Namfananisha Shaka Hamdu Shaka na Alexander the Great

budget

Member
Feb 23, 2015
42
27
Namna katibu wa NEC itikadi na uenezi Ndugu Shaka Hamdu Shaka kijana wa Mwambao wa Bahari ya Hindi pale Zanzibar anavyofanya uongozi wake imenirudisha mwezi July mwaka 356k.k. katika Mwambao wa Caspian wenye urefu wa km 2,815 nchini Persia (Iran ya leo) alipozaliwa mtoto Alexander.

Kama jinsi Shaka Hamdu Shaka alivyopata mafunzo kutoka kwenye Chama na viongozi wakongwe wa Taifa hili na kupitia Tanuru la kuoka viongozi la UVCCM akapikwa akaiva, Naam ndivyo ilivyokuwa kwa Mwamba Alexander the Great ambae katika mwaka wake wa 13 alipata mafunzo kutoka kwa Mwanafilosofia Mkongwe Duniani kwa jina la Aristoto, akapikwa akaiva.

Akiwa na Miaka 20 Alexander the Great alionyesha umahiri wake katika kuiongoza Persia (Iran) ambapo sifa zake zilivuka mipaka kufika Ugiriki na Uturuki na baada ya miaka kadhaa akawa mfalme wa nchi zote kutoka Uarabuni mpaka India.

Alexander the Great kutokana na siasa zake za kufanya vitu vinavyoonekana aliweza kuanzisha zaidi ya miji 70 mikubwa Duniani ikiwa ni pamoja na kuanzisha idea za biashara, kujenga barabara na kuwapa elimu ya sayasi wananchi pamoja na kujenga maktaba kubwa ili kuongeza maarifa.

Ndani ya miaka michache, Alexander the Great alikuwa mfalme wa Mecedonia, Ugiriki, Misri, Uturuki, Israeli, Lebanoni, Iran na Afghanistan. Alexander alifariki akiwa na miaka 32 pekee, yaani ndani ya miaka 12 ya uongozi wake aliacha alama ambayo haitafutika vizazi na vizazi.

Pamoja na kufanana sifa nyingi na Shaka Hamdu Shaka, sifa kuu wanayofanana ni katika miaka yake yote Alexander hakuwahi kushindwa vita. Hakuwahi kuwa defeated. Yaani alishinda vita zote.

Kwa wanaomfahamu Shaka Hamdu Shaka, hakuwahi kushindwa na Vita, kote alipofika Shaka nchi ilitii, tumeona tangu akiwa Ikulu Zanzibar, UVCCM Taifa, CCM Morogoro alipigana vita nyingi na aliibuka mshindi, hata kule Mikumi aliwaheshimisha wana CCM.

Naweza kusema kwamba Alexander the Great amezaliwa tena Tanzania. Shaka anaamini katika kufanya mambo mema zaidi kwa watu kuliko jinsi watu wanayomfanyia yeye, hiyo ndio tafsiri yake ya mafanikio sawasawa na imani ya mwanamageuzi Henry Ford Muanzilishi wa Magari ya Ford, na sasa Ford Ranger WildTrack.

Shaka haamini katika kusubiri fursa, anaamini katika kutengeneza fursa. Hayupo kwa ajili ya kufanya siasa bali kutengeneza siasa salama kwa nchi yetu.

Ni vijana wachache sana nchini wamefikia hatua hiyo. Shaka ameaminika na kuwa kijana mdogo zaidi kupewa kitengo kinachobeba uhai wa Chama na anakitendea haki.

Hakika kwa hazina ya vijana kama wakina Shaka ni dhahiri kuwa CCM itaendelea kushika hatamu. CCM imewekeza kwa akina Aristoto na Wakina Alexander wa Tanzania, kwa taarifa nilizo nazo ni kwamba wengi sana bado wamefichwa, siku wakipewa nafasi tutaona viwango vipya vya siasa nchini Tanzania na hilo haliko mbali.

IMG-20210614-WA0075.jpg
IMG-20210614-WA0072.jpg
 
Viongozi wa sasa hv wa CCM wanapitia Tu mbeleko za Maghufuli, Jiwe alijitoa kafara Kwa ajili ya CCM, kanunua wapinzani, kawaondoa bungeni wapinzani , kafanya kila aina ya hiana kuifanya CCM ibaki yenyewe, viongozi waliopo hawa wasingeweza lolote kukabili purkshani kama zile Kati ya 2010-2017.

Huyo dogo uliyempa hipe Hana lolote.
 
Shaka anatia mashaka. Saivi naona anatembelea vieite kiyoyozi safi kabisa
 
Labda hujajua kwamba pamoja na hayo yote, Alexander alikuwa analiwa, sasa umepatia sana kumfananisha huyu jamaa yako maana nae ndio walewale.
 
Namna katibu wa NEC itikadi na uenezi Ndugu Shaka Hamdu Shaka kijana wa Mwambao wa Bahari ya Hindi pale Zanzibar anavyofanya uongozi wake imenirudisha mwezi July mwaka 356k.k. katika Mwambao wa Caspian wenye urefu wa km 2,815 nchini Persia (Iran ya leo) alipozaliwa mtoto Alexander.

Kama jinsi Shaka Hamdu Shaka alivyopata mafunzo kutoka kwenye Chama na viongozi wakongwe wa Taifa hili na kupitia Tanuru la kuoka viongozi la UVCCM akapikwa akaiva, Naam ndivyo ilivyokuwa kwa Mwamba Alexander the Great ambae katika mwaka wake wa 13 alipata mafunzo kutoka kwa Mwanafilosofia Mkongwe Duniani kwa jina la Aristoto, akapikwa akaiva.

Akiwa na Miaka 20 Alexander the Great alionyesha umahiri wake katika kuiongoza Persia (Iran) ambapo sifa zake zilivuka mipaka kufika Ugiriki na Uturuki na baada ya miaka kadhaa akawa mfalme wa nchi zote kutoka Uarabuni mpaka India.

Alexander the Great kutokana na siasa zake za kufanya vitu vinavyoonekana aliweza kuanzisha zaidi ya miji 70 mikubwa Duniani ikiwa ni pamoja na kuanzisha idea za biashara, kujenga barabara na kuwapa elimu ya sayasi wananchi pamoja na kujenga maktaba kubwa ili kuongeza maarifa.

Ndani ya miaka michache, Alexander the Great alikuwa mfalme wa Mecedonia, Ugiriki, Misri, Uturuki, Israeli, Lebanoni, Iran na Afghanistan. Alexander alifariki akiwa na miaka 32 pekee, yaani ndani ya miaka 12 ya uongozi wake aliacha alama ambayo haitafutika vizazi na vizazi.

Pamoja na kufanana sifa nyingi na Shaka Hamdu Shaka, sifa kuu wanayofanana ni katika miaka yake yote Alexander hakuwahi kushindwa vita. Hakuwahi kuwa defeated. Yaani alishinda vita zote.

Kwa wanaomfahamu Shaka Hamdu Shaka, hakuwahi kushindwa na Vita, kote alipofika Shaka nchi ilitii, tumeona tangu akiwa Ikulu Zanzibar, UVCCM Taifa, CCM Morogoro alipigana vita nyingi na aliibuka mshindi, hata kule Mikumi aliwaheshimisha wana CCM.

Naweza kusema kwamba Alexander the Great amezaliwa tena Tanzania. Shaka anaamini katika kufanya mambo mema zaidi kwa watu kuliko jinsi watu wanayomfanyia yeye, hiyo ndio tafsiri yake ya mafanikio sawasawa na imani ya mwanamageuzi Henry Ford Muanzilishi wa Magari ya Ford, na sasa Ford Ranger WildTrack.

Shaka haamini katika kusubiri fursa, anaamini katika kutengeneza fursa. Hayupo kwa ajili ya kufanya siasa bali kutengeneza siasa salama kwa nchi yetu.

Ni vijana wachache sana nchini wamefikia hatua hiyo. Shaka ameaminika na kuwa kijana mdogo zaidi kupewa kitengo kinachobeba uhai wa Chama na anakitendea haki.

Hakika kwa hazina ya vijana kama wakina Shaka ni dhahiri kuwa CCM itaendelea kushika hatamu. CCM imewekeza kwa akina Aristoto na Wakina Alexander wa Tanzania, kwa taarifa nilizo nazo ni kwamba wengi sana bado wamefichwa, siku wakipewa nafasi tutaona viwango vipya vya siasa nchini Tanzania na hilo haliko mbali.

Huyo Alexander unayemsema wewe naye aliwahi kuolewa na mwanaume mwenzake?

Sent from my Nokia 5.1 Plus using JamiiForums mobile app
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom