Pacbig
JF-Expert Member
- Oct 15, 2017
- 1,095
- 2,079
Wadau poleni na pongezi kwa mapambano ya kimaisha ya kila siku.
Nikiwa katika harakati za kutuma maombi ya sensa. Nilipomaliza kujaza detail na kuzituma, taarifa kutoka kwenye mfumo ikasema namba yangu tayari imeshatumika (namba ni ya vodacom). Sikuwaza sana maana nilijua shida ni nini. ( sitalisemea hili ili kupunguza maelezo)
Sasa ikabidi nitumie namba nyingine ya tigo. Lakini hii namba nilikuwa sijaikaliri ikabidi nibonyeze *106# kisha nikaingiza namba yangu ya Nida ili nizione namba zilizosajiliwa kupitia hiyo namba yangu ya Nida.
Mimi nina sim card mbili tu ya Vodacom na Tigo, cha kushangaza nikakuta nina namba mbili za Vodacom zilizosajiliwa kwa kutumia namba yangu ya Nida. Namba ya kwanza ndio ninayoitumia, lakini namba ya pili siifahamu.
Nimewasiliana na Vodacom wameniambia nitembelee duka lao lililo karibu na kesho nitaenda. Ila kuna maswali najiuliza.
1. Inawezekanaje mtu akasajili simcard kwa kutumia utambulisho wa mtu mwingine?
2.unaposajili huwa tunaweka alama za vidole ili kuthibitisha kama ni wewe kweli. Sasa hata kama kuna mtu aliipata namba yangu, Alama zangu za vidole alizitoa wapi?
Karibuni kwa majibu na ushauri.
NB nimeipigia hiyo namba inapatikana na nimeongea nae. Nimejaribu kumuuliza hiyo namba aliisajili wapi, lakini hajatoa majibu ya kueleweka.