Nakwenda Same kuchukua Jimbo-Mama Kilango Ameshindwa kusukuma Maendeleo | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nakwenda Same kuchukua Jimbo-Mama Kilango Ameshindwa kusukuma Maendeleo

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by kinepi_nepi, Jul 28, 2012.

 1. kinepi_nepi

  kinepi_nepi JF-Expert Member

  #1
  Jul 28, 2012
  Joined: Aug 16, 2007
  Messages: 870
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Baada ya kufanya tathimini na kuzunguka jimboni na kuona hali ya maendeleo na maisha ya watu nimejua watu wangu wa Same wanakosa uongozi wenye uthubutu wa kuwasaidia.

  Jimbo lenye mbuga za wanyama, aridhi yenye rutuba, mikondo ya maji, hali ya hewa safi. Linakosa maendeleo , limedidia kielimu, ajira hakuna na viongozi wanalalamika.

  Mazao ya biashara kama kahawa, viazi, iliki, mbao,miwa, mboga, maziwa, nk na maeneo ya utalii yangetumiwa vizuri wilaya ingeweza kuwa na ajira za kutosha na kukaribisha hata wahamiaji kutoka wilaya na mikoa mingine.

  Ubovu wa mawasiliano hasa barabara ndio chanzo kikubwa sana kinachozorotesha maendeleo.

  Wananchi wako tayari kuchangia maendeleo yao ila wamekosa wasimamizi wazuri au viongozi wakazi. Huwezi kuwa kiongozi kwa Remote, matatizo husika hayakuhusu wala hujali. Leo Jimbo linamatatizo makubwa ya maji na huduma za afya.

  2015 naelekea dodoma kuwasaidia wananchi wangu. Nitahakikisha fungu letu kutoka dodoma linafika Same na kutumiwa kama lilivyopangwa. Mapato ya ndani ya jimbo yatatumika kama makusudio yake na kusaidia kuvutia wawekezaji wa ndani ya jimbo na nje ya jimbo, bila kusahau kuwekeza kwenye utalii wa ndani na nje ambao utatuongezea mapato na ajira.

  2015 Same lazima irejee kwenye mashindano ya elimu na kuwa kimbilio la watanzania kupata elimu bora inayoendana na mshindo wa kisasa wa teknolojia. lazima Same iwe na vyuo vya ufundi, chuo kikuu na hospitali kubwa ya chuo kwa ajili ya kusomea na kusaidia wakazi wake.

  Nataka huduma muhimu zipatikane same badala ya sasa huduma nyingi zinawafanya wananchi wasafiri. Kweli leo mwalimu anatakiwa kusafiri kufuata mshahara???

  Kwa sasa tunawakaribisha wote wadau wa Same kuelekeza nguvu kubadili uongozi wa same ili kuijenga Same yenye nuru na maisha yenye maana na kuheshimika.

  Tuanze leo Tuanze sasa
   
 2. DALLAI LAMA

  DALLAI LAMA JF-Expert Member

  #2
  Jul 28, 2012
  Joined: Jan 31, 2012
  Messages: 8,617
  Likes Received: 401
  Trophy Points: 180
  Ingia kwa jina lako tukutathmini.
   
 3. m

  mtendaji wa kijiji JF-Expert Member

  #3
  Jul 28, 2012
  Joined: Jul 3, 2012
  Messages: 539
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 35
  Tupia jina hapa
   
 4. WA-UKENYENGE

  WA-UKENYENGE JF-Expert Member

  #4
  Jul 28, 2012
  Joined: Oct 1, 2011
  Messages: 2,904
  Likes Received: 227
  Trophy Points: 160
  Weka CV yako mkuu tupate sehemu ya kuanzia!!
   
 5. Mbaha

  Mbaha JF-Expert Member

  #5
  Jul 28, 2012
  Joined: Nov 26, 2010
  Messages: 697
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Wewe unaonekana hata same wenyewe huijui! Huwezi kutaja mazao ya biashara ya same bila kutaja tangawizi na mpunga! Wewe ni wa same kweli?
   
 6. m

  mwabakuki JF-Expert Member

  #6
  Jul 28, 2012
  Joined: Jun 2, 2011
  Messages: 268
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  kwa hiyo kaka unaitwa Kinep nepi..hongera..na kilavlav kheri
   
 7. The Fixer

  The Fixer JF-Expert Member

  #7
  Jul 28, 2012
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 1,361
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 135
  Daaah, Umeniwahi sana huyu Mbunge mtarajiwa hapajui Same - Mashariki kwa Anne Kilango ila amefanya overall ya namna alivyosimuliwa Same ilivyo. Ameshashindwa kabla ya kuanza !
   
 8. MNYISANZU

  MNYISANZU JF-Expert Member

  #8
  Jul 28, 2012
  Joined: Oct 21, 2011
  Messages: 7,056
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 145
  Usiwe kama Zitto, huu ni muda wa kukiimarisha chama kwanza.
   
 9. C

  CHIEF MVUNGI Senior Member

  #9
  Jul 28, 2012
  Joined: Apr 6, 2012
  Messages: 100
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Sijapata kuona wapare wajinga kama hawa wanaodanganywa na huyu mwanamke Kilango kwanza ni mnafiki anajifanya kufoka kisha anaunga mkono mia ya mia, mimi navyojua wapare wajanja kwann mnadanganywa tena na mwanamke?
   
 10. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #10
  Jul 28, 2012
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Kile kilimo cha Tangawizi alicho ahidi wanasame kuwajengea kiwanda vp kimesha tengemaa?
   
 11. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #11
  Jul 28, 2012
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,330
  Likes Received: 19,496
  Trophy Points: 280
  yule mama kala hela ya kiwanda ...William anajua zaidi
   
 12. MANI

  MANI Platinum Member

  #12
  Jul 28, 2012
  Joined: Feb 22, 2010
  Messages: 6,409
  Likes Received: 1,862
  Trophy Points: 280
  Mjomba lakini kwa nini mnammezea si mumlipue !
   
 13. kinepi_nepi

  kinepi_nepi JF-Expert Member

  #13
  Jul 28, 2012
  Joined: Aug 16, 2007
  Messages: 870
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Asante !
  Kutokutaja haina maana siijui ninachosema sio mpunga tu na tangawizi sikuvitaja kuna mengi sana sikueleza ningeeleza ingekuwa page ishirini au zaidi.

  Same ni jimbo zuri sana lenye mengi ya kuweza kulifanya liwe jimbo tajiri sana kati ya majimbo tajiri Tanzania, kilimo cha mpunga ambacho Ndungu ndichokilinendelezwa kina sua sua sana na kihurio ambapo bado sehemu kubwa inaukosefu wa maji baada ya vyanzo vya maji kwenye mlima shengena kuanza kuharibiwa.

  Ukanda wa kuanzia kisiwani, Gonja Maore Ndugu na kihurio ndio ukanda wenye uwezo wa kilimo cha tambarare. Ukanda wa juu ndio ulikuwa unatoa ndizi, viazi, kahawa, tangawizi, iliki, vitunguu, mboga nk.

  Badala ya kubishana ni vyema tungeelimishana na kuweka bayana matatizo na masuluhisho ili mbunge wenu aweze kuwa na yakuyafanyia kazi 2015 mara baada ya kuapishwa. naomba ikumbukwe ninataka kuwa mbunge wa watu, wawapiga kura tufanye kazi pamoja kutokomeza umasikini na ndiyo tunaweza, tuache siasa za ubabaishaji.

  Asante hata kushindwa ni kuanza. Jimbo letu limetelekezwa. Mama Anne kilango ameonyesha uwezo mdogo sana inawezekana anastaili ya Chdeli Mgonja. Wabunge wengi wa jimbo la same wameshindwa kabisa kuliendeleza jimbo hili. Mama mziray alishindwa akaja yona akashindwa sasa mama yetu naye kashinwa. Sababu kubwa wamehama jimboni na wamelowea mijini na kuja huku kutuangalia kama wanyma wa zuu.

  Ni vyema ungesaidia sehemu niliyoshindwa na wapi Kilango ameweza.

  Kiwanda kilikuwa kinajengwa Mamba Miamba kwa wale waliosoma Parane nafikiri wanapakumbuka kwani sio mbali sana na Parane. Kiwanda kile hakieleweki kwani kinatajwa na kuguswa wakati wa kampeni. Uongozi wakati wa kutafuta haufai sio kwa same tu bali kwa Tanzania nzima. Ule ni utapeli tu.

  Matatizoya jimbo la same ni makubwa na kwa kiasi kikubwa ni yakutengenezwa na viongozi wa wiwlaya, wabunge na uongozi wa serikali. Wote wako likizo hakuna anayejali. Juzi nilikuwa na madiwani Same kwenye kikao chao cha madiwani kwa asilimia kubwa wanapokea tu hizo posho bila kujua wanafanya nini.

  Wito lazima kwanza kuchagua madiwani anagalau wenye uwezo na kujua kwa nini wanataka udiwani, kati ya vigezo elimu lazima izingatiwe. Nitataka kufanya kazi na madiwa wenye uelewa, ujuzi na uwezo wa kutambua na kutoa suluhisho la matatizo na maendeleo. sitataka kufanya kazi na madiwani njaa tumbo.

  Kazi hii ni kazi ya wapiga kura kwani ndio watakaonichagua mimi na madiwani wetu. Ningeomba tujadili uvumbuzi wa matatizo ya Same .

  Barabara karibu zote za Same ukiacha barabara ya same-makanya-saweni-hedaru mkomazi amabayo ni barabara ya Taifa ndio yenye lami. Barabara zingine zote vumbi na wakati wa mvua hazipitiki.

  Barabara ya Mkomazi-kihurio-ndungu-gonja -kisiwani -same tumehadiwa lami nakumbuka tangia mwinyi-mkapa na hatimaye JK ila stori ni zile zile.

  Anna kilango ni mwenyeji wa kihurio lakini sidhani kama hata anashtuka.

  Jimbo zima lina hospitali moja tu ya serikali (Same mjini na bombo Gonja ambayo ni hospitali ya kanisa ) ambazo hazina uwezo mkubwa wa kututibu kazi yake kubwa ni rufaa.

  Vi zahanati vilivyopo kama vile vya misheni bwambo ambacho ndicho kinategemewa na wakazi wa mamba miamba-kirangare, Mpinji, changuluwe na sambweni nk hakina uwezo na ni cha kanisa. Kizahanati cha serikali kilichopo mamba miamba ni choka mbaya.

  Ukienda Ndungu na kihuria taabu hizo hizo. Mbaga kisiwani balaa miaka hamsini ya uhuru. Barabara zote za juu milimani hazipitiki wakati wa mvua. shule za sekondari za kata zinakosa waalimu na kukusanya yeyote.

  Tunahitaji mbunge atakayeweza kuunganisha wilaya na serikali na kuhakikisha fedha za walipa kodi zinatumika kama inavyotakiwa na kuwa mbunifu kuongeza pato la jimbo ili kutatua kero nyingi za kutengeneza ndani ya jimbo la Same.
   
 14. Kamende

  Kamende JF-Expert Member

  #14
  Jul 28, 2012
  Joined: Mar 1, 2008
  Messages: 415
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Kama uko serios. Wasiliana na viongozi wa Chadema wa mkoa wa Kilimanjaro.

  Nichukue nafasi hii kukuhakikishia kwamba jimbo liko wazi. CCM Same ni wepesi mno. Anna Kilango ndo mweupe kabisaaaa!
  Njoo tukuonyeshe an obvious path to victory over Same East.
   
 15. b

  bangusule Senior Member

  #15
  Jul 28, 2012
  Joined: Feb 9, 2008
  Messages: 185
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  kinepi-nepi,

  kila la heri katika harakati za kulikomboa jimbo la Same Mashariki na wilaya ya Same kwa ujumla. hakuna shaka yoyote kwamba mama anna kilango kazi imemshinda na yuko bungeni kujinufaisha yeye binafsi. baadhi yetu tulilitambua hilo mapema ila wako wengi waliodanganyika na makelele ya mama kilango wasimjue kwamba ni TAPELI mzoefu.

  baada ya kupiga makelele bungeni kwamba anapinga mradi wa uchimbaji bauxite ktk msitu wa shengena, sasa mama kilango amepokea kitu kidogo, na amewageuka wananchi. gazeti la raia mwema wamemnukuu anna kilango akidai kwamba zile VIDEO alizotengeneza na kutishia kuziwakilisha bungeni ilikuwa ni kwa ajili ya "political management" tu, ili wapinzani wasiichukue hoja ya uharibifu wa mazingira ktk msitu wa shengena.


   
 16. Freema Agyeman

  Freema Agyeman JF-Expert Member

  #16
  Jul 28, 2012
  Joined: Mar 3, 2011
  Messages: 3,282
  Likes Received: 1,432
  Trophy Points: 280


  Hijajifunza toka kwa Zitto na iisue yake ya Urais?
   
 17. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #17
  Jul 28, 2012
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,330
  Likes Received: 19,496
  Trophy Points: 280
  kaka kuan hii page hapa(https://www.facebook.com/samemashariki) ..tuwasiliane vizuri tujue jinsi ya kuiendesha ..nakutakia kila la heri ..kama unataka taarifa zote kuhusu kile kiwanda cha tanzawizi nenda pale miamba wale wazee watakupa taarifa zote
   
 18. kinepi_nepi

  kinepi_nepi JF-Expert Member

  #18
  Aug 7, 2012
  Joined: Aug 16, 2007
  Messages: 870
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Kamende Asante sana, kama ilivyo mwaka 2015 ni mwaka wa kukomboa wananchi wa Same na nitawatafuta viongozi wetu jimboni na nitakutafuta mkubwa.

  Asante sana mkubwa wazee wa miamba nimeongea nao sio wote ila matatizo ni makubwa zaidi ya kiwanda cha miamba. Tuwasiliane mkubwa kufikia maendeleo ya kweli.
   
Loading...