TandaleOne
JF-Expert Member
- Sep 4, 2010
- 1,644
- 709
Ni UJINGA.,ndio ni ujinga maana hakuna neno jingine lenye kulieleza jambo lililofanywa kwa maksudi na watu na baadhi ya "wahariri" wa hovyo hovyo kupotosha juu ya kilichotokea katika kikao cha Kamati Kuu kilichofanyika juzi tarehe 3 Mei 2016.
Taarifa zilizoenezwa kuwa Kikao hicho kilivunjika, ama kulikuwa na majibizano na kutoafikiana ni taarifa za uongo MKUU na upotoshaji wa dhahiri uliofanywa na baadhi ya watu
USAHIHI wa yaliyotokea kwenye kikao hicho ni kuwa hakuna majibizano, wala kutoafikiana kwenye suala la KATIBU MKUU wala hakukuwa na hoja ya kujadili mrithi wa KATIBU MKUU kwani Katibu Mkuu yupo na hakuna kanuni, sheria ama desturi inayolazimisha kubadili Katibu Mkuu kwa wakati huu ambapo Chama kinaendelea na mchakato wa kukabidhi Uenyekiti kwa Mhe Magufuli.
Ni tabia mbaya na hakika sheria itafuata mkondo wake dhidi ya magazeti yaliyoandika taarifa hiyo ya upotoshaji kwa maksudi kabisa.
KIDUMU CHAMA CHA MAPINDUZI.