Zanzibar 2020 Namba 22: Hussein Ibrahim Makungu (Bhaa), achukua Fomu ya kuomba kugombania Urais wa Zanzibar kupitia CCM. Ajitoa kwenye kinyang'anyiro

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,797
11,959
Muwakilishi wa Jimbo la Mtoni, Mh: Hussein Ibrahim Makungu (Bhaa) nae amejitokeza kuchukua Fomu ya kuomba ridhaa ya kugombania Urais kwa Tiketi ya Chama cha Mapinduzi CCM.

Bhaa anafikisha idadi ya Wagombea 22 waliojitokeza kuomba ridhaa ya kugombania Urais wa Zanzibar akiwa yeye ni miongoni mwa Wagombea hao 22.


1592821154997.png

UPDATES
ZANZIBAR: MGOMBEA AJITOA KWENYE MCHAKATO, ASEMA ANAIPUNGUZIA KAZI CCM


Mgombea Hussein Ibrahim Makungu amejitoa katika mchakato wa kuwania kuteuliwa kugombea Urais wa #Zanzibar kwa kupitia CCM

Amedai amefikia uamuzi huo ili kukipunguzia Chama Cha Mapinduzi (CCM) kazi ya kuchuja wanachama waliochukua fomu

Hussein anakuwa mgombea wa kwanza aliyeomba ridhaa ya kuteuliwa na chama hicho kugombea Urais kujitoa katika mchakato huo
 
Mpaka ma-chekibobu sasa wanachukua form!.

Bei gani hizo form naona wanachakingia chama.
 
Naona Wazanzibar wameamua kudai Uhuru wao kupitia huu uchaguzi! Nitashangaa sana kama watakubali kutawaliwa na vibaraka wa Tanganyika!

Bora hata wampe tu shujaa wao wa siku nyingi Maalim Seif Shariff Hamad.
 
Muwakilishi wa Jimbo la Mtoni, Mh: Hussein Ibrahim Makungu (Bhaa) nae amejitokeza kuchukua Fomu ya kuomba ridhaa ya kugombania Urais kwa Tiketi ya Chama cha Mapinduzi CCM.

Bhaa anafikisha idadi ya Wagombea 22 waliojitokeza kuomba ridhaa ya kugombania Urais wa Zanzibar akiwa yeye ni miongoni mwa Wagombea hao 22.
View attachment 1485959
View attachment 1485960
mbona watamuua kwa pressure huyu baba wa watu sasa!!

 
Mwanachama wa CCM, Hussein Ibrahim Makungu amejitoa katika mchuano wa kuomba ridhaa ya kuteuliwa na chama hicho kugombea Urais Zanzibar, kwa kile alichoeleza kuwa anakipunguzia chama chake kazi ya kuchuja wanachama katika kutafuta mgombea.

Chanzo: swahilitimes

Hivi kama Wewe tu ulipokuwa ukichukua Fomu tayari ulishataguliwa na Wenzako 25 hukuweza Kukionea Huruma Chama hapo hapo usiichukue?
 
Hiyo hela ya kuchukulia fomu bora tu hata angeendea kuhongea au kunywea kabisa pombe! Iwapo tu alishindwa kwenda kuitoa sadaka kwa wenye uhitaji, na badala yake akaamua kuwapa hao ndugu zake wa Ccm kirahisi tu.
 
Back
Top Bottom