Petro E. Mselewa
JF-Expert Member
- Dec 27, 2012
- 10,279
- 25,854
Askari aweza kuwa JWTZ,JKT,Magereza,Polisi,Uhamiaji,TISS na Zimamoto. Pamoja na utofauti wa majukumu wa askari hao,lengo la ujumla ni kulinda amani yetu. Amani huletwa na utulivu na kufuata sheria na taratibu. Usingizi wetu husababishwa na kukesha kwao. Askari ni tunu yetu.
Askari wamepewa, kikatiba, jukumu la kulinda amani kwa kulinda mipaka ya nchi,kulinda raia na mali zao na kuhakikisha sheria na taratibu zinafuatwa. Amani ni zao la majukumu ya askari. Amani ni zao la kuwajibika na kukesha kwao. Amani ni zao la kujitoa kwao kwa ajili ya nchi yao
Nikiwa ni mtanzania ninayefaidi matunda ya uwepo wa askari,nalaani mauaji ya askari yeyote awaye. Nalaani askari kubezwa au kutwezwa wakiwa katika kutimiza wajibu wao. Tunapaswa kuwalinda askari wetu kwa kuwafichua wanaowawazia au kuwapangia mabaya. Taarifa ziwasilishwe kwao mapema ili zifanyiwe kazi. Tuilinde tunu yetu: majeshi yetu ya ulinzi na usalama.