Namba 10 kwenye Orodha: .... BENJAMIN W. MKAPA... Anaachwa vipi kusimama Jukwaani?

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Mar 10, 2006
33,475
39,991
Mojawapo ya vitu ambavyo labda vitahitaji majibu baadaye ni kwa vipi CDM wakati wa uzinduzi wao hawakumgusa kwa uzito unaotosha aliyekuwa Rais wa Tanzania wakati matukio mazito ya ufisadi yanatokea yaani B. W. Mkapa. Katika thread hii mengi yamejadiliwa kumuhusu Mkapa: MKAPA ABOVE THE LAW? Chama cha Demokrasia na Maendeleo kilitambua kuhusika kwa Mkapa katika maamuzi ya kifisadi kiasi cha kumuweka namba 10 katika ile "Orodha ya Aibu" akiwa miongoni mwa kina Ballali, Rostam, Lowassa n.k. Katika maelezo ya orodha hii ilisemwa hivi:

Orodha ya Mafisadi (List of Shame)
A. USHIRIKI WA MOJA KWA MOJA KATIKA VITENDO VYA UFISADI
10. BENJAMIN WILLIAM MKAPA

mkapa.gif

Benjamin William Mkapa alikuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuanzia mwaka 1995 hadi 2005 alipomaliza kipindi chake cha pili. Ufisadi wote ulioelezewa katika waraka huu ulitokea wakati wa utawala wa Rais Mkapa na anawajibika nao moja kwa moja ama kwa kuubariki au kwa kuunyamazia. Zaidi ya hayo, kuna ushahidi unaoonyesha kwamba wakati akiwa madarakani Rais Mkapa alishiriki moja kwa moja au kwa kutumia ndugu na/au washirika wa karibu wa familia yake katika ufisadi mkubwa na uliolipotezea taifa fedha nyingi. Kwa mfano, wakati akiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano, Mkapa alitumia wadhifa huo kuhakikisha kwamba kampuni iitwayo Tanpower Resources Limited inamilikishwa asilimia 85 ya hisa za kampuni ya Kiwira Coal Mines Ltd. inayochimba mkaa wa mawe huko Kiwira Mkoani Mbeya. Hisa zilizobaki asilimia 15 zinamilikiwa na Serikali. Tanpower Resources Ltd. ni kampuni iliyoanzishwa kwa ajili ya kuinuifaisha familia ya Rais Mkapa na washirika wake wa karibu. Taarifa za BRELA zinazonyesha kwamba wakurugenzi wa Tanpower Resources Ltd. ni Anna Mkapa, mkewe Rais Mkapa, Nicholas Mkapa, mtoto wa Rais, Bwana Joseph Mbuna, wakili wa kujitegemea na baba mkwe wa Nicholas Mkapa, Daniel Yona, Waziri wa Nishati na Madini wakati wa utawala wa Rais na bwana Joesph Mapundi. Baada ya Tanpower Resources Ltd. kutwaa umiliki wa Kiwira Coal Mines Ltd. kwa nguvu za Ikulu ya Rais Mkapa, iliingia mkataba na Shirika la Ugavi wa Umeme nchini TANESCO wa kujenga mtambo wa kuzalisha umeme kwa kutumia mkaa wa mawe na kuiuzia umeme TANESCO. Mkataba huo utainufaisha kampuni ya Kiwira Coal Mines Ltd., na kwa hiyo Rais Mkapa, familia na washirika wake wa karibu kwa kiasi cha dola za Marekani milioni 271 kwa wakati wote wa mkataba.

Hiyo ni sehemu kidogo tu kwani baadaye tumeweza kuona mengi sana yaliyotokea wakati wake kama Rais na hasa wakati wa mwaka wake wa mwisho. Ikumbukwe ndiye aliyewakingia kina Ballali, Rostam na wengine. Ninajiuliza maswali yafuatayo:

a. CDM inamhofia au kumheshimu Mkapa kiasi kwamba yawezekana hakiamini kabisa kuwa anahusiana na ufisadi mkubwa kabisa uliowahi kutolewa nahivyo wananchi hawapaswi kukumbushwa?

b. CDM inaamini kuwa Mkapa hagusiki kwa vile Rais Kikwete alisema "muacheni mzee wetu astaafu" wakati hataki kustaafu anapenda kujihusisha na siasa? Kama anajiingiza kwenye siasa kwanini yeye mwenyewe naye aliyoyafanya yasiwe issue kwa Watanzania?

c. CDM inafikiria kwa mfano atakaposimama leo kuzungumza huko Arumeru Mkapa atawaonesha huruma wapinzani na viongozi wao? Hivi akizungumza na kuwabeza wapinzani na kuwaita majina ya ajabu ajabu na kuwafanya duni viongozi wao atakuwa amewaonea au anafanya kile kinachotegemewa kama mwanasiasa wa CCM? Kama yeye hatowaheshimu - tayari kwa kukubali kushiriki kampeni hizi ameonakana hajali sana mambo ya upinzani - kwanini wao wanafikiria kumheshimu katika hili?

Nini cha kufanya basi?

a. CDM ioneshe kuwa CCM inamtumia mmoja wa viongozi waliosimika mfumo wa utawala wa kifisadi nchini mtu ambaye ana damu ya Watanzania mikononi mwake.

b. CDM ioneshe kuwa matatizo mengi ya madini nanishati yamejengwa kutokana na sera na sheria ambazo zilipitishwa na Mkapa.

c. CDM ioneshe vile vile jinsi kiongozi huyo huyo alivyoendelea kawaida ya kubeba na kubebana na kutolea mifano watumbalimbali. Ikumbukwe pamoja na yote yanayosifiwa kuhusu Mkapa bado leohii tunavuna mavuno ya uongozi wake.

d. CDM ioneshe kuwa mojawapo ya mambo ya ubaguzi wa rangi nchini kufanywa na wanasiasa yalifanywa wakati wautawala wake kuhusiana na Salim na jinsi gani yeye Mkapa kama kiongozi aliyelelewa na Nyerere alishindwa kuwazuia wale waliokuwa nakiu ya madaraka hadi kutupatia viongozi wa sasa. Kwa kifupi ioneshe kuwa viongozi wanaopigiwa debe na Mkapa ni utangulizi wa ufisadi!

e. CDM ioneshe kuwa CCM ilikuwa na nafasi nzuri ya kuonesha imeamua kweli kujivua gamba lakini yale yaliyotokea leo hii huko Arumeru na hasa kuhusishwa kwa BWM kunaonesha tu kuwa gamba limegoma na sasa limeganda na gamba likiganda linakuwa donda! Wapo baadhi ya watu wazuri sana ambao CCM ingewez akuwatumia lakini kwenda kumtumia mfalme wa magamba ni kosa kubwa la kimkakati!

CDM isiposhambulia pasipo huruma CCM na sera zake, isipoonesha kuwa matatizo yanayowakabili watu wa Arumeru (na sehemu nyingine nchini) yanatokana na kushindwa kwa sera za CCM (siyo kutekelezwa tu bali kushindwa in substance) basi itajikuta inaletwa karibu na kilele nakuachwa hewani! CDM ni lazima ichore mstari, iwagawe wananchi na kuwachochea wananchi kugawanyika kifikra. Pasipo kugawa fikra, hawatagawa kura!
 
Mojawapo ya vitu ambavyo labda vitahitaji majibu baadaye ni kwa vipi CDM wakati wa uzinduzi wao hawakumgusa kwa uzito unaotosha aliyekuwa Rais wa Tanzania wakati matukio mazito ya ufisadi yanatokea yaani B. W. Mkapa. Katika thread hii mengi yamejadiliwa kumuhusu Mkapa: MKAPA ABOVE THE LAW? Chama cha Demokrasia na Maendeleo kilitambua kuhusika kwa Mkapa katika maamuzi ya kifisadi kiasi cha kumuweka namba 10 katika ile "Orodha ya Aibu" akiwa miongoni mwa kina Ballali, Rostam, Lowassa n.k. Katika maelezo ya orodha hii ilisemwa hivi:

Hiyo ni sehemu kidogo tu kwani baadaye tumeweza kuona mengi sana yaliyotokea wakati wake kama Rais na hasa wakati wa mwaka wake wa mwisho. Ikumbukwe ndiye aliyewakingia kina Ballali, Rostam na wengine. Ninajiuliza maswali yafuatayo:

a. CDM inamhofia au kumheshimu Mkapa kiasi kwamba yawezekana hakiamini kabisa kuwa anahusiana na ufisadi mkubwa kabisa uliowahi kutolewa nahivyo wananchi hawapaswi kukumbushwa?

b. CDM inaamini kuwa Mkapa hagusiki kwa vile Rais Kikwete alisema "muacheni mzee wetu astaafu" wakati hataki kustaafu anapenda kujihusisha na siasa? Kama anajiingiza kwenye siasa kwanini yeye mwenyewe naye aliyoyafanya yasiwe issue kwa Watanzania?

c. CDM inafikiria kwa mfano atakaposimama leo kuzungumza huko Arumeru Mkapa atawaonesha huruma wapinzani na viongozi wao? Hivi akizungumza na kuwabeza wapinzani na kuwaita majina ya ajabu ajabu na kuwafanya duni viongozi wao atakuwa amewaonea au anafanya kile kinachotegemewa kama mwanasiasa wa CCM? Kama yeye hatowaheshimu - tayari kwa kukubali kushiriki kampeni hizi ameonakana hajali sana mambo ya upinzani - kwanini wao wanafikiria kumheshimu katika hili?

Nini cha kufanya basi?

a. CDM ioneshe kuwa CCM inamtumia mmoja wa viongozi waliosimika mfumo wa utawala wa kifisadi nchini mtu ambaye ana damu ya Watanzania mikononi mwake.

b. CDM ioneshe kuwa matatizo mengi ya madini nanishati yamejengwa kutokana na sera na sheria ambazo zilipitishwa na Mkapa.

c. CDM ioneshe vile vile jinsi kiongozi huyo huyo alivyoendelea kawaida ya kubeba na kubebana na kutolea mifano watumbalimbali. Ikumbukwe pamoja na yote yanayosifiwa kuhusu Mkapa bado leohii tunavuna mavuno ya uongozi wake.

d. CDM ioneshe kuwa mojawapo ya mambo ya ubaguzi wa rangi nchini kufanywa na wanasiasa yalifanywa wakati wautawala wake kuhusiana na Salim na jinsi gani yeye Mkapa kama kiongozi aliyelelewa na Nyerere alishindwa kuwazuia wale waliokuwa nakiu ya madaraka hadi kutupatia viongozi wa sasa. Kwa kifupi ioneshe kuwa viongozi wanaopigiwa debe na Mkapa ni utangulizi wa ufisadi!

e. CDM ioneshe kuwa CCM ilikuwa na nafasi nzuri ya kuonesha imeamua kweli kujivua gamba lakini yale yaliyotokea leo hii huko Arumeru na hasa kuhusishwa kwa BWM kunaonesha tu kuwa gamba limegoma na sasa limeganda na gamba likiganda linakuwa donda! Wapo baadhi ya watu wazuri sana ambao CCM ingewez akuwatumia lakini kwenda kumtumia mfalme wa magamba ni kosa kubwa la kimkakati!

CDM isiposhambulia pasipo huruma CCM na sera zake, isipoonesha kuwa matatizo yanayowakabili watu wa Arumeru (na sehemu nyingine nchini) yanatokana na kushindwa kwa sera za CCM (siyo kutekelezwa tu bali kushindwa in substance) basi itajikuta inaletwa karibu na kilele nakuachwa hewani! CDM ni lazima ichore mstari, iwagawe wananchi na kuwachochea wananchi kugawanyika kifikra. Pasipo kugawa fikra, hawatagawa kura!
Mkuu wangu haya makosa Chadema waliyafanya hata Igunga! Nilishangaa Mkapa kupiga kampeni ya nguvu huku CDM wakishindwa kueleza umma ukweli juu ya Mkapa! Wanadhani wananchi wote wanamjua Mkapa! Kosa kubwa kufikiri hivyo! cdm wamelazimishwa wasizungumzie Ufisadi kwani eti huo wimbo unaonesha hawana sera zingine! Cha kushangaza Mkapa anakwenda Arumeru kifua mbele alipo Mbowe,Dr Slaa na Zitto! Ustaarabu wa wapi kuonea haya mafisadi ambao hawajawahi hata kuomba radhi? CDM walipaswa kuchafua hali ya hewa juu ya Mkapa na El huko Arumeru hadi wahusika waogope kwenda!
CDM acheni kuona haya!!
 
Wanasahau kwamba Mkapa anapokuja anakuja na makorokocho yote ya "former president" kwa hiyo anakuja na msafari wa magari ya serikali, walinzi n.k Anakuja na ujiko wa kutosha kabisa kufanya mpambano kuwa ni one sided. Na kama Mkapa akitaka kuwabana kweli CDM asiishie kwenye kufungua tu bali arudi na kushiriki kampeni hadi mwisho! Sitotaka kusikia watu wanalalamika "ooh anatumia resources za serikali kwenye mazingira ya kisiasa".
 
Muda bado na kampeni zanaendelea watayazungumzia tu...siunajua ni ngumu kusema yote kwa siku moja coz ni mengi sana na muda hautatosha

Unafikiri Mkapa ataonesha hiyo consideration ya muda atakapozungumza baadaye leo? I bet you he will not spare words!
 
juzi ilikuwa ni uzinduzi tu.......makombora yanakuja juu ya huyu mkapa
Mkuu kwanza Mkapa kupata ujasiri wa kufanya kampeni ni dharau kubwa kwetu maana huyu alikuwa anaogopa hadi hafla za kitaifa zilizokuwa zinaandaliwa na chama chake! CDM wanafanya siasa waache kuwaonea haya hawa mafisadi! Uwashwe moto ikibidi tuhuma zote zibandikwe mitaani! Mkapa ameamua kuja kwenye public hadi anafanya kampeni wakati alisema amestaafu siasa na Kikwete akaomba aachwe apumzike! Kwavile kaamua kuja kwenye public waandishi msiowaoga na wananchi huko Arumeru mwambieni ajibu tuhuma zake zote! Asitufanye mazuzu ajibu tuhuma zake!
 
Ni kweli Mkapa ni mmoja kati ya watu wachache ambao wamesababisha matatizo yote yanayowakumba Watanzania kwa sasa. Lakini naamini kwenye uzinduzi wa kampeni lengo kubwa linakuwa ni kumnadi mgombea wenu kwa wapiga kura na wananchi kwa ujumla na kama ukitumia fursa hiyo kuelekeza mashambulizi kwa mtu ama kikundi cha watu unaweza ukashindwa kupeleka ujumbe uliokusudiwa. Wananchi wanataka kujua huyo mnayemnadi ana uelewa gani wa matatizo yanayowakabili na ataweka ama ana mikakati gani ya kukabiliana na matatizo hayo.

Nafikiri siku zijazo CDM watazingatia hilo na pengine tumwangalie BM yeye ataongea nini kwa wananchi wa Arumeru.
 
cdm, kwa kuwa hamna sera, kwa umaskini wenu wa mawazo na ukosefu wa mawazo, mtazungumza saana zaidi ya ccm, ufisadi na matukio mbalimbali ya humu ndani kuliko kuonesha njia.
 
Hivi the former Mr. Clean bado anaenda kufungua kampeni? Aibu kubwa kwa nchi hii, mafisadi hawana woga hata chembe!
 
Ni kweli hata mimi nilishangaa sana Igunga kwanini CDM walimhesimu wakati yeye hakutaka kuheshimiwa kwa kuwaita wapinzani majina ya ajabu ajabu? Kama leo Mkapa hata behave, naomba CDM wafanye yafuatayo wasiogope kuonekana hawana heshima kwa mtu asiyejiheshimu..

1. Wam associate Mkapa na Lowassa katika mambo yote ya kifisadi aliyoyafanya tena kwa sauti kubwa.
2. Wawakumbushe wananchi kuhusu Kiwira.
3. Wakumbushie alivyotumia ubaguzi wa rangi kumchafua Salimu.
4. Wawaambie wananchi wamuulize Mkapa aliko Balali.
 
cdm, kwa kuwa hamna sera, kwa umaskini wenu wa mawazo na ukosefu wa mawazo, mtazungumza saana zaidi ya ccm, ufisadi na matukio mbalimbali ya humu ndani kuliko kuonesha njia.
Chadema hawawezi kutekeleza kikamilifu sera zao bila Serikali! Tuone njia ili tuwasaidie kutawala? Kazi ya Chama na siasa ni kuonesha mlivyo wabovu na tunatoa suluhisho! Tukisema Mkapa ana tuhuma tunatoa na suluhisho kuwa huyu kwa aliyoyafanya hana kinga ashtakiwe!! Wananchi wa Arumeru wametawaliwa na CCM kwa miaka zaidi ya hamsini hivyo wanajua matatizo yao nani kayasababisha! CDM wanapaswa kuonesha njia na kuonesha kila uovu wa chama tawala!! Mkapa kajileta mwenyewe!
 
juzi ilikuwa ni uzinduzi tu.......makombora yanakuja juu ya huyu mkapa

Nakubaliana na Mwanakijiji, ilitakiwa Chadema wamuanzishie dozi siku ile ile ya uzinduzi, kwani kulikuwa na live coverage ya startv kwahiyo watu wengi wangenufaika na uzinduzi ule na huenda ccm wamepata nguvu za kumpeleka mkapa arumeru baada ya kuona hajaguswa na chadema.

Hata kama wataanza kumshughulikia katika mikutano mingine inayofuata lakini ilitakiwa wamshughulikie siku ya uzinduzi wa kampeni ili asithubutu kutia maguu arumeru.

Hata hivyo hawajachelewa sana wapiganaji waliko huko arumeru, bado wanayo nafasi ya kuanza kumshighulikia effectively kuanzia sasa hadi mwisho wa kampeni ili pamoja na mambo mengine ccm wasithubutu kumrudisha huko kwa ajili ya kufunga kampeni kama walivyofanya igunga.
 
Asubuhi hii mlioko Arumeru Pigeni kampeni ya nguvu Mkapa aumbuke! Hajatuomba radhi watanzania kwa ufisadi wa kutisha!
 
Labda kwa kuwa ni kwaresma atafunga break kidogokwenye mdomo wake , la sivyo chaguzi ndogo zitazidi kumvua nguo
 
Mojawapo ya vitu ambavyo labda vitahitaji majibu baadaye ni kwa vipi CDM wakati wa uzinduzi wao hawakumgusa kwa uzito unaotosha aliyekuwa Rais wa Tanzania wakati matukio mazito ya ufisadi yanatokea yaani B. W. Mkapa. Katika thread hii mengi yamejadiliwa kumuhusu Mkapa:

MKAPA ABOVE THE LAW? Chama cha Demokrasia na Maendeleo kilitambua kuhusika kwa Mkapa katika maamuzi ya kifisadi kiasi cha kumuweka namba 10 katika ile "Orodha ya Aibu" akiwa miongoni mwa kina Ballali, Rostam, Lowassa n.k. Katika maelezo ya orodha hii ilisemwa hivi:

Hiyo ni sehemu kidogo tu kwani baadaye tumeweza kuona mengi sana yaliyotokea wakati wake kama Rais na hasa wakati wa mwaka wake wa mwisho. Ikumbukwe ndiye aliyewakingia kina Ballali, Rostam na wengine. Ninajiuliza maswali yafuatayo:

a. CDM inamhofia au kumheshimu Mkapa kiasi kwamba yawezekana hakiamini kabisa kuwa anahusiana na ufisadi mkubwa kabisa uliowahi kutolewa nahivyo wananchi hawapaswi kukumbushwa?

b. CDM inaamini kuwa Mkapa hagusiki kwa vile Rais Kikwete alisema "muacheni mzee wetu astaafu" wakati hataki kustaafu anapenda kujihusisha na siasa? Kama anajiingiza kwenye siasa kwanini yeye mwenyewe naye aliyoyafanya yasiwe issue kwa Watanzania?

c. CDM inafikiria kwa mfano atakaposimama leo kuzungumza huko Arumeru Mkapa atawaonesha huruma wapinzani na viongozi wao? Hivi akizungumza na kuwabeza wapinzani na kuwaita majina ya ajabu ajabu na kuwafanya duni viongozi wao atakuwa amewaonea au anafanya kile kinachotegemewa kama mwanasiasa wa CCM? Kama yeye hatowaheshimu - tayari kwa kukubali kushiriki kampeni hizi ameonakana hajali sana mambo ya upinzani - kwanini wao wanafikiria kumheshimu katika hili?

Nini cha kufanya basi?

a. CDM ioneshe kuwa CCM inamtumia mmoja wa viongozi waliosimika mfumo wa utawala wa kifisadi nchini mtu ambaye ana damu ya Watanzania mikononi mwake.

b. CDM ioneshe kuwa matatizo mengi ya madini nanishati yamejengwa kutokana na sera na sheria ambazo zilipitishwa na Mkapa.

c. CDM ioneshe vile vile jinsi kiongozi huyo huyo alivyoendelea kawaida ya kubeba na kubebana na kutolea mifano watumbalimbali. Ikumbukwe pamoja na yote yanayosifiwa kuhusu Mkapa bado leohii tunavuna mavuno ya uongozi wake.

d. CDM ioneshe kuwa mojawapo ya mambo ya ubaguzi wa rangi nchini kufanywa na wanasiasa yalifanywa wakati wautawala wake kuhusiana na Salim na jinsi gani yeye Mkapa kama kiongozi aliyelelewa na Nyerere alishindwa kuwazuia wale waliokuwa nakiu ya madaraka hadi kutupatia viongozi wa sasa. Kwa kifupi ioneshe kuwa viongozi wanaopigiwa debe na Mkapa ni utangulizi wa ufisadi!

e. CDM ioneshe kuwa CCM ilikuwa na nafasi nzuri ya kuonesha imeamua kweli kujivua gamba lakini yale yaliyotokea leo hii huko Arumeru na hasa kuhusishwa kwa BWM kunaonesha tu kuwa gamba limegoma na sasa limeganda na gamba likiganda linakuwa donda! Wapo baadhi ya watu wazuri sana ambao CCM ingewez akuwatumia lakini kwenda kumtumia mfalme wa magamba ni kosa kubwa la kimkakati!

CDM isiposhambulia pasipo huruma CCM na sera zake, isipoonesha kuwa matatizo yanayowakabili watu wa Arumeru (na sehemu nyingine nchini) yanatokana na kushindwa kwa sera za CCM (siyo kutekelezwa tu bali kushindwa in substance) basi itajikuta inaletwa karibu na kilele nakuachwa hewani! CDM ni lazima ichore mstari, iwagawe wananchi na kuwachochea wananchi kugawanyika kifikra. Pasipo kugawa fikra, hawatagawa kura!

Mkuu uko sawa kabisa. Arumeru sio rahisi kama watu wanavyojiaminisha. Ukiangalia mgawanyo wake unatenganishwa na barabara ya Arusha - Moshi. Upande wa kusini unaoenda mpaka maeneo ya mererani unamchanganyiko mkubwa sana wa makabila na huku ndiko chadema inaweza kufanikiwa zaidi. Upande wa kaskazini huku kuna wameru peke yao. Sasa kwa mila za kimeru uongozi wa koo una sauti kubwa sana juu ya maamuzi. Mathalan SIYOI na NASARY wako kwenye ukoo mmoja. inamaana kama ukoo mmoja utagawanyika utsababisha na koo nyingine kugawanyika pia.
Kwa sababu hizi CDM ilitakiwa kuua nzi kwa Rungu! CCM wakipata nafasi huwa hawaichezei! Hebu fikiria wewe unapata mafuriko ya watu wanaokuja wenyewe kwenye mkutano wako halafu mwenzio anapata idadi kama yako lakini akiwa amewalipia nauli na chakula unadhani akiipata nafasi ya kukuua ataiacha?
Kingine ninaweza kuwa na hofu ya CDM kuwa corrupted. Sote tunakubaliana kwamba gharama za kuendesha CDM zimekuwa kubwa kupita matarajio. Haraka haraka unaweza kujiuliza watamudu vipi? sasa hapa napata shaka kama baba mkwe hajaamua kumnunulia mwanae ubunge kwa sharti ufisadi na mafisadi wasitajwe!
VIONGOZI WETU MSIANZE KUWA SOFT!
 
Mpingauonevu,

Hapo kwenye nyekundu bado sijakusoma, hebu funguka tena.
 
Back
Top Bottom