Nalaani matukio ya nguvu ya chuma, tunajitengenezea mazingira hatarishi kwa vizazi vijavyo!!!!

sammosses

JF-Expert Member
Jan 24, 2011
1,682
1,110
Tanzania inaongozwa na katiba ya Jamhuri ya Muungano ya 1977,katiba ambayo kwa utaratibu tuliojiwekea,viongozi wetu huapa kuilinda,kuisimamia na kuhifadhi,kwa maana ya kuishikilia kama mwongozo wetu.

Viongozi waliapa kufanya hayo hapo juu wapo,wamegeuka mabishoo wa kizamani kutembea wakiwa wamebeba video cassete VHR wakati nyumbani hawana televisheni set ya kutazamia hizo cassete. Viongozi wetu wanazunguka na katiba mkononi lakini maudhui ya mwongozo wa katiba wanayapuuza na kuyafumbia macho kwa kusimamia maslahi ya kikundi fulani.

Natafakari ni kweli hawaujui au ni kibri cha madaraka kinacholeta ulevi wa kupindukia wa madaraka!!!

Pamoja na mapungufu ya katiba hii,watawala wamekuwa wakiitumia kwenye mamlaka ya uteuzi kama mwongozo wao,lakini kwenye mambo yanayo tishia maslahi ya utawala wao wamejivika miwani ya mbao.

Tamko la rais kuzuia mikutano ya hadhara,si takwa la kikatiba. Soma sura ya kwanza mpk ya kumi ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano, hakuna takwa hilo,bali ni utashi na muono uliojaa hofu kwa mtawala akijilinda kwa kutoa matamko ya aina hii yanayo nyang'anya haki ya wanasiasa kufanya kazi,lakini yakitumiwa vibaya na vyombo vya dola kukandamiza misingi ya haki kwa mitulinga.

Ibara ya 14 ya katiba imesema"kila mtu anayo haki ya kuishi na kupata ulinzi wa maisha yake kwa jamii inayomzunguka kwa mujibu wa sheria

Ibara ya 15 kwa madhumuni ya kuhifadhi uhuru wa mtu binafsi na haki ya kuishi kama mtu huru hatakamatwa, kufungwa, kufungiwa, kufukuzwa au kupunguzwa uhuru wake ila tu

(a) chini ya matukio na kwa mujibu wa utaratibu unaoagizwa na sheria, au

(b) katika utekelezaji wa hukumu, ama au hukumu iliyotolewa au kupitishwa na mahakama baada ya uamuzi katika kisheria au hukumu kwa kosa la jinai.

Muktadha wa sheria umekuwa ukitafsiriwa vibaya katika maudhui ya kupoka zaidi haki kwa makusudi ya kulinda maslahi ya kikundi fulani ndani ya nchi yetu.

Hakuna asiyejuwa kuwa vyama vya siasa vinafanya siasa kwa mujibu wa katiba ya Jamhuri ya Muungano,hakuna asiyejuwa kuwa pamoja na tamko lake rais kuzuia mikutano ya hadhara,amekiuka katiba na kuyatumia madaraka yake vibaya kukandamiza vyama pinzani na kukiruhusu chama chake kufanya siasa na maandamano ya kumpongeza juhudi zake,ilihali akitumia vibaya mamlaka hayo hayo kudhibiti vitendo vya ukiukwaji wa haki unaofanywa na vyombo vya dola kuzuia wapinzani.

Ukisoma katiba ya Jamhuri ya Muungano hakuna ibara inayotoa matabaka ya kisiasa na hakuna mamlaka inayo idhinisha hisani katika kutumikia sheria za nchi kwa mujibu wa sheria.

Kitendo cha kuvamiwa akina mama wa CHADEMA kwa mabomu ya majozi wakiwa kwenye mkutano wa ndani,kimeipaka matope serikali hii inayojiita ya wanyonge. Na kimenyang'anya kwa makusudi ya kuilinda serikali ya CCM,katika kudhoofisha nguvu za vyama mbadala vya siasa.

Katiba yetu ya Jamhuri ya Muungano pamoja na mapungufu yake,imebainisha wazi katika ibara ya 20,kwa kutoa haki kama ifuatavyo;

20. kila mtu ana uhuru, kwa uhuru na kwa amani kukusanyika, kushiriki na kushirikiana na watu wengine, na kwa lengo hilo, kutoa maoni kwa umma na kuunda na kujiunga na vyama au mashirika yaliyoundwa kwa ajili ya kuhifadhi au kuimarisha imani yake au faida kwa maslahi mengine.

Kimsingi,utaona jinsi gani taifa linakosa hekima hata ile ya majadiliano kwa kutafuta suluhisho la hizi chuki zinazokuwa kama uyoga,badala yake vyombo vya dola vinatumia nguvu kubwa kuzuia mikutano.

Tukio la jana mkoani Simiyu si tukio zuri,linapingana kabisa na mkataba wa dunia wa amani wa kusimamia haki tuliosaini,lakini ina kanyaga mpango wa millennium wa kutoa fursa sawa kwa wote,na kuendeleza mfumo dume unaopingana na fursa sawa kwa wote.

Serikali chini ya Amiri Jeshi mkuu,imeshindwa kuzuia matukio haya ya nguvu ya chuma kwa Watanzania wenzetu,hali inayojenga dhana mbaya sana ya ubaguzi katika utendaji wa kila siku.

Ukiukwaji wa haki hizi hakuifanyi nchi kuwa salama zaidi ya kuchochea chuki,kutokuwa na imani na serikali na uvunjifu wa amani.

Ni bora utafutwe muafaka wa kitaifa,wanao onewa wapo kimya hatujui wanatafakari nini,na uvumilivu una kikomo,kabla ya kufikia huko tukae tutatuwe matatizo yetu,tusiige ubaya wa wenzetu ilihali sisi ndiyo tuliokuwa wakemeaji wa matukio yenye sura ya ubaguzi na wapatanishi(mediation centre),leo viashiria vyote vya kuichoka amani viko wazi,tubadilike.

#amaninitundalahakituacheuoga
 
mkuu walioleta suala la veting kwa viongozi wa ngazi za juu hawakuwa wajinga, suala hilo CCM kwa utashi wao walilipuza kwa masirahi ya wachache ie JK et al. Matokeo yake ndo haya tunayoyashudia kiongozi wa kitaifa kuwa sawa na kiongozi wa WCB ama Vijana wa UVCCM kimtazamo..poor my country.
 
Back
Top Bottom