Jamani nimewamiss! Nimejaliwa mtoto wa kiume yani mwenzenu niko bize hakuna mfano. Leo kidogo nimepata hizi dakika mbili nikaona niwakumbuke. Babake alipomwona tu nikamshangaa mwenzangu chozi linamlengalenga nikamwuliza vipi? Ati kisa kaona mwanae ana kidimpo kidevuni basi ndicho kimemliza anasema kimemkumbusha babake mzazi. Na kule kwa yule hakuna mtoto mwenye hicho kidimpo. Basi mie mwenzenu bichwa hilo!
Asanteni mlionitakia kheri. Siku nyingine tukijaaliwa nitaingia tena tushauriane hili na lile inshaallah lakini kwa leo naombeni tu niondoke mtoto mdogo sana huyu halafu sijazoea haya mambo. Byeee!
Asanteni mlionitakia kheri. Siku nyingine tukijaaliwa nitaingia tena tushauriane hili na lile inshaallah lakini kwa leo naombeni tu niondoke mtoto mdogo sana huyu halafu sijazoea haya mambo. Byeee!