Uchaguzi 2020 Nalitamani jimbo la Arusha mjini,ni wakati wa vijana wachapa kazi

Idd Ninga

Verified Member
Nov 18, 2012
4,936
2,000
Haja yangu ni kuliona jimbo la Arusha mjini likiwa Geneva ya kweli ya Afrika,kuigeuza na kuifanya Arusha kuwa makao makuu ya utalii Afrika ya mashariki na kati na kuweka mikakati na mipango na wadau wa utalii katika jimbo hili kuhakikisha utalii unatangazwa na vijana wanapata ajira ya uhakika kupitia sekta hii mama katika jimbo hili.

Nitahakikisha haki na usawa unapatikana kwa wafanyakazi wa jimbo hili,nitwaunganisha na kutengeneza vyama vya wafanyakazi vitakavyokuwa na sauti yenye nguvu na itakayosikika na kufanyiwa kazi na serikali,wafanyakazi wa chini nitawahakikishia wanajiona kuwa ni sehemu ya watu wanaostahili kupata haki zao,malipo yao ya zaida,mikataba yenye nguvu katika kazi,nitawatengenezea mazingira ya kuwa sehemu ya jamii inayosikilizwa nchini Tanzania.

Nitaanzisha mpango wa vijana kujiendeleza kielimu na kuanzisha masomo ya jioni kwa ajili yao kwa ajili ya kuwaandaa kuwa wataalamu watakaoendesha maisha yao na kufikia viwango vya juu vya elimu,elimu ya watu wazima itaimarishwa katika misingi rahisi,watoto na wanafunzi wasiokuwa na uwezo wa kupata mahitaji ya shule watapata kupitia mfuko maalumu utakaotengenezwa kwa ajili yao.

Nitahakikisha serikali inaboresha mazingira ya upatikanaji wa matibabu kwa wakazi wa Arusha mjini,madawa yafike kwa wakati na bima maalumu ianzishwe kwa ajili ya watu masikini na wasiokuwa na uwezo.

Kama mbunge wa Arusha mjini,nitaweka mkakati wa kuzungumza na watu wangu kila mwisho wa mwezi,mazungumzo ambayo yatakua ni mazungumzo ya wazi na kila mtu atakua na uhuru wa kuuliza au kutolea maoni chochote katika jimbo langu.

Nitaunganisha taasisi na asasi zote za maendeleo,kina mama,watoto,kina baba na vijana kwa ajili ya kupata fursa mbalimbali zitakazotokea,itakua Arusha ya uwazi,Arusha ya fursa,Arusha ya maendeleo,Arusha ya mfano.

Ni wakati wa mabadiliko katika jimbo la Arusha mjini,ni wakati wa vijana wachapakazi wasio na maneno,ni wakati wa kuileta Arusha pamoja.

Natangaza nia rasmi ya kugombea ubunge jimbo la Arusha mjini.

Asanteni.

Idd Ninga.
Arusha Mjini
04.07.2020
 
Idd Ninga

Verified Member
Nov 18, 2012
4,936
2,000
Labda ukaongoze ma-abdool wenzio miskitini huko
Usitake kuingiza jambo ambalo halipo,tafadhali tuache tufanye siasa zetu za amani,upendo,umoja na siasa zenye roho na utamaduni wa mtanzania,hizi unazotaka kuzianzisha hatuzihitaji Tanzania.
 
Idd Ninga

Verified Member
Nov 18, 2012
4,936
2,000
Aisee, hawawezi hitaji mtu kama wewe nauhakika huo.
nishakuchimba chimba sana Sir hujuagi tu!
.
anza kujipanga sasa upya badirika, usibishane hovyohovyo, mijadala ya dini achana nayo kuwa kama wanasiasa wengine walioko JF.
they're so smart wanacheza kama Pele
Ulijisahau sana,wakati ukichimba Na wewe ulikuwa unachimbwa vizuri sana bila kujijua, Ndio maana katika mijadala mingi nilikuwa na kuingiza usipotaka na ukaingia kilaini kabisa.
Kumbuka, wana Arusha hawahitaji mijadala ya dini, wanahitaji maendeleo,hawahitaji maneno wanahitaji kusonga mbele.
Unajificha nyuma ya ID fake na bado unajulikana hadi ukucha,unaonaje hilo ?
 
Idd Ninga

Verified Member
Nov 18, 2012
4,936
2,000
Nishakupima sana humu kwenye mijadala mbalimbali achilia mbali jukwaa la dini.
Huna uwezo wa kuongoza watu hata wawili wewe, uwezo wako wakujenga hoja ni mdogo vilevile upeo wako wa fikra ni mdogo sana.
.
Kama mtu mwenye utimamu wa fikra na mwenye malengo mazuri na makubwa usingejihusisha na mijadala ya kidini KABISA.
.
Pili ungeonyesha uwezo wako mkubwa wa kujenga hoja kwenye kila unaloliandika regardless of ni mtu gani anakujibisha.
Wewe ni mtu mbishi alafu ubishi wako wa kishamba (utaniwia radhi huu ndo ukweli) na hujui kuishi na watu ambao watakuwa manufaa kwako na licha ya uwehu au u-genius wao.
Ndio sababu kubwa ya kulichukua jimbo hili, hatutaki kuwa na watu wanaokubali kila wanachoambiwa eti kwa sababu tu wataonekana wabishi,tunataka kuwa na watu watakaosimamia katika hoja zao hata kama wataonekana viroja, tunataka vijana watakaoibadili Arusha yao na kufikia maendeleo na uchumi imara, hatutaki watu wa ndio mzeee, Ndio mzeee
 
SHIMBA YA BUYENZE

JF-Expert Member
Dec 22, 2014
137,457
2,000
Nishakupima sana humu kwenye mijadala mbalimbali achilia mbali jukwaa la dini.
Huna uwezo wa kuongoza watu hata wawili wewe, uwezo wako wakujenga hoja ni mdogo vilevile upeo wako wa fikra ni mdogo sana.
.
Kama mtu mwenye utimamu wa fikra na mwenye malengo mazuri na makubwa usingejihusisha na mijadala ya kidini KABISA.
.
Pili ungeonyesha uwezo wako mkubwa wa kujenga hoja kwenye kila unaloliandika regardless of ni mtu gani anakujibisha.
Wewe ni mtu mbishi alafu ubishi wako wa kishamba (utaniwia radhi huu ndo ukweli) na hujui kuishi na watu ambao watakuwa manufaa kwako na licha ya uwehu au u-genius wao.
Za uso laivu mchana kweupeeee. JF bana !!!

Ubaya wa mijadala ya kidini huwa ni migumu na kwa kawaida haina mshindi sana sana ni kutukanana tu kama majuha. Miye huiepuka kila inapowezekana !
 
Proved

JF-Expert Member
Sep 10, 2018
11,160
2,000
Haja yangu ni kuliona jimbo la Arusha mjini likiwa Geneva ya kweli ya Afrika,kuigeuza na kuifanya Arusha kuwa makao makuu ya utalii Afrika ya mashariki na kati na kuweka mikakati na mipango na wadau wa utalii katika jimbo hili kuhakikisha utalii unatangazwa na vijana wanapata ajira ya uhakika kupitia sekta hii mama katika jimbo hili.
Nitahakikisha haki na usawa unapatikana kwa wafanyakazi wa jimbo hili,nitwaunganisha na kutengeneza vyama vya wafanyakazi vitakavyokuwa na sauti yenye nguvu na itakayosikika na kufanyiwa kazi na serikali,wafanyakazi wa chini nitawahakikishia wanajiona kuwa ni sehemu ya watu wanaostahili kupata haki zao,malipo yao ya zaida,mikataba yenye nguvu katika kazi,nitawatengenezea mazingira ya kuwa sehemu ya jamii inayosikilizwa nchini Tanzania.
Nitaanzisha mpango wa vijana kujiendeleza kielimu na kuanzisha masomo ya jioni kwa ajili yao kwa ajili ya kuwaandaa kuwa wataalamu watakaoendesha maisha yao na kufikia viwango vya juu vya elimu,elimu ya watu wazima itaimarishwa katika misingi rahisi,watoto na wanafunzi wasiokuwa na uwezo wa kupata mahitaji ya shule watapata kupitia mfuko maalumu utakaotengenezwa kwa ajili yao.
Nitahakikisha serikali inaboresha mazingira ya upatikanaji wa matibabu kwa wakazi wa Arusha mjini,madawa yafike kwa wakati na bima maalumu ianzishwe kwa ajili ya watu masikini na wasiokuwa na uwezo.
Kama mbunge wa Arusha mjini,nitaweka mkakati wa kuzungumza na watu wangu kila mwisho wa mwezi,mazungumzo ambayo yatakua ni mazungumzo ya wazi na kila mtu atakua na uhuru wa kuuliza au kutolea maoni chochote katika jimbo langu.
Nitaunganisha taasisi na asasi zote za maendeleo,kina mama,watoto,kina baba na vijana kwa ajili ya kupata fursa mbalimbali zitakazotokea,itakua Arusha ya uwazi,Arusha ya fursa,Arusha ya maendeleo,Arusha ya mfano.
Ni wakati wa mabadiliko katika jimbo la Arusha mjini,ni wakati wa vijana wachapakazi wasio na maneno,ni wakati wa kuileta Arusha pamoja.
Natangaza nia rasmi ya kugombea ubunge jimbo la Arusha mjini.
Asanteni.

Idd Ninga.
Arusha Mjini
04.07.2020
Unataka ugombee ubunge kupitia chama gani?
 
fazili

JF-Expert Member
Jun 10, 2011
8,035

Mwache kamanda Lema wewe tafuta jimbo lingine kwa tiketi ya CDM.
 
Idd Ninga

Verified Member
Nov 18, 2012
4,936
2,000
Nahmala, huyu jamaa ana shida tena kubwa ukipitia messages zake ambazo anabishana na watu kwenye mambo ya dini au ya kawaida kabisa utacheka uanguke.
.
Ni mbishi alafu bora angekuwa mbishi mwenye uwezo wa kupambania ubishi wake ni HAWEZI sometimes huwa nafikiri huyu mwamba ana kigugumizi itakuwa.
.
Yani hata kama yuko CHADEMA huyu hata udiwani hauwezi akacheze miskitini huko, huyu akiwa kiongozi wa jamii zetu ambazo ni so diversity akiitwa Kanisani kufanya jambo atafanya unafiki maana wakulungwa tumeshamjua.
Atakuwa mlingania dini na si kiongozk wa wananchi pumbavu pumbavu tu.
Naona unahangaika sana kutaka kuileta mada ya udini,ila hebu kaa pembeni hiyo si hoja yangu kwa sasa, ubishi ni sehemu yangu ya kutetea hoja zangu, kama ungetaka nisiwe mbishi basi ungekubali like ninachokisema,yani unakataa ninachokisema halafu bado unaniona mimi mbishi,kila mtu ana dini yake lakini katika siasa hakuna wapagani wala hakuna upendeleo wa kidini.
unachotaka wewe ni kutaka kuwalazimisha watu waingie katika hoja ya kipumbavu ya UDINI.
kwa hill koma sana,usitake kuingiza ujinga huu, nakwambia tena upuuzia wa udini haupo katika hoja zangu, Kama kweli wewe mwanaume na una uwezo wa kujibizana hoja na mimi, tukutane tu majukwaani live live, siyo unajificha hapa na ID fake yako halafu unapiga kelele za mambo ya dini,katika tangazo langu sijaongelea huo upuuzi wako.
Nasema tena, acha ujinga wa kuhusisha dini katika hili.
 
Mc cane

JF-Expert Member
May 18, 2018
5,356
2,000
"Siasa za amani, upendo, umoja na siasa zenye roho na utamaduni wa mtanzania"

Nikisikiaga hizi kauli kwa siasa za Tanzania huwa nacheeeeka.... Kwa dharau
Usitake kuingiza jambo ambalo halipo,tafadhali tuache tufanye siasa zetu za amani,upendo,umoja na siasa zenye roho na utamaduni wa mtanzania,hizi unazotaka kuzianzisha hatuzihitaji Tanzania.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom