Nalipenda sana Jeshi langu la JWTZ ila nilichokiona jana pale TPDF Golf Club getini kabisa hakikuwa cha kiungwana

Mzukulu

JF-Expert Member
Feb 14, 2020
1,401
2,631
Ilikuwa ni mida ya Saa 5 asubuhi kuelekea Saa 6 mchana ambapo Mzukulu nilikuwa napita zangu ndipo nikashikwa na butwaa hadi Masikitiko makubwa baada ya kuona Kijana (nadhani alikuwa nae ni Askari) akiwa amelazwa chini katika Geti la Kuingilia TPDF Golf Club huku amebebeshwa bonge la chuma na Kuambiwa alinyanyue juu huku anayemwambia hivyo akiwa anafagia zake taratibu Kuzunguka kile Kibanda cha Walinzi.

Sikatai na wala sipingani na utaratibu wa JWTZ (TPDF) katika kuwaadabisha kwa kuwapa Adhabu Maaskari (Wanajeshi) wao kwani najua ni kitu cha kawaida Kwao na kwa Majeshi mengi duniani ila kilichonisikitisha Mimi ni Mazingira husika ya tukio lenyewe ambapo kwa uelewa wangu (na hapa nakaribisha kukosolewa) nadhani halikuwa na uungwana na ni kama vile lilikuwa la kukomoa vile.

Kwanza Mhusika alikuwa akihenyeshwa hivyo Getini kabisa (tena Geti Kuu) la Kuingilia TPDF Golf Club halafu katika Kuonyesha kuwa mtoa hiyo adhabu alikuwa na lake jambo alikuwa kama akiona wanaopita nje (Raia) ni wanaume alikuwa anamwambia ainue lile chuma na atulie nalo tuli lakini akiona tu raia wanaopita nje ni akina dada basi Mtoa adhabu ndiyo alikuwa anapata Morali (Moto) wa kumuamrisha na kumuadabisha yule askari kiasi kwamba nilijisikia vibaya mno.

Hivi huyo mtoa adhabu alishindwa nini kumuadhibu yule Afande sehemu nyingine ambayo wangekuwa wao wawili tu au kule nyuma ambako watu huwa hawapiti ili aweze kumuhenyesha vizuri kuliko kuja kumhenyesha askari pale getini kabisa ambako kila mtu alikuwa akimuona (hasa Sisi Raia) akina Mzukulu kiasi kwamba nahisi yule afande mhenyeshwaji alijisikia vibaya sana?

Na sijui yule askari aliyekuwa akihenyeshwa vile alifanya nini masikini ya Mungu. Kweli cha moto askari kakiona na kakoma!
 
Nina rafiki aliniambia jeshini walikuwa wanatumwa kwenda kukata kuni mwendo kama wa masaa manne kwenda na kurudi,wakisharudi na kutua mzigo wa kuni kambini anakuja Afande mmoja wa cheo cha juu anasipangusapangusa kwa vidole anawaambia kuni chafu zina vumbi waende mtoni wakazioshe alafu ole wako ukatae, baadaye alikuja kuachana na mambo ya Jeshi kwa sababu kama umekosea MP anakusotesha tu anavyotaka, una haki ya kukataa lakini utapoteza ajira kwa utovu wa nidhamu.
 
Ndo adhabu zao hizo mzee... Lengo la adhabu za jeshi ni kukomoa labda wewe hukuishi mazingira ya karibu na jeshi la jwtz... Mimi niliishi maeneo hayo.

Kuna siku mzee fulani alikuwa anatafuta kuni kazunguka maeneo mengi akakosa... Kuna eneo lilikuwa prohibited na wanajeshi hivyo kuni zilikuwa nyingi hilo eneo kutokana na raia kuhofia kwenda pale.Mzee akazama hilo eneo akaokota mzigo wa kutosha akaufunga na kamba mkubwa kwelikweli...

Alipomaliza akaanza tena kufanya harakati apate fungu lingine... Muda si mrefu wazee wa kazi wakatua watatu hivi....Wakamuuliza umekusanya kuni kiasi gani akaonyesha mzigo wa kwanza.... Wakamwambia fanya kuubeba akabeba... Fanya kama unatembea kwenda kwako,akageuka akawapa kisogo akatembea hatua chache wakamwamuru simama..,mzee akatii.... Wakamwambia hivyo hivyo tulia na mzigo kichwani...

Ukapita muda mzee akaanza kuchoka jasho hilo..., akawauliza mpaka saa ngapi wakamjibu hadi kuni ziyeyuke..,mzee akaanza kulia....hivyo hivyo kalia wee baadaye akasikia sauti nyuma zinamcheka....mzee kutafakari akagundua ni sauti za watoto na wanawake... Katupa mzigo chini kucheki nyuma wakazi wa lile eneo wanamcheka.... Kumbe wazee wa kazi washasepa zamaaani...Alitoka nduki na mzigo kaacha.. Nyuma watu hoi... Hatasahau nadhani...

Siyo hiyo tu kuna case nyingine nyingi tu nimezishuhudia... Hata mimi nusura wanibananishe usiku mmoja sema kilichonisaidia nilikuwa mwanafunzi bado... Nilitoka kucheki movie za Rambo na Van Dame ....Halafu sikuwa na kitambulisho cha uwanafunzi... Nilipowaambia sina kitambulisho basi wakaanza what is hiki what is kile... Mara explain hiki sijui jieleze kwa kiingereza... Uzuri maswali mengi kama si yote niliyapata.. Wakanipapasa papasa wakagundua sina chochote cha kudhuru mtu... Wakaniachia nilifurahi sana coz nilijua ni kipigo tu kinafuata... Watu noma wale asee.
 
Hukupitia JKT? Kambi zote zina kitu wanaita "Quarter guard", ambapo ndiyo geti kuu la kuingilia kambini na ndipo makao makuu ya Polisi jeshi MP wa kikosi husika na ndipo palipo na mahabusu ya kikosi husika. Waliopitia JKT wameshanielewa ila raia mtakuwa na mitazamo ya kiraia.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom