Namhurumia Rais wangu Kikwete hasa pale anapopotoshwa kwa makusudi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Namhurumia Rais wangu Kikwete hasa pale anapopotoshwa kwa makusudi

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by MziziMkavu, Jun 4, 2010.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Jun 4, 2010
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,615
  Trophy Points: 280
  jakayakikwete.jpg


  Rais Jakaya Mrisho Kikwete
  Ndugu zangu, leo tena imefika, siku ambayo tunakutana kupitia safu hii, kwa hakika tumshukuru Mungu ambaye ni mwema aliyetuwezesha mimi na wewe kuwa wazima na afya tele, hatuna cha kumpa isipokuwa kuusifu utukufu wake.
  Kichwa cha habari nilichokiandika leo kinajieleza kuwa kuna watu ambao kwa upande wangu nawaona wanampotosha Rais wetu mpendwa, Jakaya Mrisho Kikwete kwa makusudi kabisa, sijajua nia yao ni nini.Binafsi siipendi tabia hii.

  Ipo mifano ya wazi kabisa ambayo hata yeye aliwahi kuigutukia na akacharuka mbele ya waandishi wa habari na wageni wengine waalikwa.
  Kwa mfano, kuna wakati alitaka kutoa zawadi ya gari la wagonjwa kwa Halmashauri ya Arumeru, lakini badala yake walioitwa kuja kuchukua zawadi hiyo hawakuwa walengwa (watu wa Loliondo). Rais Kikwete alishituka na kwa hakika alichukia na kwa mara ya kwanza akafoka hadharani!
  Lakini si hilo tu, juzijuzi ulipitishwa mswada wa sheria ya Udhibiti wa Gharama za Uchaguzi na Rais Kikwete akasaini kwa mbwembwe kwenye viwanja vya Ikulu jijini Dar es Salaam, lakini akaibuka Mbunge wa Karatu Mheshimiwa Wilbroad Slaa akasema una makosa.

  Tulishuhudia baadhi ya viongozi wa serikali wakibisha na kumbeza, lakini kwa vyovyote Rais Kikwete kama binadamu alichukia kuona wasaidizi wake wakimpotosha, inawezekana sina uhakika aliamuru urudishwe bungeni tena baada ya kugundua ukweli.
  Ndugu zangu katika kikao cha 19 ambacho kiliahirishwa Ijumaa iliyopita tulishuhudia sheria hiyo ikirudishwa bungeni na wanasiasa wengi wakatafsiri kuwa ni ushindi wa bure kwa Dk. Slaa dhidi ya serikali kwa sababu vipengele vilivyofanyiwa marekebisho katika muswada huo ni vile ambavyo awali viliainishwa na mbunge huyo wa Karatu aliyedai kuwa viliingizwa kinyemela.

  Moja ya kifungu alichokilalamikia ni kifungu cha timu ya mgombea kuhakikiwa na msajili wa vyama, Dk. Slaa alipinga kifungu hicho kwa madai kuwa kinakwenda kinyume na misingi ya demokrasia kwani timu nyingi za wagombea zingeenguliwa kutokana na matakwa ya msajili au ofisa mtendaji mkuu wa kata.
  Binafsi ndugu zangu naipongeza serikali kwa uungwana iliyoonesha katika sakata hilo ambalo kwa hakika ni baya kwa sababu yapo madai kuwa kuna watu au mtu alichomeka vipengele ambavyo havikuidhinishwa na bunge, kisha kumpelekea Rais kusaini, kitu ambacho kwangu naona licha ya kuwa ni aibu ni hatari.

  Naamini Dk. Slaa alifanya hivyo kwa kuwa hakutaka hapo baadaye Rais apate aibu kwa sababu angetaka aipate angeacha na huko mbele angeweza kujitokea mtu akapinga sheria hiyo akidai imechomekwa maneno ambayo Bunge letu tukufu halikuridhia na akawa na ushahidi wa Hansard ya bunge ambayo huandika kila linalotamkwa bungeni na kweli ingedhihirika kuwa kilichoandikwa katika sheria na kusainiwa na Rais ni uongo mtupu!
  Mimi huwa najiuliza, kwanini watu wanafanya madudu haya? Mbaya zaidi ni kwamba yanapelekwa kwa rais wa nchi na anapotokea mtu kusema anabezwa bila kujua kuwa mwenzao aliyetoa hoja alisoma vizuri kilichoafikiwa na kusainiwa na bunge.

  Ndugu zangu nawashauri wale wote wanaomzunguka rais wawe makini katika mambo makubwa kama haya ambayo yanahusisha sheria za nchi kwani wakifanya hivyo wataondoa aibu na fedheha ambayo inaweza kumpata Rais wetu.
  Nasema hivi ndugu zangu kwa kuwa ni aibu tena kubwa kuona sheria inasainiwa na rais tena mbele ya wageni mbalimbali lakini hata kabla ya kuanza kutumika inapelekwa tena bungeni kufanyiwa marekebisho, tujiulize wenzetu wa nje wanaoona madudu haya watakuwa wanatuelewaje?
  Mimi naamini kufanya kitendo kama hiki cha kubadili vifungu na kisha kumpelekea Rais kusaini ni kumdanganya kiongozi wa nchi na kumtia aibu katika jamii ya ndani na nje na watu hao nadhani wamekuwa wazoefu kwa udanganyifu kwa rais, sasa tufanye nini jambo kama hilo lisijirudie?

  Mtakumbuka kuna wakati barabara ya Segera – Chalinze ilikatika kwa mvua na Rais alikwenda eneo la tukio, lakini Waziri aliyekuwa akihusika hakuwepo huko na alipoulizwa alisema wazi kuwa wasaidizi wa rais hawakumtaarifu! Tulipigwa na butwaa!
  Ndugu zangu, udhaifu huu kila Mtanzania anapaswa kuukemea kwa kuwa unachafua sifa nzuri ya Rais wetu na serikali yake ya awamu ya nne. Mimi sina la kufanya isipokuwa kumhurimia rais wetu, lakini huu ni ushauri wangu.
  Jipu limepasuka, siwezi kuwa adui kwa kusema ukweli.

  Namhurumia Rais wangu Kikwete hasa pale anapopotoshwa kwa makusudi - Global Publishers
   
 2. d

  damn JF-Expert Member

  #2
  Jun 4, 2010
  Joined: Feb 22, 2010
  Messages: 585
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  wasaidizi wake wajua kuwa he doesn't fit for presidential shoes. Angekuwa nafit, angeshawachukulia hatua na upuuzi wote ungesha koma.
   
 3. B

  Bulesi JF-Expert Member

  #3
  Jun 4, 2010
  Joined: May 14, 2008
  Messages: 6,447
  Likes Received: 414
  Trophy Points: 180
  Inaelekea hawa wasaidizi wa Rais wanajua weakness yake kuwa jamaa ni mvivu wa kusoma kwa hiyo kila anachopelekewa anatia saini tu bila kuhakiki!! Hii ndio sababu kubwa ninayoiona inayowafanya wasaidizi wake wawe wanamchomekea vitu visivyostahili.
   
 4. T

  Tz Asilia Member

  #4
  Jun 5, 2010
  Joined: Oct 30, 2009
  Messages: 45
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Awe makini sana, pia anachoambia achanganye na zake mwenyewe.
   
Loading...