Namba ya mkuu wa mkoa

Kiriba

JF-Expert Member
Mar 25, 2013
540
257
Mimi natoa pendekezo kwa mkuu wa mkoa atoe namba yake ya simu, yaani special mobile namba kwa ajili yakushughulikia kero zawana nchi.

Mimi binafsi na kubali utendaji wa huyu jamaa japokuwa nilikuwa simkubali kabisa kutokana na ukaribu wake na akina Rizi.

Huyu jamaa nimekuja kugundua ni mchapa kazi ila alikuwa na kundi chafu.

Huku mtaani kuna mambo mengi hayaendi. Kwa mfano mtaani kwetu kuna jamaa anafuga ng'ombe kwenye makazi ya watu. Wakati wa mvua niharufu ya mbolea majumbani hakukaliki.

Tumesharipoti hili jambo manispaa zaidi ya mara 5 lakini hakuna hatua yeyote inayo chukuliwa.

Sasa naomba mkuu wakoa aweke namba yake hapa tumpe hizi taarifa na apige marufuku ufugaji kwenye makazi ya watu kwani sheria hairuhusu.

Naamini makonda yumo humu JMF. Please, Mkuu wa Mkoa.
 
Back
Top Bottom