ProBook
JF-Expert Member
- Jan 13, 2012
- 558
- 257
Ila mwansngu we mbishi aisee,,, pole lakini
Mkuu apo kwenye O2 sensor umenigusa. Hili kweli ni tatizo watu hudharau sana mimi ni victim wa hii sensor na nilisema sifanyagi tena upuuzi nlioufanya. Gari yangu iliwaka check engine nikaifanyia service, nilijua mambo ya service tu. kitu bado kimewaka, nikachomoa betri kureset baada ta muda ilawaka tena. Nikaifanyia diagnosis naambiwa o2 sensor imebuma. Ah mi nikachukulia powa coz sikuona any difference katika ulaji wa mafuta. Matatizo yakaanza, gari ikaanza kumiss wakati iko idle tu na pale ukitoka kuondoka, nikabadili coil zote na kuweka plug mpya, ngoma haijakubali iko vile vile. Ilikuwa inaniboa mana mi cpendi kuzima gari nkiwa nimesimama nakutia story na mtu. Sinabudi ilabidi nikomae nayo tu ivo ivo. Kumbe huku mashine kidogo kidogo inaanza kupoteza uhai. Nikaanza kusikia sauti kutoka kwenye mashine tapping sound, nikampelekea fundi akanambia kuwa anahisi ni km mlio wa engine knock. Ila alinambia kuwa haina shida coz mlio haukuwa wa kutisha. Jengibe likazaliwa oil pump ikaanza kufail. Ukiwasha gari oil haipandi mpaka ufanye race kdg, na kama nipo idle muda mreeefu oil haipandi hili lakini lilizuka baada ya kutumia synthetic oil, nikachange nakuweka ya kawaida bado, sikuchukulia serious coz niliona inapanda tu nikirace nikawa nazima gari nikiwa na idle kwa mda kuepusja kurace kila wakati. Nilikosa amani kutokana na mlio wa engine knock nkafanya diagnosis nyengine error ikaja ya O2 na knock sensor, nikajua hizi sensor zimefeli, ilikuwa rahisi kuzipata nikachange lkn stil same error. Kawaida panapokuwa na engine knock na kuna knock sensor imedetect hio knock, ecu inatakiwa ifanye correction. Lakini ecu imeshindwa kufanya correction sawasawa coz O2 sensor inata value ambazo hazichange kutokana na hali ilivyo.
Niliendelea kuendesha tu ivo ivo coz niliona hakuna serious ishu. Siku moja nilikutana na mbishi njiani akataka kushindana mi nikakamua gari, kosa langu nkasahau kama nimeganda gia namba tatu, alafu nishafika rev limit, nilijua nishamaliza gia, nilikaa kwenye rev limit kwa sekunde nyingi za kutosha kusababisha matatizo katika engine, jamaa nlimpita, ata nafika destination gari ikakata moto. Kabla kuiwasha nikatizama temperature iko sawa, nikaipiga moto ikawaka lkn ule mlio wa knock sasa ndio umekuwa serious, mana nlikuwa naisikia kabisa piston unavogonga kaaaavu kavu kabisa!!! Sasa nimechange mashine mana haikutengenezeka nimeweka nyengine na sensor ya O2 nyengine! Saiv nakula raha tu.
Ukiona check engine imewaka ni vyema uifanyie diagnosis na usikimbilie service tu na ikikwambia O2 sensor basi usichelewe kutafuta nyengine ukaweka