Namchukia mzee wangu!

Yani mzee mzima wa miaka 33 umeshindwa kumjengea nyumba Baba ako.

Unakuja kutupigia kelele za ku fight (Eti bado una fight?)

Unatuaibisha
 
Nilitegemea kuona labda mzee ni mnyanyasaji, mtesaji lakini maskini baba watu hajaweka sakafu tu.

Kweli kuzaa unaweza zaa kizaazaa..watoto hatuna shukrani
Yaanj kamdharau mzee kisa sakafu .

Hizi mzee wake angeaamua kumtupa chooni enzi hizi angesemaje
 
Utakuwa una matatizo ya akili, mzee wako labda angejenga nyinyi msingepata fursa ya kusoma, labda pia alitumia pesa nyingi kuwapa elimu akijua kuwa nanyi mkifanikiwa mtakuja kulipa fadhila kwa kumjengea nyumba mzee wenu, nazani kwa umri wako tayari wewe ni mtu mzima je mipango yako yote huwa una mshirikisha mke wako? Na je huyo mama yako pamoja na nyie mlikuwa mnashirikisha mzee wenu mipango yenu? Nakushauri nenda kamwombe baba yako msamaha kabla laana haijakukuta, baba yako alipambana mpaka leo umeota ndevu adi mkun%& leo unamwona fala.
 
mwanangu e, we bado mvulana! ukikua utayajua mengi! so tuseme point kubwa ni kitendo cha mzee kutokusakafia nyumba, na unaaibika unavyowaleta madem zako!! je kuna tofauti gani wewe na mtu aliemkana mama yake kisa mama yake kimwonekano hayupo sawa!
.
.
acha mambo ya kipuuzi naukatubu kwa Mungu wako, tafuta hela wewe ndo uje uonyeshe nyumba inapaswa kuweje, unaanza kumkosoa mwanaume aliekuleta duniani? wewe mpka sasahivi umefanya nini??
.
.
yaani kijana mzima unamchukia bana yako kisa hajasakafia nyumba? Je kama yeye anapenda nyumba ikiwa hivyo yes wapo ambao wanapenda udongo ule ukipigwa maji ukafagiliwa vizuri,
.
.
acha kujilinganisha na watu, umetokea katika familia yenye uwezo wa kawaida, pambana uje kuwa na maisha mazuri! af mtoto wa kiume unawapelekaje madem nyumbani?
.
.
serious kabisa unampeleka dem kwenu eti mnatembeleana, nachojua wanaume ndo tunapelekana makwetu, tunakula pamoja nk. mwanaume mwenzio hawezi zungumzia hali ya kwenu hata kama kupoje, hao madem tafta namna muwe mnakutana out, kwa miadi!!
.
.
inshot nakuona unajiaminisha sana hapo ni kwako pia, HAPO SI KWAKO, NA UMRI WA KUKAA HAPO UMEISHA TOKA KAJENGE NYUMBA YAKO YENYE SAKAFU, usimchoshe mzee!!
.
.
na uwe unaenda kumwona, na hio nyumba ukaiweke sakafu otherwise unatafuta laana ya kufa kifo kibaya sana!! BABA HAKOSEI,
 
Mtoto asiye na shukrani ni mzigo kwa wazazi wake. Weka wewe sakafu na ubadili muonekano wa nyumbani kwenu,si unao uwezo sasa?. Unangoja nn?
 
Labda hawezi kufanya kila kitu..na ameamua kufanya vile anavyoona vinampa furaha. Mfano kama hivyo kawasomesha na kuwapa mahitaji yenu yote.

Si mumrekebishie hapo home, au hataki?
Kusomesha ni kazi sana halafu unakuta watoto wanne au watatu wamefuatana,mshahara wote unakuwa ada na matumizi ya nyumbani pamoja na kukopa juu.

Halafu wanamaliza shule mzee astaafu au aachishwe kazi na watoto bado watoto wapo nyumbani hata matumizi na kula wanamtegemea .

Then anakuja mtu anasema kwanini hujajenga nyumba ya maana jibu ni kwamba ondoka kama huwezi kukaa,mzazi kahangaika yeye anawaza atamletaje dem nyumba ya vumbi?
 
Nimezaliwa katika familia ya kawaida tu iliyokidhi mahitaji ya msing mwaka 1988. Baba yangu alikuwa mwalimu ila baadaye akaacha bila kutoa sababu za msingi. Sababu yake kubwa ninapomuuliza ni "walikuwa wakinionea wivu na walikuwa wananiroga hasa mkuu wangu wa kazi". Huwa nachukia nikisikia majibu haya na huondoka upesi kwani naweza hata kumpiga(japo naomba isije kutokea). Mama yangu ni wale mama wa nyumbani, alikutana na huyu mzee kwenye biashara, alikuwa akiuza viazi vitamu. Ni darasa la saba.

Tangu utoto tumeishi maisha naweza kusema hatukutakiwa kuishi maisha hayo, ukizingatia mzee alikuwa mfanyakazi na from nowhere akaacha kazi. Najiulizaga mno je, hakufikiria kuwa atakuwa na familia? Je alitoka mwanafunzi na hivyo akakimbia hasira za wanajamii?

Hatukuwahi kulala njaa, tulikuwa tunakula na niseme ukweli toka najitambua mzee alikuwa akitupenda mno kwa kidogo alichonacho, alijitahidi mno wanawe tusipate shida kwa kutupa kila tulichotaka ndani ya uwezo wake. Alikuwa akitutoa out n.k, katika hili naweza kusema familia yetu ni zile familia za kawaida ila tuliishi maisha ya kizungu huenda kuzidi hata baadhi ya watoto wa matajiri.

Tatizo likaja kwenye nyumba tuliyoishi, ilikuwa mbovu kulinganisha na maisha tuliyoishi. Mzee sijui alikuwa kachanganyikiwa au la, nyumba ndani haina sakafu ni vumbi tu, na wakati huo bado ilikuwa ya nyasi. Mama alikuwa akimshawishi wakarabati nyumba, alichokuwa anajibu "mtoto anayeona hapa hapamfai basi ahame" (hapo ni tayari ni mtu mzima kidogo najitambua), nilikuwa nachukia na namchukia mno kwa kaulo hizi.

Mbaya zaidi uwezo alikuwa nao kwa wakati huo kwani alikuwa mlinzi wa shirika la serikali fulani, tena wa kudumu wa kuajiriwa na serikali. Nilikuwa naona aibu mno nilipotembelewa na classmates wangu hasa wa kike (nilizidi kumchukia mzee).

Mama alikuwa akisema hutu baba yenu hanishirikishi chochote na hela zake sijui zinaishia wapi, na mzew akiulizwa kuhusu hilo alikuwa mkali mno(kwa hili chuki yangu iliendelea kukua).

Siku moja akaniambia, "mimi nimesgajitoa mhanga na maisha haya, naishi pabovu wakati wafanyakazi wenzangu wana nyumba, nataka nyie wanangu muwe mnaheshimika na mjenge ninyi hizo nyumba bora zenye sakafu kama mnavyodai". Nilimuelewa kwa kauli hii japo kidogo. Nilimuuliza kama haoni aibu akajibu " sioni aibu ni maisha niliyochagua, kama hamtaki muhame". Nilichukia mno kwa marudio ya kauli hizi.

Sasa ni mtu mzima na nimefanikiwa kidogo ila si kama ninavyotaka, naendelea kupambana. Mzee katika masuala ya ada alikuwa hasumbui kabisa, alikuwa analipa ada mpaka inabaki change na naidai shule, kwenye mambo ya elimu kwa kweli hakutaka masihara. Ila shida ni maendeleo home ikiwemo nyumba.

Nina kaka zangu wote alipoteza hela nyingi kuwapigania, acha dada zangu pia( japo walipuyanga na hela zilipotea). Katika hili nampongeza kwa 5%. Pia, mwenye kujali elimu ya dada zangu, kwani kuna mmoja alikuwa anatembea kwa miguu umbali mrefu kumpelekea baadhi ya mahitaji shule.

Pia kaka yangu mkubwa alimpa laki 3 kwa wakati huo ili aongezee kwenye biashara yake(hili hakumshirikisha bi mkubwa, na bi mkubwa alilalamika) japo bro huyu alikula mtaji. Kaka zangu wote walikataa shule kwa vinywa vyao. Waliharakia maisha, na sasa wanahaha!

Huyu mzee hela za kununua mashamba mbona anazo? Za kununua radios, TV's n.k, kwa nini ashindwe kutenga japo laki 1.5 kwa wakati ule aboreshe nyumba? Yaani simuelewagi kabisa huyu dingi, anatupambania kwenye elimu sasa kwanini asi-fight kukarabati nyumba? Kila siku ugomvi na bi mkubwa ilikuwa nk issues hizo hapo.

Pia dada zangu wote walikataa shile kwa vinywa vyao japo mzee wakati huo alitaka kuwaendeleza(nampongeza kwenye hilo). Simuelewi huyu mzee na namchukia niseme wazi, kwa sababu anasababisha aibu kwa familia, nakumbuka nyumba ndani vumbi yeye anataka kuweka king'amuzi, huu niliona upuuzi tu.

Mfano kuna wakati alishindwa kusave hela za maandalizi ya mimi kuingia chuo, muda umefika wenzangu wanakwenda chuo mimi naranda randa tu home kwenye kibanda kibovu chenye vumbi(shame), halafu tunaanza kuhangaika kuomba omba kwa mkuu wa wilaya na mbunge msaada mimi na yeye, tulikuwa tunatembea ofisi zote na kukumbana na dharau tu(shame).

Nikitakiwa kujiunga jkt mujibu, alininunulia vifaa vyote kama ilivyoelekezwa(nampongeza kwa 10% kwani alinunua vyenye bei na ubora mkubwa), ila kwa nini ashindwe kukarabati nyumba? Ambayo inabeba heshima za mtu?

Nimeaibika mno na inatosha, nilishindwa hata kulete demy ghetto kwa upuuzo huu huu, mazingira mabovu yapo hovyo hovyo. Pia, ni kwa nini japo hana hela ya kutosha ila anamsaliti bi mkubwa na wasichana mabinti kuliko bi mkubwa?( japo hufanya kwa kificho sana)Hiyo sio aibu?

Kwa nini amfiche bi mkubwa mshahara wake? Niishie hapa...

Sitaki kuongea mengi naona nitakufuru na mimi sitaki kukufuru, kikubwa ni hayo tu, jamani nishaurini kwani inafika wakati hata kuonana naye sitaki. NB:

Huyu mzee alimaliza form four mwaka 1974!
kinacho kusumbua wewe ni kushindwa kuosha kwa marafiki zako na mademu zako kuwa mna nyumba sio nzuri, hiyo ni sababu ya kijinga sana, maana mzee wako amejitahidi kuwalipia elimu kwa maisha yenu ndo muhimu
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom