Nalipongeza jeshi la polisi Tanzania | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nalipongeza jeshi la polisi Tanzania

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Magobe T, Nov 2, 2010.

 1. M

  Magobe T JF-Expert Member

  #1
  Nov 2, 2010
  Joined: Mar 19, 2008
  Messages: 2,945
  Likes Received: 357
  Trophy Points: 180
  Kipindi hiki cha uchaguzi, nimeona mabadiliko katika utendaji wa jeshi la polisi kitu ambacho kimenifanya niandike hii post kulipongeza. Kutokana na vurugu ambazo zimekwishatokea, ni wazi raia wengi wangekuwa wameshapoteza maisha au kutiwa vilema vya maisha.

  Lakini nimeona kuwa polisi wameonesha kubadilika sana! Kama ni mafunzo ndio yaliyowabadilisha, waendelee kufunzwa kutenda kazi kiustaarabu kama ambavyo wameweza kufanya. Kumbe inawezekana kwa jeshi letu la polisi kutoa ulinzi hata kama raia wana fujo kiasi gani bila kutumia risasi za moto au kuwajeruhi raia vibaya na hata kuwatia vilema vya bure. Nilikuwa nimeshaondoa imani yangu kwa jeshi la polisi hasa pale walipokuwa wakiwapiga raia bila sababu za msingi lakini sasa naanza tena kuirudisha. Miaka ya huko nyuma haikuwa hivi. Kilichobaki ni kupiga vita rushwa na kubambikia watu wasio na hatia kesi.

  Hongera jeshi letu la polisi!
   
 2. coby

  coby JF-Expert Member

  #2
  Nov 2, 2010
  Joined: Nov 28, 2008
  Messages: 342
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Kwa kweli hata mimi nalipongeza sana Jeshi la Police. Nilichogundua ni kuwa hata Police wanapenda mabadiliko na ndio maana walikua very patient ili watu waonyeshe hisia zao kali na haki itendeke. Kwa ilivyokuwa Arusha na Mwanza ingekuwa zamani tungekua tumezika mamia ya raia. Kuna taarifa kuwa wakala mmoja wa CCM Iringa aligoma kusaini form ya matokeo baada ya kuona mgombea wake kapata kura chache mno na jitihada za kumsisitiza ziligonga mwamba hadi afande aliyekuwa anasimamia akamchapa kibao ndio akasaini form
   
 3. Jatropha

  Jatropha JF-Expert Member

  #3
  Nov 2, 2010
  Joined: Apr 9, 2009
  Messages: 1,152
  Likes Received: 144
  Trophy Points: 160
  Pamoja na mafunzo, askari polisi wengi ni vijana wenye umri ulio sawa na wapiga walio kura wengi hivyo wanashare thoughts. Kutokana na viongozi wa serikali kutowathamini wananchi wakiwemo polisi na familia zao, askari hao hawaoni sababu zozote za kuwapiga wananchi wanapodai haki zao kutokana na CCM kutaka kuchakachua kura. Baadhi yao wamedai kuwa kuvipia kura hata vyama na wagombea wa upinzani kutokana na utendaji mbovu wa CCM na viongozi wake. Hivyo wananchi wanapoanda,mna kudai kura za wapinzani moja kwa moja wanakuwa wanawakilisha matakwa ya baadhi ya askari hao.

  Mmoja wa FFU katika usimamizi wa uchaguzi aliniamabi kuwa vifaa alivyovaa mwilini vinafikia Kilo 20 na alikua amesimama kwa zaidi ya masaa 24 wakati naongea naye bila ya kula wala posho. Hivyo kwa namna moja au nyingine wananchi wanakusanyika kudai matokeo kutangazwa mapema wanwasaidia askari hao kupata muda wa kupumzika kwa kuwa wenye nia ya kuchakachua kura ndio wanachelewesha kutangazwa kwa matokeo.
   
 4. Kachanchabuseta

  Kachanchabuseta JF-Expert Member

  #4
  Nov 2, 2010
  Joined: Mar 8, 2010
  Messages: 7,290
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  Husipongeze maana Urais Bado
   
 5. Bhbm

  Bhbm JF-Expert Member

  #5
  Nov 2, 2010
  Joined: Oct 31, 2009
  Messages: 716
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 35
  Hilo nalo neno kakaaaaa!!!!!!!!!!
   
 6. KakaKiiza

  KakaKiiza JF-Expert Member

  #6
  Nov 2, 2010
  Joined: Feb 16, 2010
  Messages: 10,543
  Likes Received: 2,257
  Trophy Points: 280
  Naomba hapo kwenye Red udadafue Tafadhali!
   
Loading...