Namhurumia Kikwete!

kavulata

JF-Expert Member
Aug 2, 2012
12,298
12,600
Imefikia mahala hata sherehe za ufunguzi wa shule ya chekechea haunogi bila ya kumualika Rais wa nchi. Kila mtu mwenye tafrija, uzinduzi, msiba au aina yoyote ya tukio anafikiria kuinogesha kwa kuhudhuliwa na rais wa nchi. Maana yake ni kwamba hadi kufikia sasa hakuna kiongozi yeyote kuanzia mawaziri, makatibu wakuu, wakuu wa mikoa wala wilaya wenye heshima na wanaoaminika ndani ya jamii isipokuwa Rais tu ndiye aliyebaki na afadhali.

Hili ni jambo baya sana kwa taifa na chanzo chake ni kutokana na mawaziri, makatibu, wakurugenzi, wakuu wa mikoa na wilaya kushindwa kutatua shida za wananchi kwa kutumia ubunifu wao, badala yake wengi wao huwa wanasubiri wapewe maagizo ya utekelezaji kutoka Ikulu. Kikwete amejaribu kufanya kila jambo kurekebisha jambo hili ikiwemo kuwabadilisha na kuhamisha watendaji wake angalau kutafuta ahueni, lakini wapi busness as usual. Katika jitihada zake za kuimarisha uajibikaji aliambulia Magufuli, Mwakyembe, Lowassa na Chiligati wakati wa enzi zake akiwa mkuu wa wilaya ya Temeke. Waliobakia wote ni majanga tu, wanashindwa kutatua hata suala la madawati hadi wasubiri Ikulu iwape chenchi ya rada huku wakiwa wamezunguukwa na misitu minene kwenye maeneo yao.

Hata wale wasomi kabisa kuliko Kikwete huwa hawamsaidii katika kutatua kero za wananchi na kusababisha isionekane tofauti kati ya kiongozi msomi na asiye msomi katika uongozi. Mh. Majimarefu hana elimu kubwa lakini anafanya vizuri kwenye jimbo lako kuliko wabunge ambao wana PhD.
 
Back
Top Bottom