha wana wa Mungu kama mlango sa 6 mstari wa 10 unavyosema "Wakalia kwa sauti kuu, wakisema , Ee Mola, Mtakatifu, Mwenye kweli, hata lini kutokuhukumu, wala kuipatia haki damu yetu kwa hao wakaao juu ya nchi?" Je kilio cha Mtanzania kitasikilizwa lini na hata hukumu ya kumpa haki na tumaini la kujivunia uraia na mali asili yake ?

Ni lini Mtanzania atapewa vazi Jeupe la tumaini kuwa karaha na kero za Umasikini, Ujinga na Maradhi zi karibu kuondoka?

Tujiandaeni jamani, hali si nzuri. Si suala la uhujumu na ufisadi tuu, bali ukimsoma Mbwambo, jiulize Serikali yako inafanya nini kujiandaa na kuliandaa Taifa kuelekea huko tusikokujua?

Je great depression ikigonga dunia mwaka huu ama ujao Taifa letu litanusurika vipi ikiwa bei za vyakula na mazao ni mbaya, mafuta yanapanda bei ya wazimu na uchumi wa dunia nzima unayumba?

Tanzania tunafanya nini kujiandaa na kuondokana na balaa la hao farasi wanne waangamizi?

Au tutakiri maneno ya Nyani Ngabu "ndivyo tulivyo"?
 
...Je great depression ikigonga dunia mwaka huu ama ujao Taifa letu litanusurika vipi ikiwa bei za vyakula na mazao ni mbaya, mafuta yanapanda bei ya wazimu na uchumi wa dunia nzima unayumba?

Tanzania tunafanya nini kujiandaa na kuondokana na balaa la hao farasi wanne waangamizi?

Au tutakiri maneno ya Nyani Ngabu "ndivyo tulivyo"?

Tanzania huwa hatusikii homa za recession, depression, sijui kupanda na kushuka kwa wasio na kazi, kuyumba kwa soko la nyumba, bei za pipa kupanda, tofauti ya biashara ya nje na ndani, sijui credit crunch, deni la nchi, kujiamini kwa wateja!!!

Yani utafikiri sisi ndio matajiri. Tunaishi bora liende tu!
 
Mchungaji, umeongea kitu ambacho mimi privately nimelizungumzia sana. Nadhani sasa hivi tuko preoccupied na mafisadi na nani kaiba kiasi gani, hatujaona alama za nyakati. Kuna matatizo makubwa sana duniani kote na when the going gets tough, Tanzania tutajikuta hatuna pa kukimbilia kwa sababu kila nchi hata Marekani wako busy struggling. China tusiwategemee kabisaaa! They are the new colonizers. So what are we left with? Ourselves! Mi nadhani ndiyo maana ni muhimu sana kuanza kuelekeza national dialogue toward 'farasi nne'unaowataja ikiwa ni pamoja na bei ya mafuta kupanda na bei ya chakula kupanda.
Kinachoniuma sana ni kwamba bei ya chakula kupanda should have been good news for us kama tungekuwa serious na kilimo! Lakini tusitegemee mengi kutoka serikali hii, maana mungwana yuko busy kusafiri na kujipendekeza kwa viongozi wa nchi za nje!
 
Kuhani na Susuviri,

Nimesikia maneno ya JK wakati wa ziara ya Wa-Norway, anatamba kuwa tunapata mapato kutokana na madini na kuwataka Norway wasikimbize ubawa kutokana na Ufisadi.

Najiuliza, katika safari zake zote alizofanya, sijasikia hata mara moja akisisitiza misaada ya kuimarisha Kilimo na Ufugaji. Kila siku maneno yake ni Madini, Uwekezaji wa Viwanda vya kutengeneza bidhaa, Nishati na Utalii.

Ikiwa tunaambiwa Madini ni 15% ya pato la Taifa, je tutagawanya vipi ili tukidhi mahitaji muhimu ya maisha kama Chakula na Madawa?

Where are our priorities? Au wao wako tayari wamejitosheleza na "vijisenti"?

There is a need to be aggressive to rejuvenate Agriculture. fishery and livestock sectors in Tanzania.

Tanzania is capable of feeding itself without depending on any imports. In fact if I were the government I would have raised import duty and taxes on all food imports unless the country is facing famine and we need to import food.

Hii vita ya matabaka inakuja kwa nguvu kubwa. Kilichotkea Buzwagi jana si cha kupuuziwa. Wananchi wanaona wazi kuwa walipewa fidia batili kutokana na Serikali kuwa na Watendaji kama Chenge. People fail to see that if there are accusation on corruption and the likes of Chenge could be dismisal with "vijisenti" comments, how do they expect wananchi to react?

Yes the four horsemen are coming, they are charging fast and we may not see 2010 peacefully!
 
The man is Kada wa Chama na yeye anachojua ni kilichopo sasa mezani mambo kulima ungoje mvua si zake .
 
Reverend.. tulipoacha kulijenga Taifa ndipo tulipoanza kulibomoa. Mafarasi wanne, wanakuja tena na hasira, watawala wetu wao hofu yao haiko kwa farasi na wale wapanda farasi wenyewe.

Sijui hadi mtu awapige konzi ndio wataamka katika usingizi wao huo wa pono..
 
Mwanakijiji,

Walisema wahenga, kupanga ni kuchagua!

I will step out of the topic to inject something indirectly kuhusiana na priorities na planning za nchi yetu.

When you look at ufisadi na uhujumu, there is direct relation to what is happening now and how it seems that we are about to drawn and suffocate.

We entered a 20 year contract with IPTL, they were unable to provide sufficient standby and supplement power we had to invite Richmond.

We sold 50% of TRC, we are purchasing new planes, but our railway systemt and roads are in terrible shape to sustain such bad weather conditions due to heavy rains.

We are unable to create a system that will preserve rain waters and drive our Electrical dams hence reducing cost of using oil to produce electricity for consumption.

We are unable to build strong and stable roadways and railway system that will be efficient to move people and goods with minimum and efficient consumption of oil.

As a result of this, we are going to spend more money to buy oil and food and our leaders will tour the world and beg for grants and bail out.

Tanzania inaweza jitosheleza sana kama tungekaa chini na kuangalia ni yapi ya muhimu kufanyiwa kazi kwa nguvu na fedha kiduchu tulizonazo.

Tunapuuzia uwezo wetu wa kilimo, uvuvi na mifugo. It is insane to imagine kuwa nchi imezungukwa na maziwa matatu na bahari haina uwezo wa kuzalisha samaki wa kutosha?

Ni aibu kusikia nchi kubwa kama hii, kuwa wastani wa ng'ombe kule Kilimanjaro na Arusha kutoa maziwa ni lita tatu kwa siku huku Kenya wanapata mpaka lita 70.

Ni wazimu kusikikia kuwa Tanzania ina shida ya chakula! Ardhi yote na rutuba yote zinapotelea wapi?

Njaa itatuletea maradhi. Umasikini utatuletea vita na dhuluma. Sijui ni lini hawa waliopewa madaraka wataamka na kuanza kufanya kazi zao kwa makini!
 
Reverend.. tulipoacha kulijenga Taifa ndipo tulipoanza kulibomoa. Mafarasi wanne, wanakuja tena na hasira, watawala wetu wao hofu yao haiko kwa farasi na wale wapanda farasi wenyewe.

Sijui hadi mtu awapige konzi ndio wataamka katika usingizi wao huo wa pono..

Nafkiri kunaupofu wa kutisha wakutoona kuwa taifa halijengwi na linabomolewa. nafikiri Hili ni Tatizo kubwa na la kutisha...lisiloweza hatakuelezewa hapa.

Kwenye familia ni haki na ni busara kila mwanafamilia akajaliwa na kupata "keki" sawa na wanfamilia mwingine. Hili ni jambo la kawaida kwa msimamizi wa familia yeyote mwenyi fikra timamu.

Kwenye Taifa hali ingetegemewa kuwa The same. Kwanza taifa lijitegemee na pili kila mmoja ndani ya taifa hili awe na fursa sawa ya kumili uchumi na hivyo kuwakwepa farasi wannne.

Nimemfuatia Rais Kikwete na wenzake ..hawalioni hili kabisa. Sioni nia yao ya dhati ya Kumkomboa kila mwananchi!

Hawana mtizamo wa kuwasaidia watanzania walala hoi kuweza kujikomboa na kuwa kwenye haliya heshima ya kibinadamu.

Mtu mkweli na ambaye Utu wake haujaadhirika..anajua fika kuwa hakuna njia ya kweli kabisa na ya uhakika kuwasaidia watanzania waliowengi kama sio kupitia njia ya KILIMO kwani that is the ony common FACTOR kwa kila mtanzania. Repeat: Kilimo na ufugaji ndiko ilipo siri ya kumjenga na kumkoboa mtanzania.. Hivi vingine ni nyongeza tu!

Ninaona ni kuwehuka kukwepa kuona hilo na kulisimamia kiutekelezaji!
 
Kilimo hakiwezi kupata mwekezaji ambaye yuko tayari kutoa 10% kwa kuwa return yake ni ndogo na inachukua muda mrefu kuwa realized, lakini ukiongelea madini return yake kubwa na inaonekana muda mfupi tu baada ya mradi kuanza, ndo maana hata wawekezaji wanakaribishwa zaidi kwenye madini na wamesahau kuwa kilimo ni muhimu maana itafika wakati tuna import hata mchicha.
Maendeleo ya mtanzania hayataonekana mpaka kilimo kiendelezwe kwa kuwa watanzania wengi wako vijijini na wamejiajiri kwenye kilimo, ili kuleta maendeleo ya kweli lazima serikali iwe na nia ya kweli ya kuendeleza kilimo.
 
Jamco,

Are you sure kuwa kilimo siyo guaranteed product?

Tanzania ina uwezo wa kujilisha na kuilisha Afrika Mashariki na Kati nzima single handedly, isn't that lucrative enough?

Hii biashara ya kukimbilia probability na possibility ya kuwepo mafuta na madini ya kutosha imtoka wapi na kwa nini ndio tunaiona ya maana?

Isn't it because we are always looking for short term solutions and short term realization of "super profit" instead of building a strong and steady industry that will guarantee us income and safety?

If gold runs empty or the price falls hence decline on revenues, what are our alternatives?
 
mrema alikwisha lia nji hii nji hii watu walimwona mwehu,ukweli ni kwamba roho inauma kuona nchi inavyolostishwa na mafisadi
 
halafu sasa mafisadi wenyewe yaani wanakuwa na kiburi ile mbaya yani, na hii mi nahisi wanajuwa kuwa wanayokinga inayowalinda na ndo maana hata waengine wanadiriki kusema "vijisenti"...
 
halafu sasa mafisadi wenyewe yaani wanakuwa na kiburi ile mbaya yani, na hii mi nahisi wanajuwa kuwa wanayokinga inayowalinda na ndo maana hata waengine wanadiriki kusema "vijisenti"...

Huyu farasi mmoja "Ufisadi " naona kasi yake ni kubwa sana kiasi kuwa nchi inakalibia kufilisika.
 
jamco usinichekeshe ndugu yangu, nchi sio kama inakaribia kufilisika, ni kuwa nchi imeshafilisika na ndo maana inashika nafasi ya saba kutoka chini kwa umasikini...
 
mi nakukumbusha tu mchungaji ni kuwa hao farasi wameshawafikia watanzania....
Tulichokiona ni kivuli cha wapanda farasi. Wakifika kikamilifu na kutukamata koo, damu itamwagika! kutakuwa na kilio na kusaga meno na ole kibao zitatolewa!

Muulizeni Mnajimu Mkuu Sheikh Yahya aona nini kwenye karai lake?
 
Roho inaniuma rev, your right kivuli kimeanza kuonekana, how can we knock some sense in our leader's head, hivi Rais if your reading this, umeshindwa kutambua umuhimu wa nafasi uliyonayo kihistoria, au unadharau uzito wa maamuzi unayofanya na affect zake kwa taifa hili na vizazi vijavyo, are you that cruel? au ni kweli kuwa power corrupts, kwahiyo inakuwia vigumu kutambua huku chini hali ikoje? yaani i need to reconcile within myself kuwa you simply dont give a damn, kwani dhamira yako yakuwa RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA imeshatimia, jina lako limeshaingia kwenye orodha ya waliopata kuwa marais katika nchi hii, na kila kitu kitaenda with flow, maybe that what matters to you, BUT REMEMBER YOU WILL GO DOWN ON HISTORY AS THE MOST IRRESPONSIBLE PRESIDENT EVER! and it will haunt you and your generations to come, am no threatening you but this is the reality! Do something about those four horses.
 
Mamaparoko,

Wote tunasubiri kupewa lile vazi jeupe! Tumeshaanza kilio ilhali ni vivuli vya wapanda farasi vinatutisha. Sasa Wapanda farasi wakifika si ndio itakuwa balaa kabisa?

Je inakuwaje sisi kama wananchi tunaweza kuona vivuli vya wapanda farasi na viongozi wetu hawavioni? Je wao ni Tomaso kama Mama Simba alivyosema kuwa kuandikwa kwa mambo magazetini si kigezo kwa Serikali kuchukua hatua?

For how long will they continue to be blind or pretend that every little thing is allright?

Tuwape Karoti, Samaki na miwani ya namna gani ili waweze kuona tunachokiona?
 
Balozi wa Uholanzi kasema inabidi tu invest katika kutumia akili zaidi badala ya kutumia non-renewable resources akaonekana anacheza.

Farasi wanne wanakuja, Mwanakijiji kapendekeza kupunguza/ kuondoa kodi ya mazao ya vyakula ili kusaidia hili la njaa.Njaa hii itakuwa tofauti kwa sababu inaweza isisababishwe na ukosefu wa vyakula bali kupanda kwa bei, serikali yetu sijaisikia hata siku moja ikiongelea hili.Inaonekana kama miaka 30 ya chakula nafuu katika world trade inaisha, tuna long term gani? Reserves zetu zikoje? Barabara/ miundombinu yetu ikoje? Fiscal policy zetu zikoje? Mikakati ya muda mrefu ikoje? Mikakati ya umwagiliaji ikoje? Vyama vya ushirika vimewezeshwaje? Mfumo wa soko huria unawezeshwaje? Uboreshwaji masoko ukoje? Viwanda vya kusindika vikoje?

Tuna mipango gani ya kujiondoa katika subsistence pasantry na kuingia katika 21st century agriculture? Kilimo cha sayansi kinachukuliwaje? GM products tunazikubalije?

Not to sound overly socialist, lakini, tunatumiaje bargaining power yetu kama nchi na hizi regional club zetu kama SADC katika ku regulate imbalances katika world trade? Kuondoa speculations in financial markets zinazotumia ugumu wa hali kujitunishia mifuko kwa ku speculate zaidi katika hedge funds zao? Kuwa adabisha wakubwa wa Ulaya na Marekani kutotumia chakula (biofuels)kuendeshea magari na mitambo yao? Kuyabana makampuni ya kemikali za kilimo yanayomonopolize kilimo na kupanga bei za kila kitu, kuanzia mbegu mpaka mazao?

Oil imeshafikia Hubbert peak, tunafanya nini kuhakikisha tunatumia hili kwa faida yetu?

Sijawahi kusikia viongozi wetu wanaongelea haya mambo wala waandishi wetu kuwauliza.
 
Pundit my critical brother,

I guess we are doomed.

My thinking is this; it is either the multiple of us who have same perspective on critical things with our different dimension and analysis on the issue are completely wrong or the one who is the descision maker who appears to have different take on everything is right!
 
Back
Top Bottom