Namashaka na uzalendo wa rais kikwete kwa tanzania | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Namashaka na uzalendo wa rais kikwete kwa tanzania

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by hittler, Jul 26, 2011.

 1. h

  hittler Member

  #1
  Jul 26, 2011
  Joined: Jul 18, 2011
  Messages: 55
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Matatizo yanayoikumba nchi kwa sasa mengi yanaletwa na watendaji wabovu wa serikali ya rais Kikwete,wizi wa kutisha kwenye sekta za serikali kama kule UDOM, wizara ya nishati na madini na halmashauri za wilaya siyo yakufumbiwa macho. Inashangaza sana kila tukio la uwizi likiripotiwa CAG anapewa kazi ya kupitia lakini majibu yake yamekuwa tofauti na matarajio ya wengi, yeye huwa haoni kasoro yeyote kitu ambacho ni uongo. Najaribu kujiuliza au CAG ana kampuni zake za auditing ambazo anaogopa kuzi umbua kwa kwenda kinyume nazo sehemu ambazo zimefanya kazi ya auditing na baadae kupatikana tatizo?
  Watendaji wote hawa Rais ndiyo kawateua na ana mamlaka nao, iweje Waziri mkuu Pinda aongee hadi alie alafu rais ashindwe kuwabadili au kuwawajibisha? Je, kuwa CAG ni lazima ukae miaka kumi? Na je, adhabu ya wanaotuingiza kwenye umaskin ni kuhamishwa ofisi na si kufilisiwa au ata ku hukumiwa? Kama kweli rais anapokea malalamiko haya na anayajua ila anakaa kimya, sina shaka kuwa hana uzalendo wowote katika nchi ila nae yupo kimaslai, akumbuke kwamba uelewa umeongezeka na urais ni miaka kumi tu, tutabadilisha katiba ili tuweze washtaki ata marais, nahofia rais Kikwete anaweza akawa rais wa kwanza kushtakiwa kama tukibadili katiba ili iwe fundisho, achague lipi bora kati ya kukitumikia kifungo au kuwafukuza kazi watendaji wabovu.
   
 2. M

  Mapujds JF-Expert Member

  #2
  Jul 26, 2011
  Joined: May 12, 2011
  Messages: 1,291
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 135
  Pole ndugu yangu nchi imeoza hii jamani.
   
 3. Mzalendo80

  Mzalendo80 JF-Expert Member

  #3
  Jul 26, 2011
  Joined: Oct 30, 2010
  Messages: 2,385
  Likes Received: 122
  Trophy Points: 160
  Kikwete sio Mzalendo bali ni Mwizi wa rasilimali zetu
   
Loading...