PRODA LTD
JF-Expert Member
- Oct 20, 2016
- 1,005
- 1,333
Nalaani vikali kitendo cha Jeshi la Polisi kuzuia kikao cha ndani cha Mhe.Susanne Maselle (mbunge wa viti maalum Mwanza) kwa madai kuwa kuna watu walijipanga kufanya vurugu kwenye kikao hicho. Mi nadhani kitendo cha polisi kufika kwenye kikao na kuagiza kisimamishwe wao ndio wanakua wamevuruga kikao.
Yani Mh.Maselle ameitisha kikao halali, ametumia gharama kuita wajumbe, ametoa taatifa polisi na kuruhusiwa kufanya kikao. Ghafla wakati kikao kikiendelea wanavamiwa na Polisi na kuamriwa kuvunja kikao hicho haraka, halafu OCD anasema eti wamelazimika kufanya hivyo kwa sababu wamepata taarifa kuna watu wamejipanga kuvamia na kuvuruga kikao hicho.
Huu ni utetezi dhaifu mno. Watu gani wamejipanga kuvamia na kuvuruga kikao wakati polisi wameshavamia na kuvuruga tayari?
Anyway, hata kama polisi walipata taarifa kuwa kuna watu wamejipanga kufanya hivyo je dawa ilikuwa kuagiza kikao kisitishwe? Nadhani baada ya polisi kupata taatifa hizo walipaswa kuimarisha ulinzi kwenye kikao hicho kudhibiti hao watu waliojipanga kuvuruga kikao, lakini si kuzuia kikao kisiendelee.
Mkutano mkuu wa CCM Dodoma, Polisi walipata taarifa kuwa vijana wa Chadema wamejipanga kuvamia mkutano huo lakini mbona hawakuzuia mkutano? Badala yake waliimarisha zaidi ulinzi. Sasa kwanini Sumve wazuie kikao kilichokua kinaendelea kwa amani? This z double standards na ni ishara kuwa jeshi la polisi kuna mazingira linatumika kisiasa.
Nguvu ileile iliyotumika kulinda mkutano wa CCM usivurugwe huko Dodoma, ingetumika pia kulinda mkutano wa Mhe.Maselle usivurugwe huko Sumve. Lakini kumlazimisha Maselle afunge kikao, na kuamuru wajumbe kutawanyika eti kuna watu wamejipanga kuvuruga kikao hicho ni uonevu wa wazi. Ni vzr jeshi la polisi lijitafakari na lifanye kazi kwa weledi.
Jeshi kujiingiza kwenye mihemko ya kisiasa athari zake ni mbaya sn. Tuliyoyaona Nigeria, DRC, na Kenya yanatosha. Hatutaki yafike kwetu. Jeshi la polisi na majeshi mengine yatumikie raia wote kwa usawa. Wakianza ubaguzi, raia nao watalipiza kwa kufanya ubaguzi mitaani. Hali hiyo isipodhibitiwa mapema madhara yake makubwa. Mdharau mwiba mguu huota tende.!