Namhurumia Rais Kikwete,anaumiza kichwa,yupo njia panda!

Nikukumbushe

JF-Expert Member
Jun 4, 2013
2,602
408
Hili liko wazi. Halikitaji elimu hata ya ngazi ya cheti kulijua hili.
Namhurumia sana JK,ana wakati mgumu sana. Anashindwa nani awe rais wa JMT kupitia chama chake. Hii ni hatari sana kwa rais wa nchi kuwa njia panda. Rais anakosa hata washauri. Mawaziri wake wametangaza kuutaka urais. Nani atamshauri. Washauri wake hasa makini wanautaka urais.
Miongoni mwao ni Steven Wassira,Mizengo Pinda,Magufuli,Samwel Sitta,Benard Membe,Mwandosya.
Wengine ni manaibu waziri,akiwemo January makamba,Mwigulu Nchemba. Nani atamshauri rais huyu?.
Pia,wapo waliojiuzulu kwa kashfa akiwemo Shamsi Vuai Nahodha,EL,Emmanuel Nchimbi.
Mwaka huu CCM kazi ipo. CCM haiwezi kuvuka salama,haiwezekani kubalance haya yote. Mitihani nii ni misumali ya moto kwa CCM
1.Makundi ya urais. Ni moto unaosubiri kuwaka. Ni suala la muda. Hapa nashauri kitu kimoja,ni bora ccm wachukue maamuzi magumu sasa sio wavute muda mpaka uchaguzi ukaribie. Muda huu wanaweza kukabiliana na changamoto zitakazojitokeza japo wamechelewa. Hii ni bomu. Ni zaidi ya lile la Yiroshima Nagasaki. Hapa ni suala la muda. Watakuja kukimbiana.
2.Migomo iliyotokea. Huu ni moto mwingine,migomo hii imeathiri wananchi moja kwa moja ukiwemo mgomo wa madereva na madaktari.
3.Ahadi ambazo hazitekelezeki. Mwaka 2010 walitoa ahadi chungu nzima. Ahadi hizi ni mwiba kwa CCM.
4. Utayari wa wananchi kupokea mabadiliko. Wananchi wamepokea mabadiliko kwa kiasi kikubwa. Hili limechangiwa na elimu ya uraia. Zile propaganda za nani katoka wapi,anasali wapi sasa they are no longer active.
5.UKAWA. Huu umoja ni hatari kwa CCM. Kwani hawajawahi hata kufikiria juu ya hili. Zile mbinu za wagawe ili uwatawale now ni historia.
6.Mahakama maalumu. Hapa CCM sio kuwa na mtihani tu,bali wanajuta. Kwa nini,kuna Trade off. Hapa CCM haiwezi kufavour upande mmoja na ikabaki salama. Ikumbukwe kuwa ilani ya CCM inazungumzia uanzishwaji wa mahakama ya hiyo. Wakiianzisha mahakama hiyo watakuwa wameanzisha Vita ya wao na upande fulani. Wasipoianzishe bado ni hatari zaidi.
Ni hayo tu.
 
Umeandika nini mkuu utakuwa umevurugwa siyo bure jihurumie wewe na familia yako kwakuwa hujitambui.
 
Mbona anao washauri wengiiii tena waliobobea sana wenye uwezo mkubwa kifanye kazi yake kuwa rahisi kufanikisha mrithi wake kwa tiketi ya chama chao..manake maamuzi ya ya mteule wa tiketi ya UKAWA wanayo wao wenywewe Ukawa.
Level ya Urais yuko
Mzee Mwinyi na Mzee Mkapa

Level ya Waziri Mkuu
Salim Ahmed Salim, Judge Sinde Warioba, Cleopa David Msuya na jembe lao Mzee Malechela

Level ya Ukuu wa Majeshi
Mzee Waitara na David Mwamunyange.

Wazee wenye heshima
Joseph Butiku, Pro Shivji, Kisumo, Sir Kahama, Sir Chande, Paul Rupia

Wazee wa Jadi Mikoani...

Kama machifu na wazee wenye heshima na busara kwenye ngazi ya Mkoa wasio na sura za vyama.

Na wengineo wengi ata wale ambao aliwapiga chini hakuwashirikisha kwenye kuwaomba ushauri zama hizo si mbaya kuwapigia magoti na kuwaambia Taifa linaitaji kuwasikiliza.Na CCM haitaji kufavour kundi CCM inaitaji Mwanaccm asie na kundi Kwishney....ugumu unao usema wewe kwa mtu mwenye kundi ni lazima atauona...ila Historia uwa ni Mama ya Ukweli.Hakuna Rais aliepata kuacha mtu wake kushika kiti cha URAIS Tanzania..zaidi ukiwashirikisha wakubwa wa Nchi inamsaidia Kiongozi husika kuwa na justification ya Wahusika kuwa yuko sawa katika KUILINDA Nchi na kuwa kumbe UNAUMAKINI katika kuona TAIFA linabaki mikononi mwa mtu salama na sio regardless ya matamanio na matarajio yako [Interest].
 
Ni chaguo la Mungu kumuweka madarakani Jk ili Tanzania ipone. Na Tanzania kupona ni kuchanganyikiwa kwa viongozi wa ccm na m/kiti wao na chama kutawanyika, hiyo ndiyo dawa pekee ya kupona gonjwa tulilonalo. ccm ni zaidi ya ebola, bahati mbaya gonjwa hili halifahamiki na WHO.
 
Kwa hakika mleta mada umesomeka. ume-hit point. kwa yeyote ambae hakukuelewa, basi atakuwa haelewi hata akieleweshwa. Yatosha tu kusema, ambae bado hajafahamu ulichoandika, asubiri muda umueleweshe.
 
Mkuu wanakuelewa sana ila ndio ule muendelezo wa kujaribu kufunika harufu isisikike kitu ambacho ni vigumu, CCM ipo njia panda kweli tena njia pand halafu kuna kilima.
 
Wewe mtoa post unayamsha ya nini haya majitu ambayo bado yanavuta shuka wakati kumekwisha kucha!!! Twende zetu tu,kama yatatukuta mbele ya safari poa tu!
 
Back
Top Bottom