Nalia na gazeti la zamani Sanifu, Sani, Tabasamu, By Kingo, Bongo na kadhalika, kwani ni matajiri katika ulimwengu wa sasa wa katuni

matoto ya sasa hiv hata hayajui utamu wa zille garazet za sani na bongo.ndio nikijifunzia kusoma enzi hizo 1995- 6..
nashangaa sana wachora vibonzo wamekaa kuchora siasa tu na kudhihaki wat ambao ni kama baba zao
badala wajikite kwenye ku produce comic books kama nchi za nje vile mfano wa dc comics na kupata mabilion ya fedha
kweli tupo nyuma sana

Sent using Jamii Forums mobile app
Kizazi cha dhahabu kimeshapita, sasa hivi kipo kizazi kipya ambacho kimepoteza ubunifu
 
Hayo na magazeti maarufu ya burudani miaka ya 90s mpaka, kwa wakazi wa dar walikuwa wanaelewa sana hizo kitu huwaambii kitu gazeti moja linatuzwa linasomwa na mtaa mzima, unasoma kila siku story hazichoshi, kuna watu walikua maaraufu kuliko wanasiasa, kina kipepe, lodi lofa, mapun'go, bettina na zena..

Sent from my SM-G955F using JamiiForums mobile app
UNAMSAHAU SOKOMOKO
 
Walipo kwa sasa baadhi ya wahusika wa gazeti la Sani na Bongo.
Sokomoko ni mgonjwa wa ini sababu ya unywaji Sana wa pombe Yuko kwao kigogo,
Ndulakuwili alipigwa nusu kufa kwa Tabia zake za wizi na utapeli kariakoo sasa hivi anabeba mizigo mabibo sokoni.

Kipepe na Njomba Nchumali walinusurika kuliwa na simba na baada ya Hilo tukio wakasitisha shughuli za uwindaji na sasa ni wakulima.

Lodi lofa baada ya kuwa na majibu mabaya kwa watu na kwa traffic alishindwa kulipa mkopo wa gari hivyo alinyang'anywa na sasa hivi ni dereva wa gari za serikali, mdomo wake mchafu umeisha

Pimbi hajawai kuwa na bahati, katika kupata wanawake ambapo mara ya mwisho kafanyiwa fumanizi hotel ya legacy Sinza Akala kipigo na sasa hamna mkono mmoja,

Madengee alikataa shule babake akamfukuza nyumbani sasa hivi ni fundi masofa pale keko,

Zena na Betina wako segerea sababu ya ugomvi wap toka kipindi kile.
Mapung'o Golden Boy, baada ya team aliyokuwa anachezea mbeya kushuka daraja aliamua kuacha mpira na kurudi kwao kimbiji kuwa mvuvi.
 
Ni ngumu mno nimepite bila kucoment kwenye huu uzi aisee raha ya zile katuni asikwambie mtu tu tu katuni tamu.
Mazoezi ya zile timu born town na bush stars hayakuwa ya sayari hii na vile vimaneno vyao vya kutukanana wanspokabana uwanjani acheni tu..
Kifupi jama walijua kuchora, walijua kutunga hadithi, walijua kuchekesha
The way walivyokuwa wanawachora wale wanawake mhh
Ngoja niishie hapa tu ahsante mdau kwa kuturudishia memory yale majarida yameniathiri mpaka leo napenda catoon sana nikinunua gazeti naanza kusoma katuni kwanza stori zingine baadae au nafunga na gazeti kabisa
 
Walipo kwa sasa baadhi ya wahusika wa gazeti la Sani na Bongo.
Sokomoko ni mgonjwa wa ini sababu ya unywaji Sana wa pombe Yuko kwao kigogo,
Ndulakuwili alipigwa nusu kufa kwa Tabia zake za wizi na utapeli kariakoo sasa hivi anabeba mizigo mabibo sokoni.

Kipepe na Njomba Nchumali walinusurika kuliwa na simba na baada ya Hilo tukio wakasitisha shughuli za uwindaji na sasa ni wakulima.

Lodi lofa baada ya kuwa na majibu mabaya kwa watu na kwa traffic alishindwa kulipa mkopo wa gari hivyo alinyang'anywa na sasa hivi ni dereva wa gari za serikali, mdomo wake mchafu umeisha

Pimbi hajawai kuwa na bahati, katika kupata wanawake ambapo mara ya mwisho kafanyiwa fumanizi hotel ya legacy Sinza Akala kipigo na sasa hamna mkono mmoja,

Madengee alikataa shule babake akamfukuza nyumbani sasa hivi ni fundi masofa pale keko,

Zena na Betina wako segerea sababu ya ugomvi wap toka kipindi kile.
Mapung'o Golden Boy, baada ya team aliyokuwa anachezea mbeya kushuka daraja aliamua kuacha mpira na kurudi kwao kimbiji kuwa mvuvi.
Hahahah nimecheka mbaya daah hili gazeti nalikumbuka sana
 
Dah gazeti la Bongo lilikuwa sio mchezo, yale mastori ya mule ndani ni zaidi ya bongo muvi zote kombine hazifikii utamu hule, halafu kwa wale mabaharia tunaopenda unyamwezi lilikuwa gazeti letu sana, na stori yetu ya "msako wa mr x", gazeti lilikua na harakati za maisha nyingi sana. Halafu pale mbele kulikuwa na picha ya stori ya mwezi unakuta bonge mmoja la mdada kakamilika kila idara, halafu pembeni kuna bishoo mmoja matata sana si mchezo.
Dah Msako wa Mr X sijaumalizaga ila jamaa walikua noma sana
 
Dah gazeti la Bongo lilikuwa sio mchezo, yale mastori ya mule ndani ni zaidi ya bongo muvi zote kombine hazifikii utamu hule, halafu kwa wale mabaharia tunaopenda unyamwezi lilikuwa gazeti letu sana, na stori yetu ya "msako wa mr x", gazeti lilikua na harakati za maisha nyingi sana. Halafu pale mbele kulikuwa na picha ya stori ya mwezi unakuta bonge mmoja la mdada kakamilika kila idara, halafu pembeni kuna bishoo mmoja matata sana si mchezo.
Dennis Raymond Makete
 
Hahah ila Kapteni Mapungo alikuwa na mikwara sana Aisee

Mie nakumbuka tu yale mazoezi yao huku wamejifunga mawe miguuni.

Kilichokuwa kinanifurahisha ni yale maneno yake akiwa uwanjani ubabe juu ya ubabe.

Ukweli kuna vitu tunavimiss.
Mapungo alikuwa akionewa sana na Bob Mikwara
 
Walipo kwa sasa baadhi ya wahusika wa gazeti la Sani na Bongo.
Sokomoko ni mgonjwa wa ini sababu ya unywaji Sana wa pombe Yuko kwao kigogo,
Ndulakuwili alipigwa nusu kufa kwa Tabia zake za wizi na utapeli kariakoo sasa hivi anabeba mizigo mabibo sokoni.

Kipepe na Njomba Nchumali walinusurika kuliwa na simba na baada ya Hilo tukio wakasitisha shughuli za uwindaji na sasa ni wakulima.

Lodi lofa baada ya kuwa na majibu mabaya kwa watu na kwa traffic alishindwa kulipa mkopo wa gari hivyo alinyang'anywa na sasa hivi ni dereva wa gari za serikali, mdomo wake mchafu umeisha

Pimbi hajawai kuwa na bahati, katika kupata wanawake ambapo mara ya mwisho kafanyiwa fumanizi hotel ya legacy Sinza Akala kipigo na sasa hamna mkono mmoja,

Madengee alikataa shule babake akamfukuza nyumbani sasa hivi ni fundi masofa pale keko,

Zena na Betina wako segerea sababu ya ugomvi wap toka kipindi kile.
Mapung'o Golden Boy, baada ya team aliyokuwa anachezea mbeya kushuka daraja aliamua kuacha mpira na kurudi kwao kimbiji kuwa mvuvi.
Mapungo mbona mara ya mwisho alienda kusajiliwa Arsenal, aliunganishwa na Nwanko Kanu
 
20230726_111649.jpg
20230726_112817.jpg
20230726_113454.jpg
20230726_113807.jpg
 
Back
Top Bottom