Nalamba shahada rasmi leo

Raia Fulani

JF-Expert Member
Mar 12, 2009
11,320
3,475
Wadau leo hii pamoja na wenzangu kama elf 5 hivi tunatunukiwa rasmi shahada zetu ndani ya mlimani city. Bila shaka mawazo pevu yanaongezeka ndani ya jf na jamii kwa ujumla
 
kaka Hongera sana nipo jirani na hapo naona mashamra shamra kwa kwenda mbele ila duh soko la ajira ni ngumu sana na wenzenu wa UDOM mkichanganyika ni balaa soko la Ajira lenyewe halipanuki ni lile lile tuu na Shule zetu zinafundisha ili mtu uajiriwe na si kujiajiri pagumu sana hapo mkuu
 
hongera sana..Bila shaka unatunukiwa shahada ya UZAMIVU..sio kama ile ya mtu fulani kule UDOM ya heshima
 
hongera sana mkuu, ni shahada gani hiyo ni vizuri useme unaweza kuwa unajadiliana na waajiri wako/watarajiwa hapa JF
 
Raia fulani, ni degree ya fani gani na ni ya kwanza, ya pili au ya uzamivu?

Hongera lakini kwa kuchukua hatua muafaka ya kujisomea na kupata degree yako.
 
Wadau nashukuruni kwa pongezi 'zenyu'. Ndo namalizia kijifunction hapa. Msihofu kuhusu ni gwanda la ngapi au mkozi upi. Tujenge jamii tu kwa taaluma tunazopata
 
Back
Top Bottom