Namchukia Jakaya Kikwete

Mundu

JF-Expert Member
Sep 26, 2008
2,707
638
Toka kumalizika kwa zoezi la uchaguzi na kutangazwa matokeo ya Udiwani, Ubunge na Urais, namchukia sana Kikwete. Sipendi na wala sitaki hata kuona picha yake, wala kusikia habari zake mahali popote. Ninakacha kuangalia taarifa za habari kwenye Runinga, sisikilizi habari kwa njia ya Radio; na magazeti ndio sitaki kununua kabisa kwa kuchelea kukutana na habari zake.

Amenifanya niwe na wakati mgumu na hii yote ni kwa sababu ametumia madaraka yake vibaya kwa kushirikana na NEC na hao wengine, kuchakachua kura za watanzania.

Nahisi dunia inaenda mbele nyuma. Sijui wenzangu hali ikoje kwenu?
 
We acha tu, yaani mi ndiyo hata nikisikia sauti yake napata kichefuchefu. Natamani kuhamia Burundi au hata Iraki kulikoni kuishi katika nchi inayoongozwa na wezi; yaanikuanzia Rais hadi tarishi!
 
Lakini wapo wanaompenda!

Kwa lipi alilofanya la haki?
Kumwacha Chenge achukue fomu ya kuwania Uspika?
Maisha yako yamebadilika, au ya jamaa zako kwa kuwepo kwake madarakani kwa miaka mitano iliyopita, hadi akenuliwe meno leo?
 
Toka kumalizika kwa zoezi la uchaguzi na kutangazwa matokeo ya Udiwani, Ubunge na Urais, namchukia sana Kikwete. Sipendi na wala sitaki hata kuona picha yake, wala kusikia habari zake mahali popote. Ninakacha kuangalia taarifa za habari kwenye Runinga, sisikilizi habari kwa njia ya Radio; na magazeti ndio sitaki kununua kabisa kwa kuchelea kukutana na habari zake.

Amenifanya niwe na wakati mgumu na hii yote ni kwa sababu ametumia madaraka yake vibaya kwa kushirikana na NEC na hao wengine, kuchakachua kura za watanzania.
Nahisi dunia inaenda mbele nyuma. Sijui wenzangu hali ikoje kwenu?

Yaan wewe kama mimi baada ya uchaguzi nimetokea kumchukia kikwete
sijui atafanyaje mpaka moyo wangu urudi umpende:doh:
 
Duh!!
mimi nilianza kumchukia tangu alivyoanzaa usanii wake mchana kweupe katika mambo ya msingi kwa taifa letu tunaolipenda.
Hii ya kuchakachua uchaguzi majuzi ndiyo kabisaaa.. amemwaga petrol kwenye moto unaowaka.
I really hate him!!
 
Lakini nilijua, this time angepatikana kwa kuwa nguvu ya umma ingemwondoa. Akaiba!!
 
yametimia waliyoyaahidi hadi kurudisha mafisadi ni sahhhiii kweli mie nampenda kama rais wetu kwa kuwa sina jinsi ila tunaomba amtokomeze Chenge na RA EL basi angalau tutafuta namna ya kujaribu kumpenda
 
Toka kumalizika kwa zoezi la uchaguzi na kutangazwa matokeo ya Udiwani, Ubunge na Urais, namchukia sana Kikwete. Sipendi na wala sitaki hata kuona picha yake, wala kusikia habari zake mahali popote. Ninakacha kuangalia taarifa za habari kwenye Runinga, sisikilizi habari kwa njia ya Radio; na magazeti ndio sitaki kununua kabisa kwa kuchelea kukutana na habari zake.

Amenifanya niwe na wakati mgumu na hii yote ni kwa sababu ametumia madaraka yake vibaya kwa kushirikana na NEC na hao wengine, kuchakachua kura za watanzania.
Nahisi dunia inaenda mbele nyuma. Sijui wenzangu hali ikoje kwenu?

Mundu mimi nahisi wewe humchukii kama mimi tena umechelewa sana kumchukia. Kiwango ninachomchukia mimi ni kikubwa kiasi kwamba hata kutumia neno "namchukia" naona kama haitoshi, nakuwa sijamtendea haki. Infact chuki yangu kwake haijaanza wakati wa uchaguzi huu bali toka nilipogundua kwamba Jakaya Mrisho Kikwete haipendi Tanzania wala watanzania maskini isipokuwa familia yake, marafiki zake including wanamtandao na mafisadi kadhaa. Kama nitaambiwa anaipenda Tanzania na watanzania basi nitaomba nisaidiwe maana mpya ya neno kupenda.Nina mifano lukuki ya kulithibitisha hili kwamba jk haipendi Tanzania wala watanzania maskini.

Ninamchukia sana huyu baba I wish hakuomba ridhaa ya kuliongoza Taifa hili zuri. Ila kuna kipindi huwa ninamsamehe bure kwani ninahisi haoni link (correlation) iliyopo kati ya yeye kucheza na rasilimali za nchi hii na vifo visivyo vya lazima vya watanzania wenzetu especially kina mama na watoto under 5. Otherwise angeiona link iliyopo I'm sure hata kama angekuwa na matatizo ya akili angechukua hatua japo kidogo.

At times hata dunia huwa siielewi kabisa. Kwamba wako tayari kumchukulia hatua Elabashiri wa Sudan kwa kuruhusu mauaji ya Darful lakini hawako tayari kumchukulia hatua mtu kama Kikwete, Mugabe na wengineo ambao wanaruhusu vifo vya kizembe kwa akina mama kwa kukosa huduma wakati wa kujifungua na watoto wasio na hatia maskini kutokana na curable diseases simply sababu viongozi hawa hawana priorities kwani mabilioni katika nchi hizi yanaliwa na wachache huku huduma muhimu kama afya zikikosa pesa za kutosha kuziendesha. Kwa takwimu za Tanzania nadhani ni akina mama zaidi ya 500 katika 100,000 hufa kila mwaka kutokana na ukosefu wa huduma wakati wa kujifungua. Dunia haina shida na akina mama hawa wanaokufa vifo visivyo vya lazima ila tu watu wanaokufa kwa bunduki kama kule Darful ndio tatizo kwao na wako tayari kumchukia hatua rais wa nchi.
 
Aisee poleni sana

Ila mimi nimefurahi kupita kiasi .......................... MAPINDUZII!!!!!!!!!!!!!!!!! DAIMAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAA

teh teh.,....POLENI SANA MTAZOEA
 
Mimi ndo kabisa, NAMCHUKIA KUPITA KIASI! Sitaki kuona wala kusikia Gazeti ama Redio ikitaja jina lake, wakianza tu habari zake nabadili channel.

Natamani ningekuwa SNIPER
!!:laser:
 
Tuliwambia mtashinda hapa JF tu.
picha mtaziona kila ofisi muhimu mtakazoingia.
wote mtakuwa watumwa wake
Pia ndo muajiri mkuu waserikali.
mtajiju na sifa zenu hizo.
Na mtaumia sana tena kwa miaka 5 kama hammupendi.
Kwangu mimi nokicheko japokuwa naichukia ccm siku nyingi zilizopita.
Acha kwanza mkione cha moto.
 
Mi simfagilii hata kidogo na sijawahi kumpa kura tangu ajitokeze kwenye chaguzi za urais. Nilisimliwa na kuona utumbo wa hotuba zake zenye uzito wa unyoya kabla cjafikisha umri wa kupiga kura. Mkwere ni kimjamaa flani kinahusudu mipasho na kucheza miziki kwenye majukwaa.
Na huu msimamo wangu wa kuichukia ccm na maovu yake nitawarithisha wanangu na vizaz vyote, hii ndiyo njia pekee ya kuwaangusha mafisadi ktk taifa letu.
 
Yaani nilidhania ni mimi peke yangu ambaye namchukia huyu mkwere....I HATE YOU KIKWETE
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom