Zanzibar 2020 Namba 30: Mussa Aboud Jumbe, Mtoto wa Rais wa zamani wa Zanzibar, Aboud Jumbe amechukua fomu ya CCM kuwania Urais wa Zanzibar

Influenza

JF-Expert Member
Jul 1, 2018
1,445
3,403
Mussa Aboud Jumbe, Mtoto wa Rais wa zamani wa Zanzibar, Aboud Jumbe amechukua fomu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) kuwania Urais wa Zanzibar katika Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 2020. Jumbe amekuwa mgombea wa 30 katika mbio hizo za Urais.

Vile vile Mussa ni Mkurugenzi katika Idara ya Maendeleo ya Uvuvi katika Wizara ya Kilimo,Maliasili,Mifugo na Uvuvi

EbcArMeXYAAgZUD.jpg
 
Safi sana Wazanzibari.

Sasa mngechujana wenyewe kwa wenyewe huko na mkapeleka jina la mnayemtaka CHAMWINO. Au mtapeleka majina yote haya halafu system ya CHAMWINO ndiyo itachagua mmoja inayemtaka?
 
wacheni watu wachukue ni haki yao ili mradi katiba na sheria havionyeshi ukomo wa idadi ya wachukua form. Hapo naamini Wazanzibari wanapata uwanja mpana wa kumpata mtu sahihi na mwenye maono pamoja na uwezo wa kuongoza.
 

Mussa Aboud Jumbe ni mmoja wa watoto 14 wa Rais wa pili wa serikali ya Mapinduzi Zanzibar Sheikh Aboud Mwinyi Jumbe. Sheikh Jumbe anakumbukwa kwa kupigania maslahi mapana zaidi ya Zanzibar ktk Jamhuri ya Muungano ya Tanzania.
https://www.upi.com › 1984/01/29
Tanzanian Vice President Aboud Jumbe resigned Sunday from all... - UPI.com

29 Jan 1984 · State-run radio gave no reasons for the resignation of Jumbe, president of the former sultanate of Zanzibar, but the
Rais Amani Amani Abeid Karume anasema moja ya alama kubwa alizozipigania Sheikh Aboud Jumbe rais wa Pili ni Baraza la Wawakilishi linaloamua mambo mengi kwa maslahi ya wazanzibari na historia ya taifa hilo la Zanzibar.
www.theeastafrican.co.ke
Zanzibar mourns the advocate of three-tier system of government

vice president aboud jumbe resigns from www.theeastafrican.co.ke
20 Aug 2016 · The death of former Zanzibar president Aboud Jumbe Mwinyi comes at a time ... Vice-president steps down
Mussa Aboud Jumbe ni mdau mkubwa wa kupigania masuala ya bahari na rasilimali zake. Amehudumu kama Mkurugezi wa Idara ya Samaki wa Serikali ya SMZ katika Wizara ya muhimu ya Maji, Ardhi / Makazi, Nishati, Mazingira na labda atakuwa na maono kama ya baba yake marehemu Sheikh Jumbe.
 
Back
Top Bottom