Namba za simu za Ofisi nyingi za Serikali hazipatikani

Mparee2

JF-Expert Member
Sep 2, 2012
2,580
4,262
Sijui ni nani anahusika ku huisha namba za Ofisi za Serikali kama za Mawaziri/Wizara, Wakuu wa mikoa, Wilaya, Hospitali za Mikoa, Hospitali kuu za Wilaya na taasisi nyingi za Serikali kwenye mtandao kwani namba nyingi zilizopo zilishafungiwa au zimebadilika.

Naamini kutokuwa na namba za simu sahihi za Idara/mashirika ya Serikali, huchangia Vijana wengi kuishia kuandika malalamiko kwenye mitandao, badala ya kuwasiliana moja kwa moja na ofisi husika.
 
Kuna haja ya kuzihuisha hizo namba, na ku-update baadhi ya website.
 
Mfano hai wa simu isiyopatikana ni land line ya Tamisemi Dodoma, na inaonyesha namba imekosewa.
 
Hili ni tatizo la kudumu Tanzania.tunaomba ofisi zote za serikali, idara, wizara, Halmashauri, na kadhalika simu za ofisini za TTCL ziwepo, zijulikane na ziwe zinafanyakazi.mabosi wanatembea na ofisi kwa kutumia mobile zao Kama ofisi akihama anahama na simu yake.
 
Hilo usiseme unaweza tuma email leo 02.04.2020 utakuja jibiwa 10.12.2025 hii ndio Tz na watumishi wake wa serikali.
Na kujibu email nalo tatizo kubwa sana kwenye taasisi na idara za serikali mfano NACTE bure kabisa
 
Inakupasa upewe conection na watu kama sisi!

Tofauti na hapo lazima usote.
 
Katika kipinfi hiki ni vema mawasilianonyakawa ya uhakika zaidi.
Sio kipindi hiki kwanikipindi hiki kinatofauti gani na vipindi vingine? Tunachotaka namba ziwe update na lazima ziwe TTCL na sio vinginevyo.Tatizo la kanchi ketu kila jambo ni siasa eti mpaka upitie kwa flani.
Ujinga mtupu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kuna uzembe mkubwa mno halafu nadhani wanaona sifa kutokupokea cm zao. Ni ofisi karibu zote za serikali wana ugonjwa huu. Kuna bosi mmoja ukibahatisha kumpata ofisini kwake ni shida anajidai yupo busy kweli mara kashika hili mara kaacha full maigizo.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tatizo ni kubwa hata ukiingia kwenye website ya wizara husika namba zilizomo ukipiga hazipatikani. Kwa miezi 2 nahangaika kutafuta mawasiliano na mheshimiwa naibu waziri Bashe ili nimueleze e yaliyo tupata wakulima wa korosho Mlandizi Kibaha kwa korosho tulizo uza October 2018 bila mafanikio.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
yani namba zipo ilimradi tu taasisi waonekane wana namba shame
 
Number za simu wamehamia TTCL, wakasahau kufanya update kwenye website zao.

Hili ni kila mtu anakumbana nalo hadi upewe no na wahusika zinazotumika
 
Back
Top Bottom