Rev. Kishoka
JF-Expert Member
- Mar 7, 2006
- 4,525
- 1,523
Naomba niwape mistari ya Biblia kusoma kama kianzio cha mada yangu.
Mwenye uwezo naomba usome Ufunuo wa Yohana mlango wa 6.Aidha naambatanisha hii linki kutoka Wikipedia kusaidia..
http://en.wikipedia.org/wiki/Four_Horsemen_of_the_Apocalypse
Nitanukuu Sura ya 6 mstari wa 9-10
Farasi wangu wanne wanawakilisha Njaa, Magonjwa, Dhuluma na Vita.
Ukimsoma Johnson Mbwambo katika makala yake ya Raia mwema wiki iliyopita, ni dhahiri huko tunakokwenda kwa miezi 24 hata 48 hali itakuwa ni ngumu sana kwa Watanzania kimaisha. http://www.raiamwema.co.tz/08/04/16/mbwambo.php
Beno Ndulu katuambia safari ya neema itachukua miaka 40. Uchumi wa dunia unayumba, suala nas wali ni je Watanzania tunajiandaa vipi?
Njaa; Mvua hizi za masika zimekuwa nyingi kupita kiasi na kuangamiza mazao. Je tuna akiba za kutosha za chakula kutukimu kwa miaka japo miwili?
Magonjwa; Sambamba na mvua hizi, ni mlipuko wa magunjwa, Malaria, Kipindupindu huku bado tuna pigana na ukimwi. Je kama hatuna chakula cha kutosha na bora miili yetu itajijenga vipi na kuwa na kinga asili (immune) kupambana na maradhi?
Dhuluma; Kuibuka na kushamiri kwa Ufisadi na Uhujumu kunaashiria kukomaa kwa dhuluma na unyonyaji. Je kulegalega kwa Serikali kuchukua hatua kali na za haraka kuzuia mfumuko huu was dhuluma kutaendelea mpaka lini?
Vita; Vita vya matabaka, vita vya itikadi, vita hivi mshindi atakuwa nani? Ikiwa njaa maradhi na dhuluma vinaendelea na kutugawa kimatabaka na kiitikadi, mwishowe si vita? je tutaepushaje hili?
Wakati Yohana anazungumzia kilio cha wana wa Mungu kama mlango sa 6 mstari wa 10 unavyosema "Wakalia kwa sauti kuu, wakisema , Ee Mola, Mtakatifu, Mwenye kweli, hata lini kutokuhukumu, wala kuipatia haki damu yetu kwa hao wakaao juu ya nchi?" Je kilio cha Mtanzania kitasikilizwa lini na hata hukumu ya kumpa haki na tumaini la kujivunia uraia na mali asili yake ?
Ni lini Mtanzania atapewa vazi Jeupe la tumaini kuwa karaha na kero za Umasikini, Ujinga na Maradhi zi karibu kuondoka?
Tujiandaeni jamani, hali si nzuri. Si suala la uhujumu na ufisadi tuu, bali ukimsoma Mbwambo, jiulize Serikali yako inafanya nini kujiandaa na kuliandaa Taifa kuelekea huko tusikokujua?
Je great depression ikigonga dunia mwaka huu ama ujao Taifa letu litanusurika vipi ikiwa bei za vyakula na mazao ni mbaya, mafuta yanapanda bei ya wazimu na uchumi wa dunia nzima unayumba?
Tanzania tunafanya nini kujiandaa na kuondokana na balaa la hao farasi wanne waangamizi?
Au tutakiri maneno ya Nyani Ngabu "ndivyo tulivyo"?

6:9 And when he had opened the fifth seal, I saw under the altar the souls of them that were slain for the word of God, and for the testimony which they held: 6:10 And they cried with a loud voice, saying, How long, O Lord, holy and true, dost thou not judge and avenge our blood on them that dwell on the earth?