Nalinganisha gawio langu la NMB na CRDB

Koryo2

JF-Expert Member
Nov 28, 2016
2,056
2,515
Mimi ninayo hisa 3500 katika CRDB na hisa 3500 ktika NMB. Leo nimepata taarifa kwenye simu ya ngu kuwa nimepata Tshs. 565,000 kama Gawio toka NMB lakini hisa hizo hizo kutoka CRDB nitapata Tshs.35,000.

Naomba sana mnielekeze utaratibu wa kuuza hisa zangu za CRDB kwasababu naona kama CRDB hawana nia na wanahisa wao.
 
Mimi ninayo hisa 3500 katika CRDB na hisa 3500 ktika NMB. Leo nimepata taarifa kwenye simu ya ngu kuwa nimepata Tshs. 565,000 kama Gawio toka NMB lakini hisa hizo hizo kutoka CRDB nitapata Tshs.35,000. Naomba sana mnielekeze utaratibu wa kuuza hisa zangu za CRDB kwa sababu naona kama CRDB hawana nia na Wanahisa wao.
Gawio linategemea pia thamani ya hisa zenyewe. Hiza moja ya NMB ina thamani zaidi ya hisa ya CRDB ....... hata leo ukiamua kuziuza hizo hisa, utapata pesa nyingi kutoka NMB.
 
Niliomba mkopo toka may mwanzoni wanasema uhakiki wawatumishi bado unaendelea kwahiyo hawawezi toa mkopo. Hii bank inahali mbaya sana
 
Wala sio madudu,thamani ya hisa inafanya upate gawio kubwa au dogo. Hisa za NMB ziko juu zaidi ya CRDB.
Ukimnukuu na kumjibu mtu jaribu kusoma kwanza alichoandika ili uelewe unajibu nini!
Mimi nimeongelea CRDB as whole na sio Hisa za CRDB. Na ndio maana nikapendekeza ifumuliwe na kuundwa upya. Baadhi ya wateja wa hii Benki watanielewa naongelea nini!
 
Ifumuliwe halafu? Wenye hisa ndii wenye maamuzi,kama wanaona benki yao haifanyi vizuri CEO atatimuliwa,kama inafanga vizuri usitegemee jambo kama hilo kutokea. Hawaendeshwi kwa mihemko.
 
Ifumuliwe halafu? Wenye hisa ndii wenye maamuzi,kama wanaona benki yao haifanyi vizuri CEO atatimuliwa,kama inafanga vizuri usitegemee jambo kama hilo kutokea. Hawaendeshwi kwa mihemko.
Nitakupuuza kwa sababu unaonekana unachangia ki ashki majnuni na sio kwa hoja.
Endelea na unavyoamini. Muda ukifika ndio utajua. Mimi naongea Kama mwana Hisa wa CRDB na mdau/mjumbe wa DSE.
 
Gawio linategemea pia thamani ya hisa zenyewe. Hiza moja ya NMB ina thamani zaidi ya hisa ya CRDB ....... hata leo ukiamua kuziuza hizo hisa, utapata pesa nyingi kutoka NMB.
Huyu jamaa nina wasiwasi kama ana hizo hisa kweli, maana mtu huwezi kutegemea return sawa kwenye uwekezaji wa viwango tofauti, hisa za NMB zilikuwa zikuzwa 4000 kipindi flani wakati hisa za CRDB zilikuwa zikiuzwa 400, obviously kwa idadi sawa ya hisa , uwekezaji wa NMB ndio utakuwa mkubwa zaidi ya wa CRDB na hivyo hata gawio la NMB litakuwa kubwa pia, huyu jamaa hajui hilo??
 
Nitakupuuza kwa sababu unaonekana unachangia ki ashki majnuni na sio kwa hoja.
Endelea na unavyoamini. Muda ukifika ndio utajua. Mimi naongea Kama mwana Hisa wa CRDB na mdau/mjumbe wa DSE.

Kama ni mwanahisa wa CRDB kwanini usipeleke hoja yako kwenye kikao cha wanahisa?
 
Mimi ninayo hisa 3500 katika CRDB na hisa 3500 ktika NMB. Leo nimepata taarifa kwenye simu ya ngu kuwa nimepata Tshs. 565,000 kama Gawio toka NMB lakini hisa hizo hizo kutoka CRDB nitapata Tshs.35,000. Naomba sana mnielekeze utaratibu wa kuuza hisa zangu za CRDB kwa sababu naona kama CRDB hawana nia na Wanahisa wao.
Hisa za NMB uliwekeza shilingi ngapi na hisa za CRDB uliwekeza shilingi ngapi kabala ya kuanza kuweka mlinganisho wa gawio?
 
Huyu jamaa nina wasiwasi kama ana hizo hisa kweli, maana mtu huwezi kutegemea return sawa kwenye uwekezaji wa viwango tofauti, hisa za NMB zilikuwa zikuzwa 4000 kipindi flani wakati hisa za CRDB zilikuwa zikiuzwa 400, obviously kwa idadi sawa ya hisa , uwekezaji wa NMB ndio utakuwa mkubwa zaidi ya wa CRDB na hivyo hata gawio la NMB litakuwa kubwa pia, huyu jamaa hajui hilo??
Sio kila mtu ana elimu katika masuala ya Hisa mkuu.
Cha muhimu ilikuwa ni kumpa elimu ambayo itamsaidia katika suala zima na baadae.
Kuna watu huwa wananunua Hisa ili nae akikaa kwenye Viti virefu aweze kujitamba kwamba ana Hisa za kampuni fulani, Ila kiuhalisia hata mwenendo wa kampuni husika haujui.
 
ACHA UPPUUZI HUJUI NMB NI YA MACCM NA CRDB NI YANAMAGEUZI. KAMA WEWE NI UPINZANI FATA UPEPO BASI ONDOKA CRDB KWANI WAPAMBANAJI TUTABAKI HUKUHUKU
hamna cha CCM wala upinzani mkuu,huyo jamaa hajui mambo ya hisa na gawio yanavyofanya kazi
 
Unajuaje kama sijapeleka!!??? Umepiga ramli!?

Usipanic,tunaelekezana tu. Kama umepeleka hakikisha unaungwa mkono na wanahisa wenzako. Kama unaona utendaji wa benki sio mzuri,ni jukumu lenu wanahisa kuhakikisha uongozi wa benki unabadilishwa hiki benki hiweze kufanya vizuri.
 
Kati yangu na wewe ni nani anapaniki hapa!?
Wewe unajua kwa nini CRDB imesitisha kutoa mikopo kwa sasa!? Anyways,tusichoshane na swaumu hizi. Siku njema.
 
Mkuu ungetuambia kwanza hisa moja ya Nmb thamani yake ni kiasi gani na CRDB ni kiasi gani kwa hisa maana hapa umetupa idadi ya hisa na si thamani yake.

Kama thamani ya hisa zote za kampuni hizi mbili ni Sawa basi ujue kwamba Nmb inaingiza faida zaidi kuliko CRDB maana hisa(share) ni sehemu ya mtaji na faida inayotokana na mtaji huo ndo hilo gawio (dividend)

Kwa hiyo moja kati ya factor kubwa itakayokusukuma wewe uwekeze katika kampuni fulani kwa kununua hisa zake ni kuangalia kama hiyo kampuni inaoparate kwa faida au laa ukilinganisha na makampuni mengine (sijui kama hichi ulikizingatia kabla ya kununua hisa zako)

Kwa hiyo kwa kukushauri nenda DSE utapata muongozo wa kuuza hisa zako
 
Similar Discussions

7 Reactions
Reply
Back
Top Bottom