I am Groot
JF-Expert Member
- Jul 20, 2018
- 3,726
- 10,020
Kampuni ya NALA MONEY Nala ya kijana Mtanzania Benjamini Fernandes imefungua rasmi ofisi yake ya kwanza Afrika, mjini Nairobi nchini Kenya.
Ufunguzi wa ofisi hiyo uliambatana na utiaji saini mkataba wa kibiashara kati ya NALA na benki ya Equity nchini Kenya ili kuwawezesha Watu kutuma fedha kutoka Uingereza na Marekani kwenda Kenya kwenye akaunti za Safaricom, Airtel pamoja na benki.
“Ninafuraha sana kwa hatua hii nyingine ya mafanikio kuweza kuwa na ofisi yetu ya kwanza Afrika nchini Kenya pamoja na kuendelea kuwa na ushirika wa kibiashara na benki ya Equity, hii itazidi kutusaidia kuendelea kutoa gharama nafuu, haraka na salama zaidi kwenye utumaji fedha kwa Watu waishio ughaibuni” amesema Benjamin.
Kampuni hii inamiliki APP inayopatikana kwenye google play store na apple store ambapo sio Kenya pekee bali hata Watanzania walio nchini Marekani na Uingereza wanaweza kuitumia kutuma pesa Tanzania kqa gharama nafuu na haraka.
Chanzo: Millard Ayo