Nalisihi jeshi la polisi kuacha unyanyasaji kwa wananchi

X_INTELLIGENCE

JF-Expert Member
Mar 25, 2014
10,344
14,119
Nalipenda sana jeshi la polisi ila nina chuki ya wazi na utendaji wa watendaji wa jeshi hilo...nahisi wanafuata maagizo ya watu ambao hawana taaluma ya usalama... Nakumbuka kipindi nipo mdogo mama yangu alikuwa MAMA LISHE siku moja walivamiwa na askari kulikuwa na jungu kubwa la SUPU askari wale walimwaga... wakamwaga vyakula wakaona haitoshi wakabomoa banda la mama...nililia sana siku ile nilipatwa na uchungu sana...nilimuone huruma sana mama yangu nikawa nawaona askari ni adui, adui mkubwa...

DSC_0516.JPG

Kipindi hicho ndicho kipindi kile kile jeshi hilo liliua watu wengi sana pale mwembe chai...kuna matukio mengi yakibabe yanaendeshwa na hili jeshi..matukio ambayo ni ya unyanyasaji sana...pengine ni kwasababu jeshi hilo linapokea maagizo kutoka sehemu mbali mbali zenye mamlaka...si sahihi kabisa jeshi kutumiwa vibaya, jeshi la polisi lingetakiwa kuambatana bega kwa bega na wananchi ili tulinde nchi yetu kwa pamoja...Polisi kwanini mnatumwa mtupige mabomu...Mnajeruhi ndugu zetu wanaoitafuta haki kwa halali...
Wakijiandaa%2Bkulipua%2Bmabomu%2Bmbele%2Bya%2Bkituo%2Bcha%2Bpolisi..JPG

Kwanini askari mnatumia nguvu nyingi sana kupambana na wananchi wanaojitafutia riziki ya halali...? Mnatufanya tukose amani tutakimbilia wapi wananchi sehemu pekee ambayo ingekuwa ndio mkombozi wetu inatumiwa kwa matakwa ya watu wachache wenye nguvu...

Kumbukeni nyie ni wananchi kama sisi na kazi mtu haifanyi milele kuna kustaafu au kufukuzwa mabaya mnayotutendea leo ipo siku na nyie yatawarudia tuu..

IMG_0813.JPG

Jeshi ni letu sote tukaeni pamoja tushirikiane tuijenge nchi yetu... Nchi haiwezi kujengwa kwa mabomu...kwa virungu na manyanyaso...ndio maana hata muasisi wa nchi hii hayati BABA WA TAIFA MWALIMU NYERERE alipoitaji tuwe huru alitumia demokrasia akawashawishi waliokuwa wanaotunyonya hatimae tukawa huru...

10-8-2008+1-30-26+PM_0125+-+Copy.jpg

MWALIMU NYERERE alijua kuwa akitumia mabavu kuwashawishi mababu zetu wapigane tungeuwawa wengi na tusingefika kokote...hivyo askari nawaomba mjifunzi kupitia muasisi huyu wa taifa letu...msitupige wananchi...msituoige mabomu msitumwagie maji ya kuwasha...msitutese...badala tuelimisheni juu ya kutii sheria ikiwezekana ongezeni somo la sheria darasani watoto wazijue sheria...ikiwezekana kutokana na ongezeko la mitandao mngefungua forum maalum kwaajili ya kuelekeza sheria zile muhimu...ila mkitumia mabomu kutuelekeza mtatuua mtatuua sana...tukimbilie wapi?

mabomu.jpg

Mkiwa kama jeshi kataeni kupelekwa pelekwa na matakwa ya watu wowote wale...tafute suluhu kwa njia ya amani...amani...amani...msiwapige viongozi wa dini msiwahukumu kwa makosa ya uongo makosa ya kuwasingizia ilimladi tu muwafedheheshe...acheni kabisa badala yake tumieni viongozi wa dini kunyoosha na kuwafanya raia turudi kwa MUNGU kwani sijawahi kuona kiongozi wa dini anaehubiri mapigano kanisani ama msikitini...kumbukeni ata wabepari walivyotaka kututawala walituletea kwanza imani za dini...

Muslim_police+(6).jpg

Kwanini msitumie nguvu nyingi kupambana na makahaba wanaoipa sifa mbaya nchi yetu ...ninani asiejua kuwa palipo na ofisi ya kamanda wa mkoa wa tanga usiku eneo lile kuna makahaba wanafanya ukahaba nje ya jengo la ofisi hiyo...

P1000493.JPG

Jirani na ofisi hiyo kuna maktaba ambayo imepakana na eneo lililopambwa kwa maua ya kupumzikia ni vichekesho sana ukitembea hapo nyakati za usiku...
polisi tumieni weredi wenu mpana kupambana na majangiri wanaotumalizia

Tembo...majangiri wanaomaliza wanyama wetu wa porini...pambaneni na wauza madawa ya kulevya...pambaneni na mafisadi...toeni adhabu kali kwa vijana wanaotumia madawa ya kulevya...tunakabwa na mitaa yenye vibaka mnaifahamu kwanini msiweke malindo maeneo hayo hatarishi?

Sina nia mbaya, ni ushauri tuu mkiona nimekosea kuongea hayo mniwie radhi....
 
no hawapelekwi kama bendera ila kwa nature ya kazi yao jibu ni ndio afande hakuna kupinga pinga ila wanapoenda kutekeleza wajibu wao hapo ndo shida inategemea uwezo wa askari mmoja mmoja
aisee ila inahuzunisha sana sasa kwanini hao wanaowatuma waiwatume waende wakawakamate wale walioiba fedha eg...escro..mtu anaiba mabilion
 
Sisi wana diplomasia tunafahamu kwamba ili umtawale raia lazima umtetemeshe katika kipindi chote cha maisha yake, nahuku ndiko kufanikiwa kwa serikali, hakuna namna. Mnyuzi maneno yako ni sawa unafuta ziro alafu unaandika sifuri.
 
Sisi wana diplomasia tunafahamu kwamba ili umtawale raia lazima umtetemeshe katika kipindi chote cha maisha yake, nahuku ndiko kufanikiwa kwa serikali, hakuna namna. Mnyuzi maneno yako ni sawa unafuta ziro alafu unaandika sifuri.
kumbe ila wakumbuke mjinga akielevuka...mjanja yupo mashakani
 
Leo nimependa kukumbuka kuwa polis wanawazir mpya lakin utendaj wao bado ni ule ule, ndipo nikauliza swali hili Kwa sababu thread ya kumkaribisha tulimwambia mengi bila kusahau mchango maridhawa wa saa8 .

Tukiamin nii mwanajf anasoma michango atabadlisha chombo hiki lkn cjui anasita au anasoma makabrasha pengine anafundwa au anajichua chuon moshi au bado anashona sare yake.

Nafikiri tu kwa kina lkn si hitimisho la hoja ya ukimya wako na muendelezo wa ubabe wa polisi Kwa vyama na raia, jitokeze useme tuelewe tunakoenda na jeshi kama ukiendelea kuwa kimya tutaamin nawe ni bar a ka ktk magumu yote ya watz

Ramark kutoka liwale
 
Mods dhumuni la thread yangu na hii zinalingana

Swali Kwa wazir na
Hoja ya polisi pekee
 
Mikononi mwa polisi wimbo wa mbunge wa mbeya mjini enzi hizo anaitwa mr two na mim kupitia thread hii naufanya uwe chaguo maalumu kwa wote tulowahi kuwa mikononi mwa polisi iwe police post au central
 
Back
Top Bottom