Nalifagilia sana gazeti la mwananchi.

BIG X

JF-Expert Member
Nov 4, 2011
777
212
Najua kuna magazeti mengi mazuri na watu wanayapenda sana na mimi pia. Lakini hawa jamaa wa gazeti la mwananchi mi nadhani wamejipanga vizuri sana. Habari zao ni za uhakika na ukweli, Hazina upendeleo wa kisiasa, website yao inavutia na wanaupdate taarifa zao kila siku. kwa sisi ambao tupo nje ya nchi linatusaidia sana kutuhabarisha mambo kwa haraka. Kifupi siwezi kuanza siku yangu vizuri bila kupitia website yao. Kama kungekuwa na namna na uwezo wa kuwachangia ningefanya hivyo.

Hayo ni mawazo yangu.

Hongereni sana gazeti la mwananchi
 
... hata mimi nilikuwa na wakubali sana hadi siku walipotoka na "Zitto Kabwe kala chakula chenye sumu", huku ndani ya habari hiyo wakifafanua kwamba Zitto ameambiwa na daktari kwamba ana tatizo la "food poisoning". Niliwadharau kwa umaimuna wao wa kudhani kuwa mtu mwenye food poisoning ni yule aliyewekewa sumu kwenye chakula.Mbaya zaidi, kipindi hicho, zitto alikuwa kwenye mvutano na viongozi wenzake ndani ya chadema. Mpaka leo kuna baadhi ya watu wanaamini zitto alipewa sumu bagamoyo. Mwananchi hawakuwahi kukiri kupotosha jamii hata ufafanuzi ulipotolewa na wajuzi wa lugha ya kigeni na madaktari. Hii ni aibu, na hii ndio matokeo ya kuwaajiri wafanyakazi wa bei chee ambao hata hawajasomea uandishi wa habari na wengine wamesoma miezi michache, kuwa wanahabari, wakati kuna bachelors kibao za uandishi wa habari!
 
Najua kuna magazeti mengi mazuri na watu wanayapenda sana na mimi pia. Lakini hawa jamaa wa gazeti la mwananchi mi nadhani wamejipanga vizuri sana. Habari zao ni za uhakika na ukweli, Hazina upendeleo wa kisiasa, website yao inavutia na wanaupdate taarifa zao kila siku. kwa sisi ambao tupo nje ya nchi linatusaidia sana kutuhabarisha mambo kwa haraka. Kifupi siwezi kuanza siku yangu vizuri bila kupitia website yao. Kama kungekuwa na namna na uwezo wa kuwachangia ningefanya hivyo.

Hayo ni mawazo yangu.

Hongereni sana gazeti la mwananchi

Mimi karibia kila siku nasoma website yao. Hawako up to date hawa. Habari za jana unazisoma leo kwenye website yao.
They need to be UP TO DATE.
By the way USIJE UKAWA UMETUMWA UJE ULISIFIE GAZET HILI HAPA.......
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom