Namchukia sana mume wangu kwa sababu ya wivu wake..

LAMU

Member
Jun 12, 2016
51
18
Habari zenu wana jf naombeni ushauri kwenu. Nifanyeje? Maana nimejikuta simpendi tena mume wangu kwani amezid wivu .

Nimekuwa ni mtu wa kushinda nyumbani tu hataki nijishughulishe wala kutoka kwenda kwenye sherehe na misiba hataki, pia hataki hata niongee na mtu yeyote yule hata jirani. Sasa naona kero na nimepata naye mtoto mmoja

Natamani niachike ili niepukane na kero hiii naombeni ushauri wenu
Aksanteni...
 
Kabla ya kufikiria kuachana naye..je ulishawahi kumweleza kua hupendi hiyo tabia yake ya wivu na inakukwaza? Je ameanza hivi karibuni kuwa na wivu zamani hakuwa nao? Angalia asije akawa anajihami kwako kwa kukubana ili afanye ujinga wake huko nje..
 
Huwa natamani sana kuchungwa ila asifikie huko jamani, hata msibani huendi sasa unaishije na jamii yako ndugu!!!
Ongea nae kuna maisha zaidi ya hapo mlipo, akianguka leo kesho mwanenu ataishi vipi, kaa nae mweleze kwa upendo atakuelewa la sivyo yeye ndo mchepukaji maarufu
 
Habar zenu wana jf.. Naombeni ushaur kwenu. Nifanyeje? Maana nimejikuta simpendi tena mume wangu kwani amezid wivu .. Nimekuwa ni mtu wa kushinda nyumbani tu hataki nijishughulishe wala kutoka kwenda kwenye sherehe na misiba hataki, pia hataki hata niongee na mtu yeyote yule hata jirani... Sasa naona kero.. Na nimepata naye mtoto mmoja.. .. Natamani niachike ili niepukane na kero hiii... Naombeni ushauri wenu... N
Aksanteni...
Shauri yako waoaji hawapo miaka hii
 
Zungumza naye maisha ya sasa unaishi pekee yako kuna leona kesho hata mambo kama misiba anakuzuia je likiwafika nyie nani atawafariji......ikiwezekana tafuta mtu anayemuheshi aweze kumshauri
 
Huyo bwana inaonekana anakupenda sana, pia inawezekana kuna habari mbaya kukuhusu wewe anazozipata unapokuwa umetoka. Kaa nae chini mujadiliane swala hilo ili mliweke sawa. Unaposema kuwa humpendi kwa sababu ya "wivu" wake sikwelewi hata kidogo. Inaonekana hukuwa unampenda tangu awali ama kuna anaekudanganya kukuharibia ndoa yako! Shauri yako, angalia urembo wako usikuponze. Wapo/walikuwepo warembo zaidi yako ila sasa wanajuta!!!
 
Wape habari wazazi wake juu ya hayo mambo muyajadili naamini mtaweza fikia muafaka bt kuamua kuachika sio sahihi maana ndoa ni stara, uvumilivu na mambo mengine hilo la wivu ni jambo dogo sana
 
Back
Top Bottom